Siku hayati Magufuli aliposimama imara kutetea wamachinga, mbele ya Samia

Maamuzi ya Magufuli kwa suala la wamachinga hayakuzingatia sheria,it was temporary and cheap popularity.

Uvunjifu wa sheria unaweza kuleta nafuu bandia na ya muda tu kwa kundi linalofaidika. Bali uhalisia unapofuatwa matokeo ni maumivu na kilio.
 
Maamuzi ya Magufuli kwa suala la wamachinga hayakuzingatia sheria,it was temporary and cheap popularity.

Uvunjifu wa sheria unaweza kuleta nafuu bandia na ya muda tu kwa kundi linalofaidika. Bali uhalisia unapofuatwa matokeo ni maumivu na kilio
 
Mnawapigia kelele machinga watoke bara barani ili mpitishe magari yenu, yes mpo sahihi lakini kumbukeni kuwa kuna watu hawana ajira na wanafamilia, wanategemea wauze magazeti, wauze mahindi ya kuchoma bara barani walishe familia

Kifupi ajira nchini ni janga kubwa kwa Taifa, wanaofukuza leo hao machinga wanasahau kwamba nao wamewahi kuwa machinga either kwa kuuza vitumbua/maandazi, pipi, sigara, bazoka n.k. kabla hawajafika hapo walipofika! Leo ndo wamekuwa wanyanyasaji wa wenzao. Ajira za serikali nchi nzima ni 750k Na binafisi ni 2.85m sasa hao Watanzania 58m nani atawaajiri nani atalisha familia zao kama sio kwa njia ya Umachinga kujipatia ridhiki ili kusogeza siku?! Leo Mtanzania anamnyanyasa Mtanzania mwenzake kisa anahadhi ya kukaa kwenye V8 kashasahau alikotoka.
 
Hakuna freedom isiyo na mipaka
 
kwan mkuu wa wilaya yeye ni nan? an uspecial gan mpk watu washndwe kufny biashara kisa yeye? haya matabaka yenu yakipuuz ndyo yanayowafany watu wapende kukwepa kulpa kodi ili kuikomoa serkal, pia waone siasa ndpo sehem ya kuchumia mali, badala ya kufny kazi....acha ubaguz
 
Mkuu falsafa ya mmachinga ni ngumu kuliko unavyoiongelea humu jukwaani. Uwepo wao umesababishwa na kifo cha viwanda vingi vilivyokuwa vimeajiri maelfu ya nguvu kazi.

Watu 15 waliotoka kufanya kazi kiwanda fulani wanakwenda kupata mtaji wa aina moja na wanauza vitu vya aina moja, matokeo yake wote wanafilisika kwa wakati mmoja!. Ni aina fulani ya ugangaji wa njaa usio na uhakika wa kesho itakuwa vipi.

Nawaonea huruma nikiamini suluhisho ni ufufuaji wa viwanda vingi huko mikoani. Mama Samia akiwa anatekeleza muelekeo mpya na aanze kuufikiria upya uwepo wa mtaji mkubwa utakaowainua wamachinga. Vinginevyo ni jeshi linaloongezeka na lenye mwisho wenye kukatisha tamaa.
 
Nchi. Hii bwana,ajira hakuna,watu wameajiajiri kwenye umachinga,badala ya Serikali kuwatafutia utaratibu mzuri wa kufanya biashara,serikali inawafukuza kama inatoa kinyesi,sasa mnawafukuza waende wapi?waishi vipi?
 
Kila miundombinu iliwekwa kwa kazi yake maalum, so wewe unafurahi wamachinga kuziba barabara, njia za watembea kwa miguu, mitaro ya maji, kupanga biashara zao mbele ya maduka ya watu, kutumiwa na wenye maduka kuwauzia bidhaa zao ili kukwepa kodi?? Huo ni ujinga!! Utaratibu wanaowekewa hawautaki, wanataka wabembelezwe, wao ni akina nani hasa hadi wabembelezwe kwenye hii nchi? Kuna makundi mengi tu nchi hii na hayabembelezwi, wao ni akina nani haswa?? Serikali makini haiwezi kuogopa kufanya jambo sahihi kisa eti watu watafanya vurugu, ni serikali dhaifu na iliyofeli tu ndiyo itaogopa kufanya maamuzi sahihi!! Waambie wafanye hizo vurugu zao then watajua nini maana ya mamlaka!! And sidhani kama kiongozi anayejiamini ataogopa kuwa unpopular kwa ajili ya kufanya maamuzi sahihi, viongozi wasiojiamini pekee ndiyo huwa wanapenda kuwatumia watu kama machinga kusaka sifa za kijinga...
 
Waruhusu waje wapange bidhaa na mlangoni kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…