Siku Nilipoiona Simu Kwa Mara ya Kwanza Odeon Cinema 1955 au 1956 au Nyuma ya Hapo Kidogo Sijavuka Miaka 4

Kumbe Mzee amesoma katika shule za Kanisa?
 
Shikamoo Baba, Mungu akupe maisha marefu miaka 100+ inshallah iwe heri kabisa
 
Kumbe Mzee amesoma katika shule za Kanisa?
Azarel,
Naam nimeanza darasa la kwanza Lutheran Primary School Moshi mwaka wa 1958.

Hapakuwa na shule tukisoma ndani ya kanisa.

Niko kwenye simu nikiwa kwenye laptop nitakuwekea picha ya hilo kanisa In Shaa Allah.

Kisha nikasoma shule nyingine ya kanisa St. Joseph's Convent School Dar es Salaam.

Nitakuwekea picha.
 
Mbona una shari sana ndugu
 
Nimefurahi.
 
Nimefurahi.
Azarel,

Hizo picha mbili ni sehemu hiyo niliyosimama moja ila ''angle'' tofauti.


Lutheran Primary School Moshi picha hii nilipiga 1989

Picha hii nimepiga 2021


Waliosimama kulia wa kwanza ni mimi na aliyechutama chini yangu sasa ni Chief wa Siha Edward Jonathan Kidaha, Waliosimama wa kwanza kushoto ni Gulamabbas Jivraj huyu alikuwa na akili si za kawaida anafuatia jina lake Israel tukikaa desk moja baba yake alikuwa Balozi wa Israel Tanzania.

Anaefuatia ni Charles Mesquita sina la kusema kuhusu huyu. Alikuwa hasemi mkimya si kawaida kati yake yeye na Gulamabbas sijui nani alikuwa zaidi kwa mbongo.

Inataka muda kulueleza hili darasa.
Mwangalie Chief Kidaha anaefuatia ni Razia au Salma (twin sisters) ukimruka anaefuatia Asya Kharusi kisha Bhatia mwingine. Sikuweza kumtambua nani Razia nani Salma miaka minne tuliokuwa darasa moja kuanzia Form 1 D hadi tunamaliza Form IV. Hili darasa lilikuwa likiongoza kwa kila kitu hapo shule.​
 
Kumbukumbu nzuri
 
Kwa hii picha nashawishika kusema "familia yako ilikuwa moja ya zile familia bora" kwa wakati huo. Familia chache zilikuwa na exposure ya kuweka kumbukumbu kwenye picha. Aisee, memory nzuri sana. Ingawa baba yako mdogo imebidi kumkumbusha.
 
Kwa hii picha nashawishika kusema "familia yako ilikuwa moja ya zile familia bora" kwa wakati huo. Familia chache zilikuwa na exposure ya kuweka kumbukumbu kwenye picha. Aisee, memory nzuri sana. Ingawa baba yako mdogo imebidi kumkumbusha.
Jay...
Familia ya kawaida tu ya Kariakoo.
Picha hii alinipiga Mohamed Shebe.

Mohamed Shebe alikuwa na studio yake mkabala wa nyumba aliyokuwa akikaa mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed Mtaa wa Kipata na Livingstone.

Mohamed Shebe ndiye mpiga picha wa kwanza kupiga picha za harakati za TANU na kumpiga picha Nyerere mapambano ya kudai uhuru yalipoanza mwaka wa 1954.
 
Ahsante kwa maelezo. Ila ndio hivyo, sidhani kama zile nyumba zilizo na historia ya harakati za Uhuru bado zipo, naamini zilishavunjwa kupisha majengo ya kisasa.
 
Yanga ilikuwa inapata tabu sana kwa Sigara ya Marehemu Mansoor Magram.
 
Ahsante kwa maelezo. Ila ndio hivyo, sidhani kama zile nyumba zilizo na historia ya harakati za Uhuru bado zipo, naamini zilishavunjwa kupisha majengo ya kisasa.
Jayjay,
Kuna kipindi kinaitwa Zumari nimefanya na Jaffar Mponda nilisimama nje ya nyumba ya Abdul Sykes Mtaa wa Stanley (Max Mbwana) na Sikukuu nyumba ambayo Julius Nyerere aliishi baada ya kuacha kazi ya ualimu 1955.

Nyumba hii haipo badala yake zimejengwa apartments na ofisi.

Nilisimama nje ya jengo hili nikaeleza historia ya Julius Nyerere alipofika hapo 1952 na yote yaliyopitika ndani ya nyumba ile, uchaguzi wa Arnautoglo 1953 hadi kuundwa kwa TANU 1954 na safari ya UNO 1955.

Tukaenda Mtaa wa Kipata (Kleist Sykes) na Sikukuu ilipokuwq nyumba ya Clement Mtamila mahali ulipofanyika mkutano wa Halmashauri Kuu ya TANU kujadili kujiuzulu kazi Nyerere.

Nyumba zote hizo hazipo.


Nyumba ya Abdul Sykes ilivyo sasa

Nyumba ya Abdul Sykes ilivyokuwa katika miaka ya 1980 baada ya ukarabati
Hii ndiyo ilikuwa nyumba aliyokaa Julius Nyerere mwaka wa 1955 baada ya kuacha kazi ya Ualimu

Mbele ya nyumba ya Abdul Sykes nikifanya kipindi cha Nyerere Day 2022​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…