Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #81
Mtu...kumbe mzee wangu mtu wa bara wewe
Baba yangu kazaliwa Tabora na babu yangu kazaliwa Shirati ndani ya Boma la Wajerumani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtu...kumbe mzee wangu mtu wa bara wewe
Njabu...Njabu...
NImezaliwa Mtaa wa KIpata (Sasa Kleist Sykes).
Nikitoka nyumbani kwetu kuelekea Mnazi Mmoja nakata Mtaa wa Swahili kushotom kuna nyumba ya Hassan Machakaomo.
Hassan Machakaomo baba yake Machakaomo alikuwa Mzulu aliyekuja German Ostafrika na Sykes Mbuwane na akina Plantan.
Machakaomo alikuwa mmoja wa viongozi wa Young Africans mwaka wa 1948.
Nakuwekea picha ya viongozi wa Young Africans wakiwa na Abeid Amani Karume na Mtoro Rehani mwaka wa 1948.
Hassan Machakaomo ni huyo wa kwanza aliyekaa chini.
Mtafute Karume.
Nakatiza Mtaa wa Sikukuu kulia kwenye kona na Kipata kuna nyumba ya Clement Mohamed Mtamila aluyekuwa Secretary wa TAA President akiwa Mwalimu Thomas Plantan.
Uongozi huu ndiyo uliopinduliwana Abdul Sykes na Hamza Mwapachu kwa msaada wa Schneider Abdillah Plantan wakaingia madarakani Dr. Vedasto Kyaruzi kama President na Abdul Sykes Secretary 1950.
Baada ya hapo navuka Mtaa wa Livingstone kulia ndipo ilipokuwa studio ya Mohamed Sheba aliyepiga picha nyingi sana za siku za mwanzo za TANU na kumpiga picha Julius Nyerere.
Baadhi ya picha hizi zipo katika Maktaba yangu kwa hisani ya mwanae Mbaraka Shebe.
Sasa nafika mwisho wa Kipata kushoto kuna nyumba ya Sheikh Abdallah Simba Liwali wa Songea na rafiki ya babu yangu, Salum Abdallah.
Babu yangu kaishi nyumba hii hadi 1947 alipohamia Tabora.
Mkabala wa nyumba hii ni nyumba ya Kleist Sykes.
Naingia New Street (Sasa Lumumba Avenue).
Naijua Gerezani na wakazi wake.
Hii ndiyo ilikuwa dunia yangu.
Njabu...Ulikatazwa kwenu kuwa na ukaribu na watu wasiyo wa imani yako katika makuzi, au hukumbuki kuwahi kuwa na urafiki na mtu yoyote asiye wa imani yako? Inakuwaje kwa mtu ambaye umesoma shule za kanisa siyo chini ya mbili? Hiyo ya msafara wa Dada ws Malkia mtoto anaweza kuweka kwenye long term memory sababu ni tukio la kipekee kwa maana ya umati kukusanyika pembezoni mwa barabara, magari mengi na Mhusika Mkuu kuwa Mzungu wa kike. Naamini hata ingekuwa Ulaya enzi hizo watoto wa umri huo wengi wana kumbukimbu ya kumtupia macho kwa mara yao watu wenye ngozi nyeusi.
ali maumbaDingi embu siku moja tusimulie kuhusu fedhuli mmoja bwana maumba tunamsikia hewani tu
Dah mzee mimi nina miaka 28 ila nimeanza kuvuta fegi, bangi na kunywa viroba tokea nina miaka 15 hivi nitafika 70 kweli mzee wangu?Maso...
Mimi nina miaka 70 Alhamdulilah.
Kuwa niko "active kiakili," labda maana sina hakika nikipenda kusoma na kuandika toka udogoni.
Nguvu ya kuukwea Kilimanjaro sina.
Labda kitu kimoja ni kuwa sijatumia tumbaku wala ulevi wa aina yeyote toka kuzaliwa.
Huyo huyoali maumba
fataki wa zamani,ngoja aje atuhadithieHuyo huyo
Twilu...Wapi hapo kuna ushabiki wa kidini?
Mtu chake,fataki wa zamani,ngoja aje atuhadithie
mfia dini hakumbuki hata alivyokuwa anapewa mikate na siagi kanisani na mapocho pocho mengine.....ndo maana ulikuwa hakauki kwenye vibaraza vya kanisa.Sisi wafia dini ya islamia brain zetu haiziweki kwenye kumbukumbu jina lolote la mkristo.
hawa ndo ulisoma nao st.joseph cathedral?Njabu...
Unataka kuwajua marafiki zangu udogoni?
Angalia picha hapo chini:
View attachment 2499546
Kulia waliosimama: Mohamed Said, Yusuf Zialor, Kleist Sykes, Bubby Bohari, Abdallah Tambaza, Waliochutama kulia: Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kaisi 1968.
