Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Mmmhhhh we jmaa kwa kamba me skuwezi aiseee
 
Ile shule siisahau kwanza tokea utoto nilikua sipendi maharagwe... Nilivyofika kwenye ule mji nilikaa kwa rafiki wa familia yetu kama wiki nikawa naenda kuisoma shule.... Siku natinga shule nikakuta ni ugali maharagwe tena ya mawese yasiyoiva nikawa nashangaa mbona kila vessel ni la njano.... Tulikula mawese ile shule sisahau...

Ila kuna jamaa yangu alinifurahisha sana... Siku amefika shule jioni wakamshushia katikati ya mabweni... Watu wakaanza kupiga makelele asulubiweeeee jamaa akadaka tax akarudi alipotoka...
 
Dah mwe msinukumbushe IFUNDA TECH form one mimi Suku ya kwanza tu Master P na Chichi (viongozi wa bweni) waktukabidhi viunga vya maua kuvitunza vilowe kila siku asubuhi na jioni.. Kula shida foleni kama ya kwenda mbinguni, Uonezi, Maticha wakax, Baridi Kali blanket nilfua once in whole those four years, na mengine Mengi... Heshima kwako IFUNDA TECH
 
Hahahaha thanks for sharing[emoji23]
Mimi mara ya kwanza kukanyaga boarding school ya serikali ilikua form 5 ikafika muda wa kula jioni tukaenda nikitegemea ugali kama naoujua mimi.kufika nakuta ugali fulani hvi una harufu na muonekano mbaya na maharage hayajaungwa hata yale sijui tu yalikuaje.sikula ile siku nikalala njaa.baada ya siku chache shule ilinishinda
 
MAKETESTAN BULL ON GWAH πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Waliniibia yeboyebo zangu nilizosafiri nazo kutoka mkoa.
Just imagine ndo nafika tu bwenini nikaleta usafi ule wa kihome home si nikavua mayeboyebo yangu ili ningie Dom, loooh wana wakapita nazo,nilikuja kuziona nipo form two term ya pil[emoji23].
Machalii wa Shaban Robert 06 Mzumbe Secondary tuheshimiane mazee.
 
Wale wazee wa Ndanda boy shule safi siku nimeripoti tumelala vizuri saa kumi na moja naskia kiongozi mmoja anapayuka form five amkaaaaaa!!! Huku akiimba wimbo wa blood (the game ft Damian Marley) basi huu wimbo lazima niwe nao kila kwenye music devices zangu!!!
 
Niliingia boarding form five:
Maisha ya boarding nilishayajua coz nikiwa o level weekend naenda kulala mashuleni kwa washkaji zangu!! So sikuwa na ugeni na misosi wala tabia.

Nilipokelewa na watemi wa form three, sura yangu tu wakajua huyu mwenyewe! Ilibidi wawe wananilia timing πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜ƒ

Nilianza na intro! Usiku mnene nimelala kitandani ndoo na mazaga mengine nimeweka pembeni ya kitanda! Madogo wanatest zari kuniibia wanavizia wakijua nimelala, wanashtuka nawaambia oyaaah! Rudisha ndoo!

Kesho yake ikawa story shule nzima jamaa halali! Ukigusa ndoo yake au chochote anakutoa mbio! Ikawa ni mchezo na hakuna siku nilifeli, walichemka!

Wakanibananisha bwenini siku moja usiku sina hili wala lile! Nashtuka madogo kama kumi hivi wa form three na two wamenizunguka wanadai wananipa kipigo najitia msela sana hata kama nipo five!!

Niliruka ghafla toka kitandani nikatua kwenye mabega ya yule mbabe zaidi! Wakiwa wamehamaki mbabe wao kaanguka chini nikawahi switch ya taa nikazima kukawa giza totoro!! Nilitoa mkanda niliwadunda isivyo kawaida kuniona hawanioni wanashtukia vichapo mbaya zaidi mlango walifunga wenyewe kufungua hawawezi!! Walikula kichapo heavy sana!

Baada ya vilio kuzidi mle bwenini walinzi wakaja kuvunja mlango! Kuna niliokuwa nimewapasua na bakoli ya mkanda ikabidi wakatibiwe! Kesho yake waalimu hawanielewi na hawaamini kichapo nilichotoa, nikaambiwa rudi home kalete mzazi!!

Nilipoondoka sikurudi tena, na shule nikajihamisha mwenyewe kwenda shule yenye hostel badala ya boarding, dingi alikuja kujua baadae sana shule ninayosoma tena mkoa mwingine! akanyoosha mikono!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…