Yupo mpuuzi mmoja ni marketing manager kampuni X arusha, yupo kitandani saa hizi analoongea halijulikani kawa kama kawehuka....
Alishaoa na ni baba wa familia ilikuwa ndio tabia yake kutumia hizo dawa, mkewe aliona vidonge ndani akaogopa kwani jamaa alikuwa haumwi akavipeleka famasi kuulizia ni dawa za nini akihisi uenda ni Arvs jamaa anameza kisiri kumbe ni Viagra.
Siku zote "siku za mwizi kuiba ni nyingi ila siku ya kukamatwa ni moja tu"
Mwezi uliopita kama kawaida alichepuka na binti wa chuo X Arusha yupo 3rd year kama sikosei kwani anao wengi, wakala na kunywa sasa walipoenda lodge kula mzigo akameza hayo madawa ili binti amuone yeye kijogoo si akazima katikati ya game, binti akaona lile ni balaa kwakuwa michepuko huwa inatabia ya kujua namba ya mke ukampigia kwa simu ya mzimiaji kwamba njoo lodge fulani chumba X umchukue mumeo sijui kama mzima au kafa, binti akakimbia hakubeba hata shilingi, yule muhuni alikuwa na laki kadhaa kwenye suruali yake uenda binti alitaharuki unajua mambo ya mtu kama anataka kukata roho mbele yako inatia hofu.
Mke alipofika kamkuta jamaa povu na damu zinamtoka mdomoni na puani huku mshale wake umesimama na umekaza kinoma, kupelekwa hospital mishipa miwili inayo pump damu inayotoka kwenye moyo kwenda kwenye ubongo "carotid/vertebral arteries" imepasuka damu imevujia kwenye ubongo na alidondoka vibaya chini hivyo anauvimbe ndani ya fuvu, moyo umetanuka pia, reason behind ali overdose Viagra.
Sasa yupo hoi taabani kitandani hamjui anayeingia wala anayetoka ni fedheha na aibu kwa familia.
Yule binti naona alipo chuoni huko anatetemeka sijui kama atarudia tabia ya kuwa na waume za watu, kama yupo humu ajue kuwa yule mpenzi wake angali yu'taabani kitandani akamjulie hali...
Guys haya madawa ni hatari kwa afya zetu wanaume tusitumie.