Ni sahihi kabisa, kipindi cha bunge la katiba alikuwa moto sana kutetea katiba na kuipinga serekali, baada ya kuingizwa kwenye mfumo na JPM akawa kimya na kutetea yaliyokuwa yanaendelea kipindi cha Jiwe, kutolewa kwenye mfumo ndio anaanza kelele tena mi namuona ni mchumia tumbo tu hana lolote. Na hafai kuwa kiongozi sababu kiongozi hupaswi kutoa siri za mfumo pale unapokuwa nje ya mfumo angejifunza kwa Nchimbi ,Nchimbi alipelekwa na JPM Cuba lakini alitulia sasa yuko wapi.Aliomba mwenyewe!?
Unataka kusema Alijiuzulu mwenyewe ubunge? Malawi aliomba kupelekwa? Au Cuba
Kinachoonekana sasa hiv ni matokeo tu, ila alianza maneno na darasa lake lile la uongozi baada ya kuwekwa kando ya mfumo
Eleza nikuelewe unapodai "kinacho mpa shida zaidi Pole pole ni kuwa nje ya mfumo na si msukumo wa kizalendo" wakati yeye mwenyewe alijiuzuru nafasi ya Ubalozi yenye heshima na manufaa binafsi kibao?Polepole huyuhuyu? Binafsi nimeacha kumsikiliza maana ni kama anatafuta attention zaidi kuliko kutoa hoja.
Kwa kipindi kama hiki unaanzaje kutishia kwamba flan akiongea na mimi ndo nitataja!?
Kwanin asitaje moja kwa moja kama ni jambo ambalo wananchi wanapaswa kujua?
Ni wazi kinacho mpa shida zaidi Pole pole ni kuwa nje ya mfumo na si msukumo wa kizalendo.
Watanzania kwa kupenda ushabiki tunaona tumepata mtetezi.
Binafsi simuamini huyo bwana mkubwa kwakweli
Watu sio Mtu..., na hata kama ni mtu anatoa wazo / idea ambalo linafanyiwa kazi na kutekelezwa pia hio sio destination (kwamba tumefika) bali maboresho yanafanyika kila wakati kutokana na kuona practically what works and what does not..., hivyo kilichopo leo kinakuwa bora kuliko jana..., na sio kila ajaye anakuja na yake; na ukizingatia ni kupeana vijiti miaka mitano mpaka kumi no wonder ni mwendo wa kufuma na kufumua.... (na hizi politics zetu za attack and surival) na sio to do what is good for the common man.Mifumo haishushwi toka mbinguni, inatengenezwa na watu, hivyo ni lazima uwe na watu sahihi kwanza ili ujenge mifumo.
Hiyo nafasi ya heshima unayosema ilikuwa ni ya kumtoa nje zaidi ya mfumo, Kumbuka alikuwa Mbunge na iko wazi kabisa alikuwa anaelekea kwenye nafasi zaidi ya hiyo( Uwaziri)Eleza nikuelewe unapodai "kinacho mpa shida zaidi Pole pole ni kuwa nje ya mfumo na si msukumo wa kizalendo" wakati yeye mwenyewe alijiuzuru nafasi ya Ubalozi yenye heshima na manufaa binafsi kibao?
Kweli maboresho ni zoezi endelevu ila usifananishe China na sisi, wale walikuwa hapa kabla ya Mao. Walikuwa na mitandao yao (Dynasties) iliyowafanya wawe dhaifu, Mao alipoingia wanamtandao wakakimbilia Taiwan.Watu sio Mtu..., na hata kama ni mtu anatoa wazo / idea ambalo linafanyiwa kazi na kutekelezwa pia hio sio destination (kwamba tumefika) bali maboresho yanafanyika kila wakati kutokana na kuona practically what works and what does not..., hivyo kilichopo leo kinakuwa bora kuliko jana..., na sio kila ajaye anakuja na yake; na ukizingatia ni kupeana vijiti miaka mitano mpaka kumi no wonder ni mwendo wa kufuma na kufumua.... (na hizi politics zetu za attack and surival) na sio to do what is good for the common man.
Unadhani kwanini wachina wanakata mbuga ?!!! Hawana uoga wa kufanya mambo haraka haraka (ya kuonekana hivyo wana-plan long term) Huku kila mtu akija anataka sifa kwamba hii ni miradi yangu na ya yule nisimalize nisijempa sifa (and this even USA is prone to it).
