Siku hayati Magufuli aliposimama imara kutetea wamachinga, mbele ya Samia

Siku hayati Magufuli aliposimama imara kutetea wamachinga, mbele ya Samia

Hili swali ni vyema iulizwe serikali,ila kwa kiufupi ni kwamba barabarani siyo sehemu sahihi ya kufanyia biashara-Barabara ina matumizi yake sahihi yaliyo-ainishwa kisheria.
images (2).jpeg
 
Mswaada ungepelekwa Bungeni ili kufuta matumizi ya Barabara za mijini kwa magari na vyombo vingine vyenye kutumia Barabara pamoja na sehemu za waenda kwa miguu

Ili kwamba iwe halali kwa Wamachinga kuchuuza bidhaa zao Mabarabarani bila bugudha.
 
Kwenye nchi isiyoweza kuajiri wahitimu wa elimu ya upili, vyuo vya kati na vyuo vikuu, wamachinga mama lishe na bodaboda ndizo sekta inayomeza wale waliokosa ajira na wakang'ang'ania mijini. Kuwanyanyasa hawa ni kuwakumbusha ukosefu wa ajira..
Kwanza serikali iwathamin sana kwa kujiajiri kwani wanapunguza uhalifu, ukahaba ombaomba umasikini na utegemezi kwa ujumla
Pili si kweli kwamba hawalipi kodi kwani bidhaa hawanunui? Na kama hawalipi kodi basi maana yake shida iko kwa wafanyabiashara wanaowapa bidhaa
Pili ni jukumu la serikali kutengeneza mfumo utakao watambua na kuwawezesha kulipa kodi
Mwisho kundi hili ni tabaka la vijana wenye nchi, wapiga kura, wenye uwezo wa kufanya mabadiliko hata kwa nguvu. NI MTAJI WA KISIASA.
Wote wanashabikia kuondolewa wamachinga kiholela ana lengo la kisiasa... Na watageuka mbelen. Niwakumbushe wakati wa JK wapinzani wote walitaka nchi iwe na national carrier shirika la ndege. JPM alipoingia akaubeba ule ushauri akawekeza ATC na baadae wakatafuta visingizio wakamgeuka.
 
Mbona watu wanajitoa ufaham kuhusu hiyo hotuba? Jamaa anasema watengewe na kuwekewa miundombinu rafiki ndio waondolewe.
Hapa mjadala ungekua utekelezwaji wa hilo agizo la kuwawekea miundo mbinu sasa. Linawezekana na kutekelezeka?
 
Ye ndo aliwatengeza baada ya kuuwa sekta binafsi zilizoajiri vijana, kwa kuwabambika kesi matajiri, ikiwemo kuwafilisi wakakimbia nchi wakafunga biashara watz wakakosa ajira ikawalazimu kuzagaa barabarani akaona fursa akawatumia kisiasa
 
Na wewe unaunga mkono wakapange biashara hata kwenye mlango wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya? Hilo litakuwa ni Taifa la namna gani? JPM anafahamika alikuwa mtu wa kupenda sifa za hovyo hovyo especially kutoka kwenye makundi ya watu wenye uelewa mdogo katika jamii
Achana nae huyu! Chuki zake dhidi ya Samia na ukabila wake zinamfanya ajitoe ufahamu humu siku hizi!
 
Wavuvi wanalipa kodi?
Wakulima wanalipa kodi?
Wafugaji wanalipa kodi?

Mnachekesha na vijisababu vyenu 😂😂
Pia kikubwa kwa jamii yoyote iliyostaarabika huwezi jenga barabara na kuanza kuitumia kama soko!! Wote tunaonekana hamnazo!! Halafu watu wanapita barabarani na kugongwa
 
Serikali ya ccm imeshindwa kwenye suala la ajira,ni uonevu kuwaondoa machinga pasipo tengeneza kwanza mifumo ya uzalishaji Ili vijana warudi kwenye uzalishaji na sio kuwa wachuuzi na madalali wa kuuza bidhaa za viwanda vya China na kukuza uchumi wa china.
Mkoloni aliweza maliza tatizo la ajira nchini kwa raslimali hizi hizi ambazo serikali ya ccm ni kipofu kuzitumia.
 
