Siku nimebaki mimi na kipa tu na ghafla mpira ukugeuka sufuria la hela ndipo nilipoamini uchawi upo!

Leo kumbe chai inapatikania huku na hamniambii
 
Longolesa...hao jamaa ni htr sana.
 
Hivi huko EPL hawatumii uchawi!

Kuna mwamba alikuwa rafiki yangu tulikuwa tunapiga mishe pahala. Sasa moja ya vyanzo vyake vya mapato ilikuwa kukodiwa kupiga ball. Kuna siku kakodiwa kakubali fresh kabisa na nikam-escort hadi ground.

Maajabu nikaona jamaa kachomoa dakika za mwisho kabisa kabla ya game kuanza.
Nikamuuliza kwa nini! anasema hao wachezaji wa timu wanataka wacheze bila kinga yoyote, kwamba yeye kashachoka kulogwa, mkimkodi lazima muwe na kinga kwenye timu yenu.
 
Huu uzi utakutana na Chai za kila aina
 
Kitambo sana niliamini uchawi upo.

Nilikuwa nachezea timu moja ya daraja la tatu kule Temeke. Ile siku nilitanguliziwa mpira nikawatoka mabeki wa timu ya Yombo Makangarawe, nikampiga chenga kipa ambaye alikuwa ameshatoka golini, gafla mbele yangu sikuliona goli nilichofanya niliamua kupiga tu mpira mbele yangu.

Cha ajabu niliona mashabiki wanashangilia goli wakati mimi mwenyewe sikuliona goli mbele yangu.
 
Nakumbuka huu siku
 
Siku hiyo bwana tulikuwa na game na timu ya mtaa mwingine walikuwa wahasimu haswa, kila game walikuwa wanatupiga siku hiyo tukasema ngoja tuende kwa sangoma ingawa binafsi sikwenda ila masharti tuliyopewa ni kujipaka mafuta ya nguruwe 🐷 siku ya game, tulijitokeza mafuta balaa wote tunanukia haswa iwe ulikuwa muislam ilikuwa lazima upate, hata hivyo pamoja na mafuta yetu tuliambulia kichapo cha bao 2 bila
 
Kuna game sikumbuki ni African sports ya Tanga na timu gani sijui wakati jamaa anapiga shuti golini watu wameanza kushangilia goli mara ghafla Mpira unapasuka kabla ya kuingia golini.
 
Kama ni hivyo basi nimeacha kumlaumu Bangala kwa kukosa ile penati mpaka tukarnda kuokota mpira Chamazi
 
Hii ndio taarifa iliyokaa mkao na yenye kueleweka...hakuna mbambamba.
 
Dah kumamake wallah umenikumbusha ndondo za kaliua asee

kulikua na shekhe anaitwa shekhe seif alikua bingwa sana kwenye haya mambo...

kuna wakati hata Simba waliwahi mtumia huyu mzee

mpira wa bongo bila uchawi hutoboiii...
 
Noma hio mzee nawapata vizur hao gheto man from turian
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…