Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Longolesa...hao jamaa ni htr sana.Haaaahaaa a.. Umenikumbusha nikiwa nacheza ligi daraja la tatu mkoa wa dodoma .. Tulikutana na walugaluga fulani kutoka Mlali huko.
.. Halftime tulikula 4 BILA.. Kumbe kuna mganga wao nje akienda chooni tu hapo karibu na uwanja akitoka tu.. Uku chuma kinaingia.... Tulisanuliwa hatukuamini.. Ikabidi viongozi wamuangalie second half.. Kweli akaingia chooni.. Alivotoka mda sio mrefu tupigwa la 5..wakaamini..ikabidi jamaa azuiwe kjingia chooni na wahuni... Game hii tulikula 5-0.
Eehe haohaoLongolesa...hao jamaa ni htr sana.
Nakumbuka huu sikuKuna mechi Moja ya Simba na Yanga Mwanzoni mwa miaka ya 90 pale shamba labibi mchezaji wa Yanga Rajabu Rashid alijikuta akiokota mpira ndani ya ene la 18 la timu yake.
Hata haileweki kilimkuta Nini, Mwamuzi akaamuru ipigwe Penalty kuelekea Yanga goli la kaskazini ya uwanja.
Penalty ilienda kupigwa na mchezaji na mpiga penalty mashuhuri wa Simba Hamis Tobias Gaga.
Gaga akapiga Penalty mpira ukagonga Mwamba ukarudi uwanjani Yanga waka okoa Ile hatari langoni mwao.
Ile mechi Simba walifungwa 3-1 Kwa Magoli ya Makumbi Juma, Tomas Kipese na Sanifu Lazaro
.Uchawi upo sana. Yanga imewekeza sana kwenye uchawi. Kukiwa na mechi wanatoa maelekezo kwa matawi yote watafute waganga wafanye kazi
Hii ndio taarifa iliyokaa mkao na yenye kueleweka...hakuna mbambamba.Kuna mechi Moja ya Simba na Yanga Mwanzoni mwa miaka ya 90 pale shamba labibi mchezaji wa Yanga Rajabu Rashid alijikuta akiokota mpira ndani ya ene la 18 la timu yake.
Hata haileweki kilimkuta Nini, Mwamuzi akaamuru ipigwe Penalty kuelekea Yanga goli la kaskazini ya uwanja.
Penalty ilienda kupigwa na mchezaji na mpiga penalty mashuhuri wa Simba Hamis Tobias Gaga.
Gaga akapiga Penalty mpira ukagonga Mwamba ukarudi uwanjani Yanga waka okoa Ile hatari langoni mwao.
Ile mechi Simba walifungwa 3-1 Kwa Magoli ya Makumbi Juma, Tomas Kipese na Sanifu Lazaro
Noma hio mzee nawapata vizur hao gheto man from turianKombe la uzinduzi wa Wilaya ya Mvomero mwaka 2001 uwanja wa shule ya Msingi Mvomero. Timu za ndondo maarufu za Wilaya ya Mvomero kama Gheto boys na Asec za kijiji cha Mvomero, Wami Magereza, Timu za Dakawa na Turiani. Fainally ni Gheto na Asec.
Hii Asec ilikuwa chini ya waarabu waliokuwa vizuri kiuchumi pale Mvomero na walikodi wachezaji wa ligi kuu na walikuja na coaster imejaa wachezaji wa ligi kuu nadhani zamani ilikuwa inaitwa ligi daraja la kwanza kama sikosei toka Dar kama Kipanya Malapa mzee wa ndondo, masamaki geofrey (marehemu), kipa Chachalamuya "Madusi" Ally Yusuph"Tigana" na wengine toka Dar. Refa ni Mwalimu Liyapiyapi toka Lusanga Sekondari akosqidiwa na Mgambo maarufu anaitwa "Ombopa". Game imewalalia Gheto boys iliyokuwa chini ya vijana wa kijiji cha Mvomero Rama Lundenga, Siwaseme (Fundi wa Mpira) na Abu Ramadhani "Amokachi" (alikuja chezeaga Yanga huyu jamaa) na Salumu wa "ghetto". Ikabidi viobgozi wa gheto wawasiliane na Babu alikuwa kijiji cha mvomero kitongoji cha "Dibamba". Hahaaa Mtaalamu akasema ngoja, ushindi ni wenu msiwe na shaka. Jamaa akachukua gobore lake na kulipiga juu. Pepo likawaingia wachezaji wa Asec na kuanza vurugu dhidi ya refa na wao kwa wao. Game ikaisha kwa vurugu na gheto akawa bingwa. Hii mechi ndio chanzo cha Pengo kwenye meno ya Kipanya Malapa.
Huyu mtaalamu alitumiwa tena na Mtibwa mechi moja na simba pale Manungu ile mechi Mtibwa alifungwa ila Golikipa wa Simba Mwameja alimpiga refa from nowhere kwani babu yule ndio alikuwa anayatuma mapepo na kuwaingia wapinzani na kuamza kuleta vurugu bila chanzo
Kombe la uzinduzi wa Wilaya ya Mvomero mwaka 2001 uwanja wa shule ya Msingi Mvomero. Timu za ndondo maarufu za Wilaya ya Mvomero kama Gheto boys na Asec za kijiji cha Mvomero, Wami Magereza, Timu za Dakawa na Turiani. Fainally ni Gheto na Asec.
Hii Asec ilikuwa chini ya waarabu wa Mvomero na walikodi wachezaji wa ligi kuu na walikuja na coaster imejaa wachezaji wa ligi kuu akina Kipanya Malapa mzee wa ndondo, masamaki geofrey (marehemu), kipa Chachalamuya "Madusi" Ally Yusuph"Tigana" na wengine toka Dar. Refa ni Mwalimu Liyapiyapi toka Lusanga Sekondari akosaidiwa na Mgambo maarufu anaitwa "Ombopa". Game imewalalia Gheto boys iliyokuwa chini ya vijana wa kijiji cha Mvomero Rama Lundenga, Siwaseme (Fundi wa Mpira), Abu Ramadhani "Amokachi" (alikuja chezeaga Yanga huyu jamaa) na Salumu wa "ghetto". Ikabidi viongozi wa gheto wawasiliane na Babu alikuwa kijiji cha mvomero kitongoji cha "Dibamba". Hahaaa Mtaalamu akasema ngoja, ushindi ni wenu msiwe na shaka. Jamaa akachukua gobore lake na kulipiga juu. Pepo likawaingia wachezaji wa Asec na kuanza vurugu dhidi ya refa na wao kwa wao. Game ikaisha kwa vurugu na gheto akawa bingwa. Hii mechi ndio chanzo cha Pengo kwenye meno ya Kipanya Malapa.
Huyu mtaalamu alitumiwa tena na Mtibwa mechi moja na simba pale Manungu ile mechi Mtibwa alifungwa ila Golikipa wa Simba Mwameja alimpiga refa from nowhere kwani babu yule ndio alikuwa anayatuma mapepo na kuwaingia wapinzani na kuanza kuleta vurugu bila chanzo na Mtibwa akapewa point za mezani.
MwanoHahahaaaa, wakaguru ni wabaya tu kiujumla. Kuna jeshi lao la Sungusungu la Gairo, Wamasai wanalifahamu hilo.
Hahaaa, unawafahamu sio. Hao sio mchezo enzi hizo.Noma hio mzee nawapata vizur hao gheto man from turian