Siku tukimtumia Polepole vizuri, Nchi yetu itapiga hatua vizuri sana

Whistle-blowers kulindwa kisheria ni mpaka kuwepo na mkakati wa kuwaondoa wanatandao, kwanza, kwa hali ya sasa, hakuna wakuwalinda. Kutegemea miujiza ya kwamba uongozi huu utayeyuka, ni kosa kubwa sana, hatutakuwa tunawatendea haki vizazi vijavyo.
Katika kufanikisha hayo kwanza inabidi tuilete katiba mpya ile ya rasimu ya Warioba, inayopendekeza Rais kushitakiwa endapo atakengeuka.
Hili nakumbuka kipindi cha Rais Mwinyi, ambapo pesa nyingi zilichapishwa na kujaa mitaani, bila kuwa na uzalishaji wowote. Vijana wakawa wanadharau kazi na wasomi, sababu tuu... ukizunguka zunguka mitaani, kufanya mission town, unapata pesa.

Kuzuia maisha ya upigaji dil na ujanja ujanjai, inabidi kwanza pesa izuiwe, isizagae mitaani bila kuifanyia uzalishaji. Watu wataiheshimu pesa na ule wizi wizi na udalali utakoma.

Kwa ufisadi mkubwa, kama ule wa kuuza mali za umma, mfano migodi ya makaa wa mawe, sheria kali za uhujumu uchumi, zinatakiwa kutumika ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…