chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Hamna aliyesema wafukuzwe kama mbwa..waondolewe barabaraniBado sijaona sababu ya msingi kabisa ya kuwaondoa wamachinga barabarani.
Kama wanaziba njia na wanakaa kwenye mifereji ilo linazungumzika na inawezekana kuwasogeza sio kuwafukuza kama mbwa. Hii nchi ni ya kila mmoja.
Kuna watu nimeona wanasema nchi za weupe hakuna wamachinga....nawaambia watembee waone kuna nchi wamachinga mpaka kwenye reli.
Afadhali hao wanafanya uzalishaji kuliko hawa machinga hawazalishi chochote..wakawe wakulima, wavuvi wazalisheWavuvi wanalipa kodi?
Wakulima wanalipa kodi?
Wafugaji wanalipa kodi?
Mnachekesha na vijisababu vyenu [emoji23][emoji23]
Thanks Mama D....uko sahihi Sana kwa. andiko lako hili....sisi wengine tumebahatika kuona awamu zote zauongozi wa nchi hii..kwangu Mimi baada ya Nyerere kiongozi anayefuatia kwa mikakati ya dhati kwa nchi yake na hasa maendeleo ya watu wake ni JPM...this man was a true son of Tanzania and Afrika....Binafsi huwa namfananisha na Thomas Sankara aliyeuawa kwa mbinu za kijasusi za ufaransa...JPM alikuwa anaipenda nchi hii kwa dhati...ila yeye mwenyewe alijua asingedumu kwa muda mrefu na ndiyo maana alikuwa anasema amejitoa mhanga...mabeberu siku zote hawako tayari kumuona kiongozi wa nchi ya dunia ya tatu na mwenye msimamo Kama wa JPM...ndiyo maana viongozi Kama Chavez, Sankara, Ghadafi, Lumumba na wengine waliuawa...
Tanzania tulibahatika kuwa na JPM na itachukua miaka mingi TZ na Afrika kumpata Kama yeye....
Hilo ni soko, na ni baadhi ya maeneo tu, huku hadi City Center machinga wamefurika
Bongo kuna njia za waenda kwa miguu!!! Labda huko kwenu masaki.Fanyeni biashara kwa kufuata taratibu zilizowekwa na sio kufanya biashara kwenye mitaro na njia za waenda kwa miguu
Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Warudi walikokua kabla, wote wale walioko mabarabarani wana meza zao katika masoko na minada, wameziacha wamezikodisha kwa machinga wengine, hivyo hakuna ambae hana pa kwenda, hata hivyo si jukumu la mamlaka kuwatafutia mahali pa kuenda , sababu hapo walipo siyo mahali sahihi na ni kinyume na taratibu za mipango miji.Serikali isikwepe wajibu wake, kama haiwezi kutafuta permanent solution basi itafute temporary solution. Hawa watu wanafukuzwa wanaenda wapi?
Nani kasema wanatofautiana? Waguse wamachinga isivyo halali uone muziki wake !Kumbe hata Mwendazake aliona kwamba wamachinga wanahitaji kuwekewa utaratibu mzuri ndio wahamishwe. Ndio agizo la Mama Samia pia. Hawatofautiani.
Jifunze kuishi bila mwendazake. Kila nabii na zama zake ndugu.
Siweki neno:
Lakini ukitaka kujua kwa nini wamachinga walimlilia sana, kujitokeza kwa wingi njiani kumzika ni hii hapo juu
Hata Rais wa awanu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akisoma Tanzia yake huko Chato, alimsifu Hayati kwa kutowasumbua wamachinga kwenye utawala wake!
Wamachinga wanatafuta hela ya kula, Wasaidiwe kwa kujengewa miundombinu kwanza na siyo kufukuzwafukuzwa kama mbwa
Huko kwa weupe ni kwao, ndio maana hata Mkuu wao kasema tusijifananishe nao kwa kutoa mfano wa coca cola.Bado sijaona sababu ya msingi kabisa ya kuwaondoa wamachinga barabarani.
Kama wanaziba njia na wanakaa kwenye mifereji ilo linazungumzika na inawezekana kuwasogeza sio kuwafukuza kama mbwa. Hii nchi ni ya kila mmoja.
Kuna watu nimeona wanasema nchi za weupe hakuna wamachinga....nawaambia watembee waone kuna nchi wamachinga mpaka kwenye reli.
Taratibu zimewekwa na lazima ziheshimiwe ...bila shaka hta hpo unapoishi kuna choo na sio kila sehemu panatumika kujisaidiaBongo kuna njia za waenda kwa miguu!!! Labda huko kwenu masaki.
Acha unaaAu km hawawez wahamie Burundi ... Au vipi mwenye nchi????
Rudi shule utoe umbumbumbu...kwani machinga si wanalipia vitambulishoLabda utakuwa unaishi Afghanistan wewe... Huwezi kuvua bila leseni, mkulima kuna ushuru wa mazao kwa gunia ukipeleka sokoni, mfugaji ukipeleka mifugo mnadani kuuza unalipa ushuru pale mnadani...