Siku Nilipoiona Simu Kwa Mara ya Kwanza Odeon Cinema 1955 au 1956 au Nyuma ya Hapo Kidogo Sijavuka Miaka 4

Mzee wangu, changamoto ni moja ya darsa katika maisha, naomba unisimulie changamoto japo moja tu katika maisha yako hasa enzi za ujana wako, iwe ya kiuchumi, kijamii au hata kifamilia, ilio wahi kukupata na ukaikabili katika namna ambayo huto sahau na pengine ikawa somo zuri kwa mimi nilie katika rika ambalo ni maji ya moto. (japo kwa ufupi tu mzee wangu).
 
Saigon ilikuja kujaa WATU wa usalama mnooo mpk ikafikia jambo likiongelewa pale jioni lipo ikulu hasa enzi za mwinyi na hata JAKAYA alipokuja saigon lengo ni kupata popularity ya watoto wa mjini kupitia tiss (zamani ikiitwa idara Maalumu) kabla ya mkapa kuiunda 1996.
 
Nini maoni yako kuhusu kubadili jina la Dar es Salaam na kuwa Mzizima. Maana kwa asili mji huu ulianza kwenye kijiji kilichoitwa Mzizima.
 
SIKU NILIYOIONA SIMU KWA MARA YA KWANZA ODEON CINEMA 1955 AU 56 AU NYUMA YA HAPO KIDOGO SIJAVUKA UMRI WA MIAKA MINNE
Nakumbuka kama jana vile.

Nilikuwa mgonjwa na baba yangu mdogo Mzee Issa akanichukua kunipeleka hospitali.

Ilikuwa usiku lakini si usiku mkubwa kiasi cha saa moja hivi.

Nina hakika na hili kwa kuwa Mzee Issa kanibeba tunatoka nyumbani Mtaa wa Kipata (Sasa Kleist Sykes Street) kwa miguu na nawaona watu mtaani njia nzima hadi tunafika New Street tunavuka Mnazi Mmoja tunapita kushoto tunaelekea Sultan Street (Libya Street).

Hapa Mnazi Mmoja palikuja kujengwa Mnara wa Uhuru.

Siku zile Mnazi MMoja ile ilikuwa uwanja mtupu hauina chochote ni mchanga mtupu.

Tunaingia Ring Street (Sasa Jamhuri Street) tunapita pembeni ya Odeon Cinema tunaingia mitaa ya Uhindini jirani na Msikiti wa Sunni kulikuwa na hospitali maarufu sana ya daktari wa Kihindi nakumbuka ingawa sina hakika jina lake lilikuwa kama Dr. Koya.

Mama zetu wakimsifia sana kwa kutibu watoto.

Hii hospital imedumu hapo kwa miaka mingi hadi mimi nimekuwa mtu mzima nikipita pale nikiiona.

Baada ya kutibiwa baba yangu mdogo Mzee Issa miaka ile alikuwa kijana akawa ananirudisha nyumbani.

Ndipo tulipopita tena Odeon Cinema tukaingia ndani kwenye call box (kibanda cha simu) kilichokuwa pale ndani.

Baba yangu alikuwa kazini akifanyakazi Telephone Exchange.
Jumba hili hadi leo lipo.

Mzee Issa akatia pesa kisha akapiga simu kuzungumza na baba yangu kumfahamisha kuwa kanipeleka hospitali na nimetibiwa.

Mzee Issa akanipa simu nimwamkie baba yangu.
Sikuweza kuzungumza.

Miaka mingi ikapita.

Siku moja nikamhadithia Mzee Issa habari hii.
Alishtuka.

Akawa kashangaa kisha akaniuliza, ''Mohamed unakumbuka habari hii?''

326990267_3458502591073338_625044799509994387_n.jpg

327556309_1913726512302146_4804005542629042379_n.jpg

327246206_488592410128550_2450343156164433652_n.jpg

I wish to meet you so that you can tell me how dar used to be back in the day.
 
