Siku ya kwanza kupika ilikuwaje? Ulichopika kiliiva?

haha umenikumbusha 2003 nimeanzisha geto ngoja nipike chips kavu viazi nkavitia chumvi mara ya kwanza kupikia mkaa....we wacha vichemke masaa havikauki vianepeta tu mwisho wa siku nkala hivyo hivyo vimejaa mafuta tii..nkaja jifunza mahala baada ya siku kibao viazi mviringo ukitia chumvi havikauki kwenye mafuta siku hizi ni shefu..mzuri sana...
 
Mbona Mimi huwa naweka chumvi lakin natumia ges hapo shida ni mkaa ukiweka chumvi vinakuwa na ladha nzuri sana
 
Mbona Mimi huwa naweka chumvi lakin natumia ges hapo shida ni mkaa ukiweka chumvi vinakuwa na ladha nzuri sana
yaani upishi bora ukiweka chumvi uwe kama unavianika maji maji yapungue au viwe vikavu kabisa kuna muhindi pori alinifunza hicho
 
yaani upishi bora ukiweka chumvi uwe kama unavianika maji maji yapungue au viwe vikavu kabisa kuna muhindi pori alinifunza hicho
Unavichuja maji na usiweke chumvi vikakaa mda wakat mafuta yanaanza kupata joto ndio unaweka chumvi
 
2005 nilimwambia mama anipe mchele kidogo nijifunze, akanambia hana mchele wa kuchezea so akanipimia mwingi ili nipike chakula cha wote, kilichofuata ni mabao kila hatua mpaka wali ukakamilika, nahisi walikula na machozi yangu
Darasa zuri sana
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nlikua kijijini na sista....kuna mahali akawa anaenda akaniachia maagizo nichukue samaki (ameshakaangwa) nimchemshe kidogo atakuja kuunga mwenyewe.

Kwa mara ya kwanza sasa mie kupika, yule samaki nikamuweka kwenye chungu, nikamjazia mimaji, weka kwenye kuni alichemka kama maharage, naongeza tena maji nachochea kuni naenda kucheza....kazi yangu ilikua kuongeza maji na kuni tu sister anarudi samaki hafai akapika mwingine
 
Mpaka umri huu sijawahi kumaster jinsi ya kusonga ugali , naweza kuupika ila kipimo huwa kinanipa shida sana ! Naweza kupika mkubwa sana kupitiliza au nikapika ugali mdogo sana hata mtoto hashibi ! Ila ile kukadiria kipimo exactly sijawahi !! Angalau naweza kuuivisha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ww hukuacha mafuta ya chemke Sanaa,mm upishi wa chips huwa natia chumvi moja kea moja na zinatoka nzur Tena kavu
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wengine tulianza kupika wadogo hata sikumbuki km niliwahi kutoa boko, uzuri km sijui pishi huwa nauliza then baada ya hapo ni ufundi siku hizi kuna YouTube basi maisha rahisi sana
 
Mimi niwe mkweli nyumbani kwetu kupika watu ni 0 .Sasa kuna mboga za majani hizi watu wakizipika zinakuwa bado na rangi yake ile ya kijani supa kwelikweli.Mimi kila nikijaribu iwe chainizi,mchicha ,tembele yanalegea ,halafu halafu yanakuwa na mamichuzi kweli kweli kama yale walikuwa wanapika wakina bimkubwa homuu.
 
2005 nilimwambia mama anipe mchele kidogo nijifunze, akanambia hana mchele wa kuchezea so akanipimia mwingi ili nipike chakula cha wote, kilichofuata ni mabao kila hatua mpaka wali ukakamilika, nahisi walikula na machozi yangu
Kumbe tupo wengi tuliojifunza in hardway, mimi ilikua middle 90's mama anatoa darasa la kupika wali, aloo ilikua kimbembe
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘Š
 
πŸ˜ƒ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…