Updates
Hili suala mpaka sasa linazidi kuchukua taswira mpya kila masaa yanavyozidi kwenda aisee.
Yaani kumekuwepo na utata mkubwa sana namna taarifa hizi zinavyotolewa na madaktari kiasi mpaka sasa tumerudia vipimo tena lakini naona madaktari hawanipi info ambazo ni clear kuhusu hili suala.
Sasa kumeibuka mashambulizi mazito sana ya kishetani dhidi yangu baada ya kukaidi taarifa za madaktari,maana kuna mashaka mengi sana kuhusu hili suala zima kuanzia vipimo.
Mashambulizi yaliyoibuka ni makali sana kiasi nahisi uwezo wangu wa kumtetea mtoto na mama yake ni kama unaenda ukingoni.
Devils wanamtaka mtoto wangu kwa namna yoyote ile na hali sio poa kabisa.
Mapambano ndio kwanza yameanza rasmi kuanzia jana..
Mlio na familia zenu mnazozipenda hebu wakingeni wapendwa wenu mapema na haya mashetani.
Cha pili msisaini mikataba ya ya utajiri ya kuzimu kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo.
Niishie hapa kwanza niendelee na mapambano haya mpaka hatua za mwisho.
Nitarudi tena mrejesho mwingine ila mtoto bado yupo tumboni mwa mama yake. Sasa hivi anawindwa mama mtoto ili auawe habari za mtoto ziishie hapo.
Hicho ndicho napambana nacho pamoja na kumtetea mtoto.