Siku Mtanzania atakapotumia haki yake kumchagua kiongozi anayemtaka ndio tutaona Maendeleo ya Kweli Tanzania

Hii nchi tataizo lipo kwa vijana they know nothing about civil Rights sasa how comes Mtu mwenye miaka 70+ km kinana au Jk kuwa na influence ktk nchi yetu ...Vijana hawajitambui wanawaza ngono 24/7 na sasa hivi Ccm imeleta Mpira so ningumu mtu anayewaza ngono na Simba na Yanga kusimama kwa Ajili ya kuondoa lichama chakavu.

Nachokiona Ccm itatawala Hadi miongo minne so tusubir miaka ijayo 40
 

Naona swala lililojirudia hapa kupata Demokresia yetu ni mpaka Mtutu wa bunduki,

I still think tuna kazi ya kuwaamsha watu wajue kinachoendelea...

Kama watu wengine wangekua na awareness ya ufisadi unavyohujumu uchaguzi na nchi.....then kwa mfano huu mgogoro wa Wamasai ingetosha kabisa to get the ball rolling.....

Tatizo una create vipi hio awareness ndani ya Jamii kama kila Fisadi anahakikisha hufanyi hivyo, na pia kama TISS inashikiliwa na mafisadi, hata hio vita unaianzaje?? si TISS watajua na kuwaambia Mafisadi, then unakuwa silenced for good...lol...
 
Rebecca a.k.a Beck a.k.a Rabi a.k.a mwalimu,Lol.
Machozi yako nimeyaona,lol.
Unaumizwa na hii hali,lol.
Unataka mabadiliko,lol.
Basi yatakuja wakati ukifika na haupo peke yako,lol.
Ila umeumiza kichwa sana kufikiri ni kwa jinsi gani tutoke katika mkwamo huu unaozidi ule wa IST iliyozama ktk tope na tairi zote kuishia kabisa,lol.

Kaka yetu,aliwahi kutuelekeza njia(japo naye hakuwa na utayari)
Alisema ELIMU.
Yaani yule bibi yako kule Nanyumbu angekuwa na elimu sahihi juu ya nchi yake,uchumi wake,jamii yake mahitaji yake na hata UHURU wake,basi asingekubali kupelekeshwa kumchagua kiongozi na GENGE(et vyama vya siasa)siye na dira!
Hivyo elimu ikishasambaa kote na kwa wote,basi tutafika tuendako,LOL!
 
Hicho ndio kikwazo ukianza spread awareness kifungu cha uchochezi kinakuhusu kisha unapotezwa
 
'Those who vote decide nothing. Those who count the vote decide everything.'
- Dictator Joseph Stalin.
 
Kwahio suluhu ni kukiua CCM tu kisiwepo kwenye ramani
 
Kwahio suluhu ni kukiua CCM tu kisiwepo kwenye ramani
Tuwe na uthubutu kama hapo Kenya tu, wala sio mbali mkuu. KANU ya Kenya kimekuwa chama cha kawaida tu, hakina nguvu yoyote kwa sasa.

Je, wenzetu Kenya walifanyaje walau kuweza kukitoa madarakani, wakaweza kufanya amendments za katiba yao?(japo tunaambiwa it's a very corrupt country) lakini ndio economy powerhouse ya EAST AFRICA.
 
Tatizo la kwanza Tanzania hatujui tunataka nini.
 
Mkuu ni kweli ELIMU ingeweza kumsaidia bibi yangu afanye maamuzi sahihi...lol

Ila huku Jamiiforums kama umenotice kuna sentensi iko very common; Ujinga wa watanzania ni Mtaji wa CCM...lol

CCM inatumia ujinga wa watanzania kufanya ufisadi, na katika kulinda ufisadi CCM itahakikisha watanzania wanabaki mambumbumbu, Yanajilimbikizia mali ambazo shule zingejengwa a lot of people wangepata access to Education, specific Elimu ya Uraia, ambayo kila Raia angekuwa nayo, asingefanywa Mdoli kwenye Nchi yake mwenyewe.... 😑

Yote yana Mwisho...😳
 
UPO SAHIHI MKUU

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…