Shehe hata fegi hujawahi onja??😀
Mokaze,
Alhamdulilah sikuwahi kunywa ulevi wala kuvuta sigara.

Wakati niko kazini mtihani wangu mkubwa ulikuwa katika party ambazo ilibidi nitayarishe.

Nilikuwa Idara ya Masoko na lazima wateja wetu tuwafanyie takrima tukiwa na mikutano mchana tunawapa lunch na pombe kidogo.

Ikiwa jioni dinner na pombe hadi wachoke wenyewe.

Sasa linapokuja suala la vinywaji nikitaabika sana.
Mimi ndiye nilikuwa paymaster.

Nakumbuka kisa kimoja wakubwa zangu wananiuliza, ''Mohamed mmeweka Safari Beer peke yake?''

Mimi nikamjibu ndiyo.

''Kwani hakuna bia za maana mbona mnatufedhehesha kwa wageni wetu?

Ndipo nilipojua kuwa beer zina daraja zake kutokana na brand mfano Castle, Amstel, Stella Artoir nk.

Hii beer ya Stella kwa mara yangu ya kwanza niliijua Alexandria, Misri.
Baadae nikaja kuiona imeletwa Dar es Salaam na ilikuwa maarufu sana.

Lakini Misri ulevi unauzwa kimya kimya hautangazwi na lazima ufike hoteli maalum si kama kila mahali utapata pombe.

Wakubwa zangu wakawa wanasema, ''Huyu Mswahili anajua wapi mambo haya.''

Lakini mara moja nikamtafuta Manager wa hotel nikamwambia afanye haraka sana alete beer zingine zenye majina.

Nikawa nimejifunza.
Mtihani.
 
Kweli Shk, ulikumbwa na mtihani mzito, pole sana.
 
Wakati mwingine ilikuwa kichekesho sana.
Siku moja nilikuwa Tilbury Port.

Hii ni bandari ndogo maili chache kutoka London.
Jioni mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tunabarizi Stella Maris.

Hii ni sawa na Mission to Seaman huku kwetu yaani club ambayo mbaharia wanaweza kwenda kupumzika, kupata chakula na vinywaji.

Ikawa wameingia vijana kutoka Afrika ya Kusini wakantuona Waafrika wenzao tuko pale.

Katika kundi letu alikuwapo kijana kutoka Afrika Kusini basi mazungumzo yakaanza.
Katika wale vijana mmoja akatuagizia pombe sote tuliokuwa pale.

Mimi nikakataa.

Yule kijana tuliyekuwanae pale akanivuta pembeni akaniambia kuwa katika mila zao mimi kukataa kinywaji alichoniagizia yule mgeni wetu ni sawa na kumuambia kuwa yeye ni adui yangu.

Nikasisitiza kuwa mimi sinywi pombe.

''I know Mohamed you dont drink let us get back and tell my brother that you dont take alcohol but you would be glad to have a coke.''

Basi yule kijana nimpomueleza haya maneno alifurahi sana na gumzo likanoga.

Siku hizo Afrika Kusini bado kuwa huru na Mtanzania hadhi yake ilikuwa juu sana kwa hawa ndugu zetu wa Kusini.

Siku nyingine In Shaa Allah nitakupa mkasa ulionikuta hoteli moja Maputo wao speciality yao ni wali samaki na beer.

Nimeingia bila kujua niketewa wali samaki na chupa moja ya beer.
Nini kilitokea?​

1674929916246.jpeg

Kulia Othman Shariff (Egypt) na Kushoto ni Abdul Indabawa (Nigeria)
Tilbury Port​

Katika maisha yangu nimewahi kusali sala kuu mbili ndani ya darasa.

Nimesali Eid El Haj Tibury ndani ya darasa la shule ya msingi na nkikasali sala ya Ijumaa John Hopkins UnIversity, Washington DC.
 
Kweli mzee wetu unayo matukio ya mtu kujifunza na kutia hamasa na furaha, basi usichoke kituhadithia. Bravo.
 