Luku....hawa ndo ulisoma nao st.joseph cathedral?
Luku...mfia dini hakumbuki hata alivyokuwa anapewa mikate na siagi kanisani na mapocho pocho mengine.....ndo maana ulikuwa hakauki kwenye vibaraza vya kanisa.
Nao ndo wamemsomesha huoni akitoa airtime,ameamua kuwa selective muslim extremist.
kihoro kitakua babu mudi!
Chali...Dah mzee mimi nina miaka 28 ila nimeanza kuvuta fegi, bangi na kunywa viroba tokea nina miaka 15 hivi nitafika 70 kweli mzee wangu?
Ila mzee Mohamed Said wewe ni tunu katika taifa hili huwa nafurahi sana nikiona uzi wako.
Mzee sikukuu kafariki nadhan 2020 au 2019 nyumbani kwake Sinza. Mwanae ni rafki yangu sana..Niache....
Saigoon ilikuja 1967 baada ya mgawinyoko wa club yetu ya kwanza Everton.
Sote tulikuwa shule ya msingi.
Mimi nilikuwa na umri wa miaka 15 wastani wa umri wetu sote ulikuwa katika hapo yaani miaka 15, 16, 17.
Wala hatukujua kama hii club itakuwa maarufu kiasi hiki.
Picha hiyo hapo chini ni Saigon Club 1980s Mtaa wa Sikukuu na Narung'ombe.
View attachment 2497529
Kulia: Marehemu Yunus, Mussa Shagow, Mohamed Said, Mkongo na Marehemu Ghalib Hamza(Guy).
Saigon katika 2020s:
View attachment 2497531
Kulia: Marehemu Nusura Faraj, Manzi, Marehemu Abdulkarim Shah (BuljiI) chini kulia Shariff Pazi na Mshike.
Alex,Mzee sikukuu kafariki nadhan 2020 au 2019 nyumbani kwake Sinza. Mwanae ni rafki yangu sana..
Miaka ya 1990 nilipata kuishi mtaa Gerezani Kariakoo
Saigon ndio pahara pekee nilikuwa nawaona. Jakaya Kikwete.. Abubakary Mgumia marehemu. Mansor Margam marehemu. Ditopile Mzuzuri Marehemu. Ismail Rage. Na wengine wengi tu..
Ni Stella Artois, nakumbuka Mzee alikuwa anakuja nazo kutoka Airport ya KLM (KIA) baadae hii kampuni ikaanza kutengeneza Plisner Beer ambayo watanganyika wanamudu beiMokaze,
Alhamdulilah sikuwahi kunywa ulevi wala kuvuta sigara.
Wakati niko kazini mtihani wangu mkubwa ulikuwa katika party ambazo ilibidi nitayarishe.
Nilikuwa Idara ya Masoko na lazima wateja wetu tuwafanyie takrima tukiwa na mikutano mchana tunawapa lunch na pombe kidogo.
Ikiwa jioni dinner na pombe hadi wachoke wenyewe.
Sasa linapokuja suala la vinywaji nikitaabika sana.
Mimi ndiye nilikuwa paymaster.
Nakumbuka kisa kimoja wakubwa zangu wananiuliza, ''Mohamed mmeweka Safari Beer peke yake?''
Mimi nikamjibu ndiyo.
''Kwani hakuna bia za maana mbona mnatufedhehesha kwa wageni wetu?
Ndipo nilipojua kuwa beer zina daraja zake kutokana na brand mfano Castle, Amstel, Stella Artoir nk.
Hii beer ya Stella kwa mara yangu ya kwanza niliijua Alexandria, Misri.
Baadae nikaja kuiona imeletwa Dar es Salaam na ilikuwa maarufu sana.
Lakini Misri ulevi unauzwa kimya kimya hautangazwi na lazima ufike hoteli maalum si kama kila mahali utapata pombe.
Wakubwa zangu wakawa wanasema, ''Huyu Mswahili anajua wapi mambo haya.''
Lakini mara moja nikamtafuta Manager wa hotel nikamwambia afanye haraka sana alete beer zingine zenye majina.
Nikawa nimejifunza.
Mtihani.
He ll never mention one, They y'll Kafir to himMuulize huyo Mzee, kule St Joseph shule ya Kanisa, katikati ya jiji, alikokuwa anasoma miaka mingi, hakufahamiana au kujenga urafiki na mtu yeyote asiye Muislamu? Hata Baniani?
• Kleist Sykes streetAlipokuwa na miaka 4 kakumbuka hadi alipokatiza mtaa wa Kleist Sykes SIKU MOJA?!! Mitaa yote ya Kariakoo hadi kufika Odeon Cinema ya wakati huo kaicha.