Maelezo yako umechinganya kwa kujua au makusudi.Hiyo nafasi ya heshima unayosema ilikuwa ni ya kumtoa nje zaidi ya mfumo, Kumbuka alikuwa Mbunge na iko wazi kabisa alikuwa anaelekea kwenye nafasi zaidi ya hiyo( Uwaziri)
Baada ya kifo cha Rais JPM sijui umesahau sarakasi zilizokuwepo!?
Baadae ndo akapelekwa Malawi kama balozi kutoka bungeni direct, mbona vitu viko wazi Mkuu.
Naam sisi na sio fulani; Ingawa fulani pekee anayeweza kuleta mabadiliko ya Kiuchumi na maendeleo ya vitu kwa kasi ni a Benevolent Dictator; ila pia hilo ni tatizo sababu ukishampa mtu uwezo wa kuwa Dictator kumpata Benevolent au a Sadist ni a matter of Bahati Nasibu...Kweli maboresho ni zoezi endelevu ila usifananishe China na sisi, wale walikuwa hapa kabla ya Mao. Walikuwa na mitandao yao (Dynasties) iliyowafanya wawe dhaifu, Mao alipoingia wanamtandao wakakimbilia Taiwan.
Sasa Ifike wakati na sisi tufanye 'a paradigm shift' kwenye nchi yetu ili tutengeneze mifumo imara.
Sawa Polepole tumekusikia.Kijana huyu anapoongea huchoki kumsikiliza. Hachoshi kama vile Mwalimu Nyerere Huwa hachoshi kumsikiliza hotuba zake. Polepole ana uwezo mzuri wa kujenga hoja na ana akili sana.
Unajua mtu mwenye uwezo wa kuongoza na kutenda Huwa anapimwa kwa njia tofauti na moja wapo ni uwezo wa kujenga hoja na kui practice hoja. Mimi nilivutiwa sana na creativity yake wakati akiwa katibu wa itikadi wakati wa Rais Magufuli. Alikuwa anasikiliza kero papo kwa hapo na kuzitatua. Hakika watu wengi walifaidika na kusaidika sana wakati wake ndugu zangu hasa wanyonge ambao Rais wa sasa amewakana.
Hoja za Polepole ni nzuri na ndivyo mataifa makubwa ya kijamaa yamefanikiwa kwa namna hiyo. Polepole ni aina ya watu ambao hata ukimpa dhamana ya Juu na hata ku present kitu mbele ya mataifa mengine au raia wa kigeni huwezi kuwa na mashaka kwamba anaweza kutindinganya au kubanganza lugha. The guy is fluent enough na ameelimika vizuri kabisa.
Mimi naona tumepata hasara kumpoteza kijana huyu kwasasa although naamini atarudi baadae tena katika nafasi ya Juu zaidi na mungu atatia wepesi. Binafsi namuombea kila siku kwa mungu kwanza awe salama na siku moja aje kulitumikia Taifa hili.
Ndugu zangu asikudanganye mtu wanyonge wanateseka nchi hii kwasasa basi tu. Nikiona mtu anasema anatiki October Huwa najiuliza huyu anaishi nchi Gani? Huduma za umma zimedorora Hadi aibu. Nitoe mfano Mimi mwenyewe mwezi wa 8 nilijaza fomu za kupata huduma ya maji kwenye nyumba yangu.
Nilichokutana nacho kwenye ofisi ya idara ya maji ni aibu na fedheha. Hadi Leo sijapata maji. Watu wanataka kwanza mzungumze pembeni. Kila nikiomba control namba naambiwa mtandao unasumbua.
Sasa kwa hoja hizi za Polepole naona kabisa ni nzuri na huenda akiwa kiongozi wetu tunaweza kutoka hapa.
"Watanzania ipendeni Tanzania kama mnavyowapenda mama zenu" maneno haya yalitamkwa na Mwl.Nyerere akiwa kitandani katika siku zake za mwisho hapa Duniani.
"Kuwa nje ya mfumo na si msukumo wa kizalendo"Polepole huyuhuyu? Binafsi nimeacha kumsikiliza maana ni kama anatafuta attention zaidi kuliko kutoa hoja.
Kwa kipindi kama hiki unaanzaje kutishia kwamba flan akiongea na mimi ndo nitataja!?
Kwanin asitaje moja kwa moja kama ni jambo ambalo wananchi wanapaswa kujua?
Ni wazi kinacho mpa shida zaidi Pole pole ni kuwa nje ya mfumo na si msukumo wa kizalendo.
Watanzania kwa kupenda ushabiki tunaona tumepata mtetezi.
