Siku hizi watu wanavurugwa sana mtu hata hakujui anakufokea njiani

Ejolisi

Member
Joined
Aug 26, 2022
Posts
57
Reaction score
87
Leo mida ya mchana nimetoka naelekea kwenye safari zangu nikakutana na mama flani ivi mfupi mwenye sura ya ugomvi sehemu kama ya kilima ivi kuna ka mteremko alivyoniona kutoka mbali kaanza kubwata kwa sauti kubwa wewe unaenda wapi nakuuliza unaenda wapi😂😂 si nakuuliza yaani nikikufikia nitakubutua mpaka uchanganyikiwe.

Niliogopa sana sababu hakuna mtu mwingine alikuwa anapita njia ile na hakuna njia nyingine ya kupita nikataka nikimbie nikashindwa, akaja kwa spidi akanitazamaa basi nimekufananisha😒 hata hakuniambia pole, kanikera sana.
 
Nimecheka sana
 

Ahahahahah aisee watu wamevurugwa sana utakuta hapo alikuwa anatafuta tuu useme kitu na wewe Kwa ukali Basi apate chanzo cha kukufokea zaidi na hata kukutwanga kabisa


Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…