Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Siku droni ya houthi ilipoweza kupenya mpaka TelAviv na kupiga jengo liliosababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi kadhaa,papo kwa papo asubuhi yake tukasikia bandari ya Hodeida imeshambuliwa.
Kwa shambulio la ballistic hapo juzi na kupita siku mbili bila majibu kuna mambo mengi ya kujiuliza.
Jee Israel imeanza kutetemeka inapopigwa, hivyo kupata kigugumizi cha kujibu.Hapo zamani haikuwa hivyo.
Au wameogopa baada ya kujua kuwa Houth wana vitu kama hivyo vya ziada wanavyoweza kuvivurumisha tena Tel Aviv.Ikumbukwe Houth wameshazidondosha droni za MQ-R 9 kumi mpaka sasa.
Yawezekana ndio Israel inajipanga ili ikifanya shambulio liwe kubwa zaidi na kuongeza kutisha maadui zake kama ilivyosema baada ya kushambulia Hodeida kuwa piga lile lilikuwa ni ujumbe kwa maadui zake mashariki ya kati yote.
Ujumbe nilioupata binafsi ni kuwa Netanyahu na baraza lake wanafikiri itakuwaje iwapo ballistic kama ile ikirushwa mara ya pili na ikatua mjini kati TelAviv watawezaje kuzuia wananchi kuingia barabarani kwa nguvu kutaka kumuondoa madarakani.