Binafsi simuamini huyo bwana mkubwa kwakweli
Hana lolote, mnafik tu.Ni binadamu tu amechoka kukumbatia uovu
Acha hizo wewe.....Je wajua kwamba ndo ajaye ? Kupitia mlango fulan ? Keep this
Kwani sasa hivi hatuko kwenye udikteta?Naam sisi na sio fulani; Ingawa fulani pekee anayeweza kuleta mabadiliko ya Kiuchumi na maendeleo ya vitu kwa kasi ni a Benevolent Dictator; ila pia hilo ni tatizo sababu ukishampa mtu uwezo wa kuwa Dictator kumpata Benevolent au a Sadist ni a matter of Bahati Nasibu...
Ufisadi wa sasa unatisha sana, wananchi wanahali mbaya halafu watu wanaiba bila kificho.Lakini kitakachotokea kama mambo yataendelea kuwa hivi tegemea machafuko ya hali juu duniani (the likes of French Revolution) Sababu watawala wa sasa worldwide wamejisahau na hawajui kula na vipofu na mbaya zaidi automation na teknolojia inaendelea kupunguza uhitaji wa nguvu kazi hence wengi kukosa ujira na Gap ya Have and Have nots kuongezeka; Kusipofanyika mabadiliko ya kina na ya haraka sana kitakachotokea ni for the detriment of everyone...
Usi underestimate watu wasio na cha kupoteza, Tanzania tunaweza kuweka historia mpya.Extreme Poverty anywhere is a threat to Societies Everywhere... (By the way sitegemei changes kubwa kufanywa na these crops of Politicians; they are neither pioneers nor men/women of the people rather self serving, overpaid, under-performing primadonnas)
Is it Benevolent ?Kwani sasa hivi hatuko kwenye udikteta?
Sasa ingekuwa wametishika sana wangesha-react ila bado wana hope and we do not know for sure kuhusu Ufisadi sababu unafichwa na hata ukitoka unapitia ulaghai wa uwekezaji / PPPs n.k.Ufisadi wa sasa unatisha sana, wananchi wanahali mbaya halafu watu wanaiba bila kificho.
Still they have hope na alternative haijaaminika vilivyo kwa kuonekana ni walewale..., Amini nakwambia the biggest threat ni extreme poverty kwa watu kukosa ujira hivyo kutokuwa na basic needs; mbaya zaidi all services zinageuzwa kuwa money making scheme na all commanding height kuuzwa not to the highest bidder bali who gives kick-backs the most....Tumeshafikia breaking point, si raia wala askari, watanganyika wamechoka.
Tanzanians still have hope and opportunities are still available; and whichever will happen won't be new... in the world context we have been here before (Nothing New, Only the History you do not Know...)Usi underestimate watu wasio na cha kupoteza, Tanzania tunaweza kuweka historia mpya.
Mkuu kweli huwa nakukubali...ila hii kamba kabisaaa..walah haiwezekaniJe wajua kwamba ndo ajaye ? Kupitia mlango fulan ? Keep this
Shida ni watanzania sisi wenyewe tunatabis ambazo sio za kijamaa unafki, uongo, udokozi na uoga hizi sio tabia za kijamaa kabisa.Kabla ya kuwaza hayo, jambo ninalo kutaka utafakari ni kwanini Mwl alie kuwa na mawzao mazuri zaidi ya Polepole hakuweza tekeleza malengo yake ya kijamaakama alivyo fanikiwa ktk maeneo mengine, pili watanzania wangapi wako tayari kuishi sera za kijamaa?
Quite the opposite.Is it Benevolent ?
Kuna wazalendo wanaojua kiundani ufisadi unaoendelea, na baadi ya mabo yamekuwa yakivuja, mfano tulisikia Polepole akiongea kuhusu bandari, inawezekana DP World wamesingiziwa tuu, wamiliki ndiyo hao hao wanamtandao.Sasa ingekuwa wametishika sana wangesha-react ila bado wana hope and we do not know for sure kuhusu Ufisadi sababu unafichwa na hata ukitoka unapitia ulaghai wa uwekezaji / PPPs n.k.
