Chamoto
Platinum Member
- Dec 7, 2007
- 9,883
- 22,310
Whistle-blowers kulindwa kisheria ni mpaka kuwepo na mkakati wa kuwaondoa wanatandao, kwanza, kwa hali ya sasa, hakuna wakuwalinda. Kutegemea miujiza ya kwamba uongozi huu utayeyuka, ni kosa kubwa sana, hatutakuwa tunawatendea haki vizazi vijavyo.Hili jambo halipaswi liachwe kwa utashi atakayekuwepo madarakani bali mikataba yote iwe wazi tena kwa lugha nyepesi hata kibibi au babu kule kijijini aweze kusoma na kuelewa..., Pia katika kuvujisha kutegemea wanasiasa pekee (ambao currently ni wachumia matumbo na wana maslahi yao) tungehitaji sana Media / Wanahabari / Whistle-blowers wanaolindwa kisheria ili waweze kupeleleza ni nini kinaendelea na mali zetu na wajukuu zetu....
Je, tutegemee wapinzani kuibua madudu ya Chama Tawala au tupate Wanahabari wazalendo wenye nguvu za Kisheria kuibuia madudu ya wanasiasa
Katika kufanikisha hayo kwanza inabidi tuilete katiba mpya ile ya rasimu ya Warioba, inayopendekeza Rais kushitakiwa endapo atakengeuka.Sasa huoni kama Kiongozi tu anaweza akabadilisha either kunyonga au kuleta sheria madhubuti pia anaweza akaja mwingine akaleta sheria kandamizi au akabadili mambo mazuri (je kweli tuweke maisha yetu rehani kwamba every five to ten years fingers crossed kama tutapata madhubuti au gharasha ?
Hili nakumbuka kipindi cha Rais Mwinyi, ambapo pesa nyingi zilichapishwa na kujaa mitaani, bila kuwa na uzalishaji wowote. Vijana wakawa wanadharau kazi na wasomi, sababu tuu... ukizunguka zunguka mitaani, kufanya mission town, unapata pesa.Tatizo kuu sio Mtandao uliopo; bali ni loophole ya uwezekano wa mtandao kuwepo; Power Abhors a Vacuum; Hata ukiondoa hawa wa leo wengine watachipuka kwa haraka sana hapo hapo (where there is money there is crime) Hususan crop ya sasa ambayo kimaadili wizi umekuwa ujanja na upigaji dili, kama vile ni kitu cha kujivunia (utasikia mtu mtaani ukiongelea ufisadi na wizi anakwambia either una wivu au unapenda umasikini) sasa huoni kwamba tatizo kubwa ni la kiutamaduni kwamba tumehalalisha wizi na tunashindwa kutofautisha (Uchapakazi na Ujambazi, Ujanja na Upumbavu, Uchoyo na Ulimbukeni)...., Mtu anasifiwa kwa kuuza Mali ya Vizazi kwa short term gain na Ujiko wa Kitaa kutoka kwa watu wenye myopic thinking..., Zamani mtu akifukuzwa kazi kwa kuiba mali ya Umma ukoo mzima mnaona aibu na watoto wake shule wanakuwa wanajishitukia (leo hii mtoto wake atatembea kifua mbele kama vile mzee wake ni Jemadari aliyeshinda vita)
Kuzuia maisha ya upigaji dil na ujanja ujanjai, inabidi kwanza pesa izuiwe, isizagae mitaani bila kuifanyia uzalishaji. Watu wataiheshimu pesa na ule wizi wizi na udalali utakoma.
Kwa ufisadi mkubwa, kama ule wa kuuza mali za umma, mfano migodi ya makaa wa mawe, sheria kali za uhujumu uchumi, zinatakiwa kutumika ili iwe fundisho kwa wengine.