iamwangdamin
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 864
- 1,798
Natoa rai kwa polisi , msiue watu! Msiue watu please!
Rais Samia, usiue watu, epusha kumwaga damu ya watu wasio na hatia!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Natoa rai kwa polisi , msiue watu! Msiue watu please!
Rais Samia, usiue watu, epusha kumwaga damu ya watu wasio na hatia!
Wananchi waliomweka kiongozi madarakani kikatiba, wanaweza kumuondoa madarakani pia Kwa njia ya maandamano ya Amani.tuwekee kifungu cha katiba tujisomee.
Samimia must go ni valid mwaka 2025 sio sasa mkuu.Wananchi waliomweka kiongozi madarakani kikatiba, wanaweza kumuondoa madarakani pia Kwa njia ya maandamano ya Amani.
Sa100 must go ni harakati na hamasa za kuitoa CCCM na sa100 madarakani ukitegemea huu ni muda wa chaguzi.
Acheni kutisha raia wasio na hatia.
Harakati na maandamano ya raia wasio na silaha yameruhusiwa kikatiba.
NB: HAKI ya kuchaguliwa inaenda sambamba na HAKI ya kukataliwa ikiwa Kiongozi anaziba masikio asisikie maelekezo ya boss wake(wananchi).
Nami nikuulize,Samimia must go ni valid mwaka 2025 sio sasa mkuu.
Ni Rais wa kiwango cha chini sanaView attachment 3103790
Rais wetu mpendwa leo hii ataanza ziara rasmi Mkoani Ruvuma katika kuzindua miradi ya kimkakati ya Kitaifa.
mkuu umeandika vizuri sana...Nami nikuulize,
Kwani Mbowe alipotamka sa100 must go, alisema ni lini she must go?
Hiyo HOFU yatoka wapi?
Mbowe anaamsha umma wa Watanzania kuikataa CCM na Samia kuanzia muda huu unapoanza uchaguzi wa mitaa na kuendelea Hadi 2025 uchaguzi mkuu.
Vyama vya siasa vimeruhusiwa kufanya KAZI zao kisiasa kikatiba kabisa.
Nami Kwa maoni yangu,
Sa100 must go ni muhimu kabisa Ili vyama vibadilike, Leo CHADEMA ishike Nchi, kesho CCM nk nk.
Hiyo ndio DEMOKRASIA.
Samia Sio Malkia Elizabeth kwamba utawala wake Hauna ukomo!!
Ikiwa hataki kuondolewa madarakani Yeye na chama chake,mkuu umeandika vizuri sana...
ninachopenda wewe ni moja ya watu wanaojadili hoja bila lugha za kuudhi..
turudi kwenye mada...
samia must go haikutakiwa kutamkwa kwenye maandamano, kwasababu kauli kama hii inaweza kuamsha watu wakamtoa raisi madarakani kwa njia zisizo halali(kidemokrasia)...
hii kauli ingetamkwa na mbowe kwenye mikutano yao ya siasa isingechukuliwa kwa uzito wowote, maana anawashawishi watu wachague mtu wa chama chake kipindi cha uchaguzi...
maandamano hua yana sababu na malengo yake...
kimsingi sababu ya haya maandamano ni utekaji na mauwaji ya raia...
lengo lake ni kulazimisha serikali ifanye uchunguzi thabiti na wahusika wachukuliwe hatua...
raisi ameshalaani mauaji hayo, hivyo kwa vyovyote hawezi kupinga maandamano yenye nia njema(kupinga hayo mauaji)...
sasa watu wenye akili na nia njema wangekuja na slogan inayopinga utekaji na mauaji...
ukisema samia must go, maana yake hayo maandamano ni ya kumuondoa samia...
ukisema samia must go in 2025 watu wanakuelewa kirahisi.
Ni kweli kulaani pekee haitoshi, ndivyo maana aliagiza uchunguzi wa kina ufanyike...Ikiwa hataki kuondolewa madarakani Yeye na chama chake,
Kulaani pekee haitoshi bila kuchukua hatua, IGP na Ndugu Masauni kuendelea kuwepo Ofisini Hadi sasa ni sababu kuu ya Mbowe kusema " Samia must go".
Awafute KAZI Ili kuonyesha amechukuzwa na yanayoendelea Kwa uwajibikaji wa pamoja.
Pia wanasiasa wasihamaki wanapotishwa kuondoshwa madarakani kama ambavyo Huwa wanafurahia kusifiwa pindi wanapotimiza wajibu wao.
Sasa unataka IGP ajichunguze ndugu yangu?Ni kweli kulaani pekee haitoshi, ndivyo maana aliagiza uchunguzi wa kina ufanyike...
Sasa kabla uchunguzi haujaisha tunaitisha maandamano ya kumtaka atoke madarakani!
Uko sahihi, lakini ulitamani nani achunguze mkuu?Sasa unataka IGP ajichunguze ndugu yangu?
Kuwa fair basi, Tanzania ni yetu sote,
Mambo ya vyama tuyaweke kando,
Nchi kwanza, vyama baadaye.
Kwa wengine kuua mtu kuna raha yake, rai yako hawataielewa.Natoa rai kwa polisi , msiue watu! Msiue watu please!
Rais Samia, usiue watu, epusha kumwaga damu ya watu wasio na hatia!
Ingekuwa ni kwenye sanduku la kura hiyo move ingekuwa halali na ya kidemokrasia kabisa. Lakini kwenye maandamano ni move ya kukosa hekima na maarifa.Dhamira kuu ya chama chochote Cha upinzani ni kukiondoa chama tawala madarakani.
Hivyo basi Sa100 must go ni move halali kabisa kwenye utawala wa kidemokrasia.