Siku nimebaki mimi na kipa tu na ghafla mpira ukugeuka sufuria la hela ndipo nilipoamini uchawi upo!

Siku nimebaki mimi na kipa tu na ghafla mpira ukugeuka sufuria la hela ndipo nilipoamini uchawi upo!

Niko kwenye daladala nimesoma hii post nimejikuta nimecheka kwa sauti kubwa hadi waliojirani wamenishangaa.
 
Haaaahaaa a.. Umenikumbusha nikiwa nacheza ligi daraja la tatu mkoa wa dodoma .. Tulikutana na walugaluga fulani kutoka Mlali huko.
.. Halftime tulikula 4 BILA.. Kumbe kuna mganga wao nje akienda chooni tu hapo karibu na uwanja akitoka tu.. Uku chuma kinaingia.... Tulisanuliwa hatukuamini.. Ikabidi viongozi wamuangalie second half.. Kweli akaingia chooni.. Alivotoka mda sio mrefu tupigwa la 5..wakaamini..ikabidi jamaa azuiwe kjingia chooni na wahuni... Game hii tulikula 5-0.
[emoji23][emoji23][emoji23]noma sana
 
Habari kaka.

Kuna dada nina shida nae, kuonesha nipo serious nimemwambia popote alipo niko tayari kumfata tuonane.

Mie nipo mitaa ya Ubungo.

Dada ameniambia anaishi Temeke Yombo. Amesema kama ni kuonana, basi isiwe mitaa ya mbali na Temeke. Yaani tusiende mbali. Anaishi kwao.

Mie Temeke sio mwenyeji, napajua Tandika kituo cha daladala na ile barabara ya kwenda Buza.

Naomba unielekeze Yombo iko pande gani. Yaani nafikaje.

Halafu kingine, maeneo ya huko Temeke kuna mahali tulivu naweza mpeleka mtu wangu tukakaa kwa ajili ya mazungumzo.

Wote hatunywi pombe.

Napenda sehem iwe na mandhari tulivu, romantic. Tuweze kuongea kwa utulivu, kisha giza likiingia nimrudishe kwao Yombo mie nirudi Ubungo.

Nisaidie mkuu. Nampenda sana huyu dada.

Kuhusu usafiri nina private car.
Duuh
 
Kuna Timu mbeya inaitwa ngorongoro miaka ya 80 mwishoni , ilikuwa inamilikiwa na mtu binafsi. ilikuwa imekusanya wachezaji mastaa miongoni mwao ni Sekilojo wachezaji vijana wenye uwezo mkubwa.
Kuna mechi walikuwa wanacheza na halmashauri ya Kyela lakini wakati hiyo Timu inavuka barabarani mchezaji wao mmoja akagongwa na gari akajeruhiwa ikabidi mechi ihairishwe. kile kitendo Timu ya Kyela walikichukulia kama ushirikina hivyo mechi ya marudiano star wa ngorongoro Lau akaanguka uwanjani kukimbizwa hospital Hali mbaya ikabidi afatwe mganga wa Tukuyu Star lakini akashindwa akawaambia anayeweza kumwagua ni mganga aliyemloga.
bahati mbaya akafariki ikabidi azikwe na mpira wake.
waliyofanya tukio ni watu wa Kyela na marehemu alitokea huko ikabidi kiitishwe kikao na baada ya hapo mhusika mmoja baada ya mwingine akapukutika.
tukija Kwa marehemu Lau ni mtu aliyekuwa na kipaji Cha ajabu, baada ya kumaliza mtihani wa mwisho form four alikuta mizigo yake imeshapakiwa kwenye gari na kuajiliwa kama mchezaji kupangwa guest na kulipwa mshahara. kama asingekumbwa na majanga angekuja kuwa mchezaji maarufu Tanzania.
Kwa wale waliosoma mwakaleli watamkumbuka.
 
Back
Top Bottom