Bado sijaona sababu ya msingi kabisa ya kuwaondoa wamachinga barabarani.

Kama wanaziba njia na wanakaa kwenye mifereji ilo linazungumzika na inawezekana kuwasogeza sio kuwafukuza kama mbwa. Hii nchi ni ya kila mmoja.

Kuna watu nimeona wanasema nchi za weupe hakuna wamachinga....nawaambia watembee waone kuna nchi wamachinga mpaka kwenye reli.
Treli ikitaka kupita inawasubiri waondoshe bidhaa?
Jamani uongo mwingine!
 
Serikali ya ccm imeshindwa kwenye suala la ajira,ni uonevu kuwaondoa machinga pasipo tengeneza kwanza mifumo ya uzalishaji Ili vijana warudi kwenye uzalishaji na sio kuwa wachuuzi na madalali wa kuuza bidhaa za viwanda vya China na kukuza uchumi wa china.
Mkoloni aliweza maliza tatizo la ajira nchini kwa raslimali hizi hizi ambazo serikali ya ccm ni kipofu kuzitumia.
Hawaondolewi wanapangwa sehemu stahiki watambuliwe na sio kusababisha usumbufu kwa wafanyabiashara wenzao ambao kodi zote stahiki wanalipa
 
Rais Magufuli alikuwa na SAUTI YA KIMAMLAKA hii Mungu huwazawadiwa viongozi wachache sana.

Tanzania ilikuwa inamuhitaji bado Rais Magufuli kuliko yeye alivyoipenda nchi yake na kuitumikia kwa moyo mmoja.

Narudia

Tanzania ilipoteza kiongozi makini sana ila hatujui Mungu alikuwa na mpango gani,ALITUWEZA na ukweli utabaki kuwa hivyo.
 
Na wewe unaunga mkono wakapange biashara hata kwenye mlango wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya? Hilo litakuwa ni Taifa la namna gani? JPM anafahamika alikuwa mtu wa kupenda sifa za hovyo hovyo especially kutoka kwenye makundi ya watu wenye uelewa mdogo katika jamii
Wewe hujui kitu kabisa....JPM alikuwa anafahamu Hali halisi ya maisha ya mtu wa kawaida...JPM aliagiza machinga wawekewe utaratibu mzuri na siyo kwenda kumwaga bidhaa zao Kama utawala wa makaburu...Nadhani wewe ni miongoni mwa wapotoshaji wakubwa au huelewi namna watu wanavyoteseka kimaisha...kumbuka machinga wa Sasa ni tofauti na wale wa miaka ya nyuma...kwenye umachinga wa Sasa wapo waliofika vyuo vikuu na wenye elimu ya sekondari waliokosa ajira...wako kwa maelfu na maelfu nchi nzima mijini na vijijini...Nyie endeleeni kushabikia ujinga unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Sasa wa serikali ya awamu ya sita...mtakuja kujuta..pale vurugu zikitokea kwa magari kushambuliwa, ofisi kuchomwa Moto na maduka kuunguzwa sijui mtajificha wapi...siyo kwamba mtu anapenda kutandaza bidhaa barabarani anafanya hivyo ili apate chochote kuilisha familia na kusomesha watoto wake...eti Sasa mtu anakuja kukanyaga bidhaa hizo ambazo mtaji wake labda ni sh. 40 elfu tu....Mimi kamwe siwezi kushabikia dhuluma, ujinga na upumbavu wa Aina hii...ni unyama kwa kweli...Sasa ipo baadhi ya mijitu ndani ya serikali ya Sasa inadhani huu ndio wakati wa Kula...inafanya vitendo vya hovyo San wea ambavyo vinamchonganisha Raise na wananchi...Hivi Sasa Mama hazungumzwi vizuri mitaani kwa sababu ya mijitu iliyoko madarakani inayofanya vitendo vya kinyama kabisa...Mijitu hi nadhani imeamua kumhujumu Rais.....upo wakati Mama anasema nendeni mkakae vizuri na wamachinga na kuweka utaratibu mzuri yenyewe yanaziba masikio na siku ya pili yanaanza kubomoa vibanda huko vingunguti na kwingineko...hovyo kabisa...
 
Back
Top Bottom