View attachment 2498610
Kulia Othman Shariff (Egypt) na Kushoto ni Abdul Indabawa (Nigeria)
Tilbury Port​

Katika maisha yangu nimewahi kusali sala kuu mbili ndani ya darasa.

Nimesali Eid El Haj Tibury ndani ya darasa la shule ya msingi na nkikasali sala ya Ijumaa John Hopkins UnIversity, Washington DC.

Hao jamaa wawili unawasiliana nao??
 
Mzee Mud ungeandika kitabu cha historia ya mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam ya leo ilivyokuwa wakati huo ingenoga sana
N...
Lakini ili historia ipendeze inahitaji pawepo matukio ya kuhadithiwa.

Nina makala nimepata kuandika miaka ya nyuma kuhusu mitaa.

Nikiipata In Shaa Allah nitaiweka hapa.
 
Hebu soma haya naeleza mitaa ambayo Julius Nyerere alikuwa akipita sana wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mitaa hii Mwalimu akipita akiwa kaongoza na Abdul Sykes na Dossa Aziz.

SIKU NILIYOIONA SIMU KWA MARA YA KWANZA ODEON CINEMA 1955 AU 56 AU NYUMA YA HAPO KIDOGO SIJAVUKA UMRI WA MIAKA MINNE
Nakumbuka kama jana vile.

Nilikuwa mgonjwa na baba yangu mdogo Mzee Issa akanichukua kunipeleka hospitali.

Ilikuwa usiku lakini si usiku mkubwa kiasi cha saa moja hivi.

Nina hakika na hili kwa kuwa Mzee Issa kanibeba tunatoka nyumbani Mtaa wa Kipata (Sasa Kleist Sykes Street) kwa miguu na nawaona watu mtaani njia nzima hadi tunafika New Street tunavuka Mnazi Mmoja tunapita kushoto tunaelekea Sultan Street (Libya Street).

Hapa Mnazi Mmoja palikuja kujengwa Mnara wa Uhuru.

Siku zile Mnazi MMoja ile ilikuwa uwanja mtupu hauina chochote ni mchanga mtupu.

Tunaingia Ring Street (Sasa Jamhuri Street) tunapita pembeni ya Odeon Cinema tunaingia mitaa ya Uhindini jirani na Msikiti wa Sunni kulikuwa na hospitali maarufu sana ya daktari wa Kihindi nakumbuka ingawa sina hakika jina lake lilikuwa kama Dr. Koya.

Mama zetu wakimsifia sana kwa kutibu watoto.

Hii hospital imedumu hapo kwa miaka mingi hadi mimi nimekuwa mtu mzima nikipita pale nikiiona.

Baada ya kutibiwa baba yangu mdogo Mzee Issa miaka ile alikuwa kijana akawa ananirudisha nyumbani.

Ndipo tulipopita tena Odeon Cinema tukaingia ndani kwenye call box (kibanda cha simu) kilichokuwa pale ndani.

Baba yangu alikuwa kazini akifanyakazi Telephone Exchange.
Jumba hili hadi leo lipo.

Mzee Issa akatia pesa kisha akapiga simu kuzungumza na baba yangu kumfahamisha kuwa kanipeleka hospitali na nimetibiwa.

Mzee Issa akanipa simu nimwamkie baba yangu.
Sikuweza kuzungumza.

Miaka mingi ikapita.

Siku moja nikamhadithia Mzee Issa habari hii.
Alishtuka.

Akawa kashangaa kisha akaniuliza, ''Mohamed unakumbuka habari hii?''

326990267_3458502591073338_625044799509994387_n.jpg

327556309_1913726512302146_4804005542629042379_n.jpg

327246206_488592410128550_2450343156164433652_n.jpg

Unanikumbusha call center za miaka ya 1998 hadi 2002 maeneo ya kariakoo haha..ilikuwa unawe coin ya 100, kumbe zimeanza kitambo?
 
Back
Top Bottom