IamBrianLeeSnr
JF-Expert Member
- Nov 10, 2022
- 2,010
- 4,179
Huu uzi na udumu kwakweli 😂😂😂😂View attachment 2581294
Wali:
Kidume nikapika wali. Ule wali ulikuwa ukiweka kwenye sahani unalia kama kitenesi.
Tambi:
Zilitoka zimebandiana kama ugali halafu mbaya kishenzi.
Mchicha:
Ulitoka mchungu kweli kweli kama mti wa mwarobaini
hongera mkuu wengine tulijikita kutengeneza magari ya mabamba na kukimbiza maringi udogoniMm najua karibu vyakula vyote na kazi zote za nyumbani, yn mpaka namuonea wivu mke wangu mana atajinenepea
Daaah! Hayo yalikua mauaji ya samaki sio mapishi😂😂😂😂Nilipiga sato kwenye chungu nikaweka chini na majani ya mgomba nikimuiga bibi yangu kuongeza udambwiudamwi. Kilichotokea nilikuta samaki ameungua kawa mweusi kama 2pac wa ghana.
Ilikuwa mara ya kwanza kuachwa home peke yangu kwa kushtukiza.
😂😂😂Daaah! Hayo yalikua mauaji ya samaki sio mapishi😂😂😂😂
HahahahDaaah! Hayo yalikua mauaji ya samaki sio mapishi😂😂😂😂
safiiiii👏👏👏sanaa yan niamshe saa saba za usiku unataka chapati utakula mkuu
Shea maujuzi hayo MkuuMimi nilikuwa napka wali kawaida boko nlipoanza ishi peke yangu.
Kuna mwanajeshi mwanaume alikuwa jiran alinifundisha kupika wali hadi leo nna muda nimepka ila mtu yeyote akionja wali niliopika huwa anasalute. Kati ya kitu najua kupka ni wali unachambuka balaa na ni kwa jiko la gesi au umeme nje ya hapo siwezi.
Daaaah, umenichekesha🤣🤣🤣🤣🤣Nilipika sato kwenye chungu nikaweka chini na majani ya mgomba nikimuiga bibi yangu kuongeza udambwiudamwi. Kilichotokea nilikuta samaki ameungua kawa mweusi kama 2pac wa ghana.
Ilikuwa mara ya kwanza kuachwa home peke yangu kwa kushtukiza.
Nimefikiria ilikuaje wakati unakula nimekufa mbavu🤣🤣🤣🤣Maisha haya nilishawahi kumkaanga samaki bila kumtoa magamba
Hii ni kali ya mwaka 🤣 🤣 🤣 🤣View attachment 2581294
Wali:
Kidume nikapika wali. Ule wali ulikuwa ukiweka kwenye sahani unalia kama kitenesi.
Tambi:
Zilitoka zimebandiana kama ugali halafu mbaya kishenzi.
Mchicha:
Ulitoka mchungu kweli kweli kama mti wa mwarobaini
Hukuwahi kuharibu hata kimoja kwenye harakati za kujifunza?Mm najua karibu vyakula vyote na kazi zote za nyumbani, yn mpaka namuonea wivu mke wangu mana atajinenepea
Huyo alikuonea kwakweli, ugali wa watu 10+ si mchezo'Mecheka sanaaa.
Kwenye pishi la ugali kwa mara ya kwanza wengi sana hukosea.
Mie nakumbuka nikiwa drs la nne dada alinilazimisha kupika ugali wa watu zaidi ya 10 kwenye jiko la mkaa.
Nikabana mbanio kwa kutumia mapaja, moto ni mkali , aisee sitasahau. Ugali ulikuwa na mabongebonge ya kutosha japo uliiva😀
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣Kuna siku nilikuwa home alone si nikapika njegere nikajua Kama maharage tia maji mengi nikayaacha yachemkie nakuja kufunua nakuta uji wa njegere nikayaunga ivoivo kibishi
Muda wa kula nikawa napaka njegere juu ya wali Kama vile blue band jinsi inavyopakwa kwenye mkate😁
Hapo wengi walikuwa ni wadogo, watu wazima walikuwa kama wawili. So, haukuwa mkubwa kiihivyo! Sema nilikuwa sijawahi kupika ugali hata wa mtu mmoja.Huyo alikuonea kwakweli, ugali wa watu 10+ si mchezo
Kuharibu kawaida sana hy, ili ujue ni lazima ukoseeHukuwahi kuharibu hata kimoja kwenye harakati za kujifunza?
Tuambie, kipi kilikutesa sana kumasta? Kililika siku ya kwanza?😀😀Kuharibu kawaida sana hy, ili ujue ni lazima ukosee
Sasa hivi uko vzr au bado zinatoka kama vibaragaranakumbuka mara yangu ya kwanza kupika chapati, zilitoka kila moja na shape yake halafu ngumu kama kaukau nilisemwa ile siku sitakaa nisahau