Hii ya kutokuwa na uzalendo dawa ni ndogo tukipata kiongozi madhubuti. Tutaweza weka sheria kali za kufunga au hata kunyonga mafisadi (kama China).Pili tatizo kuu uzalendo umekwisha na utamaduni wa sasa wizi ndio ujanja ni kwamba hata asiyeiba ni kwamba hajapata opportunity na ukipata opportunity wote waliokuzunguka wanategemea hali yako itabadilika na isipobadilika wanakucheka kwamba ulipata opportunity na haukuitumia (the whole society is rotten); ila hio itabadilishwa na extreme poverty (wengi ambao hawatapata opportunity ya kuiba sababu hawana hata makombo wata-react) na chuki ya have and have nots itaongezeka na kila mwenye nacho atakuwa tarnished na walionacho walioiba na hata ambaye sio mwizi ataonekana mwizi (wanaochuma Janga watakula na wakwao ambao ndio kina sisi)...; Case in point madogo wengi Kenya hawana hope ndio unaona kina Gen Z kila siku wapo kitaa kwa hapa huenda hali hio itakuja kwa Gen Alpha
Kweli, kama mtandao wakiendelea kushupaza shingo, tutafika huko haraka sana, watu kuingia mtaani, maana watu wanahasira kuona machawa wanamaisha mazuri bila kufanya kazi ya maana, wakati wananchi wanapigwa mitozo isiyo na maana.Still they have hope na alternative haijaaminika vilivyo kwa kuonekana ni walewale..., Amini nakwambia the biggest threat ni extreme poverty kwa watu kukosa ujira hivyo kutokuwa na basic needs; mbaya zaidi all services zinageuzwa kuwa money making scheme na all commanding height kuuzwa not to the highest bidder bali who gives kick-backs the most....
Hali isipobadilika Gen Alpha lazima wataingia mtaani (and not for the call of politicians bali survival instinct)
Tanzanians still have hope and opportunities are still available; and whichever will happen won't be new... in the world context we have been here before (Nothing New, Only the History you do not Know...)
Tunachohitaji ni Transparency (UWAZI) kwenye mali za UMMA wakati mikataba yote inafanyika na sio after the fact; sababu kama mikataba ni Siri na haiwekwi wazi who is the wiser (hata ikivuja watu watasema ni uzushi) na kama tunategemea huyu leo ndio atavujisha je akipenyezewa rupia kwenye udhia ? Hili jambo halipaswi liachwe kwa utashi atakayekuwepo madarakani bali mikataba yote iwe wazi tena kwa lugha nyepesi hata kibibi au babu kule kijijini aweze kusoma na kuelewa..., Pia katika kuvujisha kutegemea wanasiasa pekee (ambao currently ni wachumia matumbo na wana maslahi yao) tungehitaji sana Media / Wanahabari / Whistle-blowers wanaolindwa kisheria ili waweze kupeleleza ni nini kinaendelea na mali zetu na wajukuu zetu....Kuna wazalendo wanaojua kiundani ufisadi unaoendelea, na baadi ya mabo yamekuwa yakivuja, mfano tulisikia Polepole akiongea kuhusu bandari, inawezekana DP World wamesingiziwa tuu, wamiliki ndiyo hao hao wanamtandao.
Sasa huoni kama Kiongozi tu anaweza akabadilisha either kunyonga au kuleta sheria madhubuti pia anaweza akaja mwingine akaleta sheria kandamizi au akabadili mambo mazuri (je kweli tuweke maisha yetu rehani kwamba every five to ten years fingers crossed kama tutapata madhubuti au gharasha ?Hii ya kutokuwa na uzalendo dawa ni ndogo tukipata kiongozi madhubuti. Tutaweza weka sheria kali za kufunga au hata kunyonga mafisadi (kama China).
Tatizo kuu sio Mtandao uliopo; bali ni loophole ya uwezekano wa mtandao kuwepo; Power Abhors a Vacuum; Hata ukiondoa hawa wa leo wengine watachipuka kwa haraka sana hapo hapo (where there is money there is crime) Hususan crop ya sasa ambayo kimaadili wizi umekuwa ujanja na upigaji dili, kama vile ni kitu cha kujivunia (utasikia mtu mtaani ukiongelea ufisadi na wizi anakwambia either una wivu au unapenda umasikini) sasa huoni kwamba tatizo kubwa ni la kiutamaduni kwamba tumehalalisha wizi na tunashindwa kutofautisha (Uchapakazi na Ujambazi, Ujanja na Upumbavu, Uchoyo na Ulimbukeni)...., Mtu anasifiwa kwa kuuza Mali ya Vizazi kwa short term gain na Ujiko wa Kitaa kutoka kwa watu wenye myopic thinking..., Zamani mtu akifukuzwa kazi kwa kuiba mali ya Umma ukoo mzima mnaona aibu na watoto wake shule wanakuwa wanajishitukia (leo hii mtoto wake atatembea kifua mbele kama vile mzee wake ni Jemadari aliyeshinda vita)Kweli, kama mtandao wakiendelea kushupaza shingo, tutafika huko haraka sana, watu kuingia mtaani, maana watu wanahasira kuona machawa wanamaisha mazuri bila kufanya kazi ya maana, wakati wananchi wanapigwa mitozo isiyo na maana.