Nilikuwa naupiga mwingi kiasi, kabla sijazeeka.
Mtama, Lindi kilikuwa kituo changu cha kwanza cha kazi baada ya kuajiriwa. Kama kawaida ya ujana, nikajichanganya kitaa na kufahamika mitaa ile na vijiji vya jirani vyote kuhusu usakataji wangu wa kabumbu. Kule, kabumbu (ligi) linapigwa sana baada ya mavuno.
Siku moja nikapata 'dili' la kwenda kushiriki ligi fulani huko kijiji fulani vilivyopo juu huko Makonde Plateau kijiji fulani km unaelekea tandahimba. Huko nikakuta kuna vilabu viwili vyenye majina makubwa ya timu za epl; Chelsea na Aston villa😂😂😂😂. Mimi niliajiliwa na Chelsea (kwa makubaliano yetu).
Kufupisha habari, nilifanikiwa kwenda na timu hadi fainali. Siku ya fainali ilipofika ulipigwa mpira si wa kawaida. Ngoma ilikuwa ngumu mno hadi dakika za mwisho. Ghafla, dakika za lala salama, bila kurarajia nikajikura mimi na kipa tu. Watu wote walijua, kutokana na mambo yangu, kazi imeisha na kuanza kushangilia.
Ebwana eee, huwezi kuamini ile nataka kuachia shuti nashangaa sioni mpira na badala yake naona sufuria jeupee kubwa kiasi limejaa hela, nikashikwa na bumbuazi nisijue nifanye nini.
Mara akili ikaniambia 'Acha ujinga' okota hela hizo. Nikaokota. Nilipomaliza kuokota tu nasikia filimbi ya refa na hapo kila kitu kikarudi katika hali ya kawaida, yaani fahamu zangu zikarudi. Kwa mshangao wangu, nikajikuta nimeshikilia ule mpira na hivyo ikabidi upigwe kuelekea kwangu. Kila mmoja akabaki ananishangaa pasipo kuamini.
Mwishowe mechi tukapoteza na huo ndo ukawa mwisho wangu wa kushiriki habari za mpira. Nilikoma!