Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Mimi siku ya kwanza kuongea kizaramo ilikuwa pale kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwl Nyerere. Aisee ulikuwa mtiti sio wa kiswahili
 
balaa la kiingereza ni pale ukute unaoongea nao wanakijua vilivyo yaani wanakucheck tu unavyovunja. Hatari sana jameni, Elimu yetu ya kibongo uozo tu, eti na sasa wanataka watu wajifunze kwa kiswahili kuanzia nursery mpaka universities. Hapo ndo tutakuwa tumeloga jumla
Mola atufanyie wepesi
 
Wandugu kama mjuavyo wengi wetu tumesoma shule za st. Kayumba kwa hiyo Ngeli ni ishu kwetu. Basi kwa kuunga unga hivyo hivyo nikachaguliwa Chuo (UDSM) sasa kufika huko si ndo mambo ya Seminar za DS 101 natakiwa ni-present ilikuwa balaa usiku kabla ya seminar sikulala naogopa.

Kwenye seminar yenyewe sasa jasho lilinitoka mwili mzima balaa yaani naona nyota nyota tu daah! sitaki kukumbuka. Lakini namshukuru Mungu baada ya pale nilifanya bidii y kujifunza kwa kusoma zaidi vitabu vya kiingereza na kuongea na watu wasiojua kiswahili (hasa waganda, Wazambia & Waganda).

Angalau sasa mambo si mabaya Ulimi si mzito tena kiviile!!! English aisee ni hatari jamani. SHIKAMOO KIINGEREZA

**Halafu mademu wanazingua mno, ukikosea wanakucheka balaa daah. Ukiwa na demu chuo ni shidaa sana
Mimi kidog nizimie nilipotakiwa kuongea kiingereza mbele ya wazungu. Ilikuwa australia na nilitakiwa kufanya presentation. Hiyo sik7 sitoisahau maishani mwangu
 
ungewataja inhesaidia kubaini kuwa huwasingizii. pia kuwasilisha mada no rahisi kuliko kufundisha. (siwatetei ila isije ukawaonea hata wale wanaosaidia wanafunzi wasiosikia kingereza kikitamkwa kwa haraka ktk umbali Fulani
Nikiwataja utawajua hata? Maana wewe umesoma Zoom Polytechnic wale wa UDSM utawajulia wapi?
 
mtoa mada umenikumbusha mbali sana aisee mimi nitabaki kumlaumu Nyerere kwa kung'ang'ania Kiswahili shu;e za Msingi (Nursery/pre-school mpaka Std. 7). Hao mademu nao makauzu sana wanakuchekaje kwani wao walikuwa wanakijua KIZUNGU?
Mkuu nakuunga mkono hakuna sehemu mzee nyerere alifeli kama hapo.. Wabongo tulivyowajanja tungekuwa mbali tatizo KINGE.
 
Write your reply...wakati wa o level kuna kitu inaitwa ku speech. pale assemble!. siku ticha akanambia nispeech!. ukizingatia alikuwa anantafuta sana. ikabidi tuu niseme TIGO EXPRESS YOURSELF!. usiulize viboko nilivyolandikwa!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]my name is
Jamani kidhungu mkisikiage tu kwa watu ni kirahisi ukimsikia MTU anasema ngoja iwe zamu yako.Nakumbuka enzi zile Mbeya day sec school nikiwa form one,kulikuwa na mambo ya Ballotspeech 'morning talk'Basi bwana huku na kule bila kutegemea wala kuambiwa mapema eti nikachagulia kuwa Kiongozi Wa Morning talk ya kila siku,nilipoitwa jina tu kwanza mwili uligoma ukizingatia kwa wakati huo kulikuwa na Ticha mmoja Mnoko sana Mwakasala....jamani bada ya kufika mbele nikajikuta nasema my name is... My name is....my name is ..kama Mara kumi wkt Mimi ndo nilitakiwa kuwa mfano Wa kuongea na si kwamba nilikuwa sijui ila kiingereza mbele za watu halafu for the first time it real shocked me,kilichokuja kunitesa ni bada ya hapo wanafunzi ikawa ndo salamu yao sasa my name is... na ukizingatia nilikuwa MTU maarufu sana.Ilinisumbua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi tupo O level, akaingia mwalimu wa zamu, akaagiza tujihesabu, ajue idad ya watoro, bas ghafla ikaanza One,Two,Three..... Kufika nyuma kimyaa, tunaanza tena, ikifika pale kimyaa, kumbe jamaa imewakutia namba 12,13,14,15 ilikua ni vita kuzitaja..! kwa usalama wote wakahamia mbele ili waanze na 0ne.. hizi si mteremko.
Mkuu dah umenivunja mbafu asee yani mpaka watu wananishangaaa apa

Sent from my VFD 301 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom