Siku niliyojua mama yangu anaumwa UKIMWI mwaka 2005

Ina huzunisha sana.

Ila sio wote wanaopata Ukimwi, kwasababu ya sex ( ngono zembe ) au malaya. Tusihukumu waathirika, tuwapende tuwajari tuwatie moyo. Ingawa sasa hivi hofu ya ukimwi haipo watu wanatiana kama mbwa
Kweli tupu, sio yule Bibi kizee anayesema Watoto Yatima ni zao la uasherati na uzinzi
 
Mwaka 2005 ilikuwa tayari kuna ANGAZA hali haikuwa tete.

Mara ya kwanza kumuona muathirika ilikuwa 1998 ilikuwa Soo.
 
Hata sasa hivi mkuu Tsh unaua sana, ila wanasingia mala tb mala figo mala malaria sugu .. mala cansa, unafyeka sana, ukimwi haujaacha kuwa ukimwi mapigo yake ni yale yale
Sio wanasingizia mkuu, logic ya HIV ni ngumu kuielewa kwa mtu wa kawaida, UKIMWI au HIV ni upungufu wa kinga mwilini sasa what follows baada ya kinga kuisha ndio kinachoua, mfano TB, Pneumonia, Cancers, Meningitis nk, so kwenye Cheti cha kifo sababu ya kifo inatajwa ule ugonjwa Marehemu alikufa nao! Ila naungana na wewe bado watu wanakufa ila yale makali kama ya ule wa 80s au 90s yamepungua thanks to ARVs.
 
Kweli kabisa, elimu ya haya mambo ipo chini sana. Vijana wanaisha we huoni vijana wanavyokufa ? Sinza tabata na mitaa kama hiyo ni shida mkuu
 
Mmm unamthalilisha mama yako,si kila kitu ukiposti,kama ni la kujivunza sawa waweza kuposti lakin hili sio la kujivunza.baba na mama hata wakifa waheshimiwe
 
Mimi nilikuwa naimba sijui hata ulikuwa wimbo wa nan! Niliimba

Kosa la marehemu baba hakuvaa kondoo..
Kosa la marehemu mama hakuvaa kondoo..

Kumbe ile siyo kondoo bwana ni kondom nilikuja kujua baadaye sana.Nilishtuka sana na vile nilikuwa naimba kwa sauti
 
Mmm unamthalilisha mama yako,si kila kitu ukiposti,kama ni la kujivunza sawa waweza kuposti lakin hili sio la kujivunza.baba na mama hata wakifa waheshimiwe
Labda wewe bado una mawazo kwamba ukimwi ni ugonjwa wa kudhalilisha na unapaswa uwe ni siri, kwangu mimi sioni udhalilishaji wowote alioufanya, Mungu amlaze mahala pema mama yake.
 
Pole sana kwa kumpoteza Mama [emoji19][emoji17]
 
Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…