Niliyojifunza kuhusu kumiliki gari kwa hela za kudunduliza ni kwamba LITAKUTESA SANA. Nilifanyia makosa kama yako kununua SUV kali ya ndoto zangu kwa hela ya kudunduliza mpaka nikaiandikia Uzi huku.
Leo hii imepaki miezi 12 kama siyo 13. Brothet, watu hawakuonei wivu ila kumiliki gari Hilo kwa hela za mawazo za miaka zaidi ya mitano. Mnhhh!
Nimejifunza kwa makosa yangu. Kama wakati ungerudi nyuma ningenunua hizi
TOYOTA Pixis Epoch G, 2010>
HONDA Life G, Zest 2010>
NISSAN Moco, Otti 2010>
MITSUBISHI EK Wagon 2010>
DAIHATSU Mira, Move, Esse 2010>
SUZUKI Alto, Wagon R, Palette 2010>
SUBARU Stella, Pleo, Lucra 2010>
MAZDA Carol 2010>
Ila uzuri ni kuwa tunajifunza kwa makosa. Ninaamini utajifunza ama utainjoi. Jiandae kwa lolote.
Note: kwa mtu mwenye hela za kudunduliza tafadhali USIKURUPUKE. Utalichukia gari, utawachukia watu. Heri ununue hizo nilizotaja