Siku ya kwanza kupika ilikuwaje? Ulichopika kiliiva?

Wali na dagaa kwangu hapana, hayo ni matumizi mabaya ya Mchele, kitu ubwabwa maharage
 
Nilianza kupika nikiwa darasa la nne.. ugali ulikataa kuiva kabsa nikaumwaga kwa siri nikapika mwingine... nakumbuka ilikua ni usiku mvua inanyesha alafu jiko linavuja....
 
Wali na dagaa kwangu hapana, hayo ni matumizi mabaya ya Mchele, kitu ubwabwa maharage
Vyote vipo konki hasa ukipata dagaa ambayo haina mchuzi aaaaah...mpaka nimejilamba hapa πŸ˜‹πŸ˜‹
 
Nakumbuka bi kubwa alisafiri akaniacha na madogo,siku hiyo msosi ulikuwa hausomeki,kuna mchele kidogo,ndizi mbichi kidogo,na nje kuna mbogamboga za majani shazi kama figili,maboga,iksema isiwe shida,nikamenya ndizi na kukatakata vipandevipande,katakata mboga za majani,chukua mchele osha,ti kwa ufuri moja,weka jikoni ,tia mafuta ,vikawivaa,nikawapa wale,mpaka leo wananiit profesa πŸ˜€
 
😁😁vyakula vingi najua kuvipika havijawahi nisumbua kuvipika Kwa mara ya kwanza, kitu sijawahi kupika ni pilau kila nikimiss nanunua
 
We jamaa ni comedian 🀣🀣eti mpaka leo wananiita professor
 
Ahahahah mbona vibaragara..wewe utakuwa umekaa mkoani kigoma maana ndio wanasema kabragara au khabago maana vinatengenezwa kwa unga wa muhogo mchanganyo wa ndizi za kuiva.
Hahaha
 
Kwanza nlianza kupika chai!

Then kuna kipindi nikawa nipo home bi mkubwa akienda kazini anaacha pesa tu utajua utapika nini na hakukuwa na beki tatu!! Dah nikawa napika ndizi mzuzu na kuku choma.

Baadae nikaanza kuchukulia upishi kama hobby, nikawa napika chakula chochote ninachokitaka! Nlijifunza jinsi ya kutumia kisu jikoni, jinsi ya kukata veggies katika shape mbalimbali ,mapishi ya local foods na international !! Lol nlipooa nikawa namfundisha mama watoto kupika siku mojamoja!

Huwa naenjoy zaidi nikiwa nachoma nyama huku nimezungukwa na wanangu. Tunaanza kuila nyama ikiwa jikoni kwanza.

Kila pishi nalipika ila ishu inakuja kwenye kuosha vyombo mara baada ya kupika!!

Jitahidi sana kuwafundisha wanao wajue hizi life skills kama usafi, kupika, kuosha vyombo n.k hakika wakijua hayo wataweza kuishi mahali popote bila ya tabu.

Ukijua kupika vizuri hata majirani wanaweza kudhani kuwa ni tajiri sana kumbe bajeti ya misosi uliyopika haizidi hata 5000/=tsh
 
Nakuunga mkono kabisa hapo kwenye kufundisha watoto shughuli ndogondogo za nyumbani ni muhimu sana aisee hata kama anasoma bording schools akirudi home ni kufanya kazi mpaka atazoea tu na kujua.
 
🀣🀣🀣Noma
 
2005 nilimwambia mama anipe mchele kidogo nijifunze, akanambia hana mchele wa kuchezea so akanipimia mwingi ili nipike chakula cha wote, kilichofuata ni mabao kila hatua mpaka wali ukakamilika, nahisi walikula na machozi yangu
Bora alikuwepo kukuelekeza, lasivyo ungelisha watu vitukoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hata mimi mara ya kwanza kupika ni ugali ila angalau mie niliacha maji yakachemka. Ila kilichofuatia itv....πŸ™†πŸ™†πŸ™†πŸ™†
 
Nilipika ugali.. sikumbuki kama uliiva au la ila ulilika
 
chapati nilisukuma roundi ikapitiliza kwenye kibao, nakumbuka jikoni nilikua nahangaika sana nikisukuma na mimi nasogea mama aligomba sana hio siku na alikua akikufundisha n mara moja tubya pili inakuhusu
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…