Kwahiyo mtu asipojionesha mwenyewe Polepole ataendelea kuwafichia hayo machafu?
Kwa maendeleo ya taifa, hiyo ishu ya Wasira inawezaje kuwa hoja?
Asante kwa maswali yako nikianza na la kwanza.
Kama ulimfatilia Polepole utaungana nami kuwa lengo lake halikuwa kuwataja waovu au kufichua hayo machafu kama unayosema, Polepole alidai kuwa mchakato ndani ya CCM wa kumpata mgombea urais Mama Samia haukuwa wa haki kwa maana umekiuka desturi zao katika chama hivyo alimuomba Mama Samia awarekebishie CCM yao na yeye asigombee urais, mbali na hilo alitaka kuwepo na maridhiano ya kitaifa yatakayoshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo vyama vya siasa sanjari na kuachiwa huru mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lisu ili arudi kwa familia yake ndipo waingie katika uchaguzi.
Kwa kuwa hayo aliyoyadai hayakutekelezwa kama alivyoomba, akaja na awamu ya pili kwamba kinachomfanya mama Samia kushupaza shingo ni kwa sababu CCM imetekwa na wana Mtandao na kubwa zaidi mifumo ya Nida, tume ya uchaguzi na CCM imeungana hivyo kwa mantiki hiyo kuna asilimia kubwa ya matokeo kupikwa na CCM kushinda, kwa kipindi chote hicho hakutaja mtu yeyote wala uchafu wowote, ila baada ya kujitokeza Rostam akamjibu, alipojitokeza Kikwete akamjibu na alipojotokeza Wasira pia akajibiwa na ndugu Kamwaga mwandishi wa habari kuhusu Gesi Cuba kuuzwa 2000 pia alipewa majibu yake.
Kwa mtirirko huo utagundua kuwa Polepole amesimama katika madai yake ya CCM kukiuka desturi yake ambayo mwenyewe anasema ni kumwaga Oil.
Swali pili Inshu ya Wasira nimekupa kama elimu ili ujifunze usichokijua kwa watu wanaojua, Mzee Wasira alimchokoza Polepole na yeye akamjibu kuwa Wasira siyo mwema kama anavyojinasibu mbele ya Umma na sababu yake alimtukana Mwalimu Nyerere je wewe ulilijua hili?
Ushauri wangu kwako usiwe kama punda unakufa na njaa hali ya kuwa chakula kipo mgongoni mwako, Polepole ni mtu na nusu jifunze kutoka kwake utafanikiwa asante.