Edward A Chapa
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 977
- 1,408
Acha udini wewe Mzee,kaa ulee wajukuu zako.
Hakuna anayekusifia
Hakuna anayekusifia
Kwahiyo vita ya majimaji, ilikuwa JIHAD??Yoso,
Hapana haja ya kunitukana.
Tunajadili historia hii unaeleza uyajuayo nami naeleza niyajuayo.
Sasa haya matusi ya nini?
Nimemuuliza Mwalimu Hussein Bashir ambae ameandika kitabu, ''Jihadi Kuu ya Maji Maji,'' ambacho ni kitabu kizuri sana kuhusu Vita Vya Maji Maji na yeye akanigusia kidogo tu kuhusu Bi. Khadija Mkomanile kama anavyozungumza hapo kwenye hiyo video.
Soma barua ya Chifu Songea bin Ruuf kwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:
''Asalaam Aleikum, Ninakuletea barua kupitia Kazembe.
Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini.
Tupo katika kupigananao hapa.
Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano.
Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea.
Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).
Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu.
Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa.
Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe.
Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.
Chupa hii, na daíwa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita. Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.
Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.
Hassan bin Ismail anakusalimu.
Salam nyingi,
Sultan Songea bin Ruuf.''
![]()
![]()
Khadija Mkomanile alisilimishwa dini na Mmatumbi Omar Kinjala aliyetumwa na Kinjekitile kuwaatarifu kuhusu dawa ya ajabu ambayo ingebadilisha risasi kuwa maji.. hakuwa na Uislamu wa kuzaliwa ..acha uongo wewe Mzee Mdini wa kutupwa..
Kwa hiyo kama vita vya majimaji vilikuwa ni Jihad ya Waislamu wazawa dhidi ya wakoloni wa kikristu.Yoso,
Hapana haja ya kunitukana.
Tunajadili historia hii unaeleza uyajuayo nami naeleza niyajuayo.
Sasa haya matusi ya nini?
Nimemuuliza Mwalimu Hussein Bashir ambae ameandika kitabu, ''Jihadi Kuu ya Maji Maji,'' ambacho ni kitabu kizuri sana kuhusu Vita Vya Maji Maji na yeye akanigusia kidogo tu kuhusu Bi. Khadija Mkomanile kama anavyozungumza hapo kwenye hiyo video.
Soma barua ya Chifu Songea bin Ruuf kwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:
''Asalaam Aleikum, Ninakuletea barua kupitia Kazembe.
Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini.
Tupo katika kupigananao hapa.
Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano.
Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea.
Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).
Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu.
Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa.
Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe.
Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.
Chupa hii, na daíwa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita. Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.
Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.
Hassan bin Ismail anakusalimu.
Salam nyingi,
Sultan Songea bin Ruuf.''
![]()
![]()
Yoso,
Hapana tatizo ikiwa wewe mwenyewe unaona lugha yako ni ya kistaarabu.
Uamuzi ni wangu kukukwepa au kukustahamilia.
Mpwimbe,Kwahiyo vita ya majimaji, ilikuwa JIHAD??
Eyce,Kwa hiyo kama vita vya majimaji vilikuwa ni Jihad ya Waislamu wazawa dhidi ya wakoloni wa kikristu.
Kwa hiyo wakristu wa kingoni na kabila zingine za kusini waliungana na wajerumani kupigana dhidi ya wazawa wenzao ambao walikuwa ni waislamu ?..
Je, hao wangoni na wamatumbi walio waislamu waliipigana hiyo vita dhidi ya uvamizi wa mkoloni au dhidi ya ukristu wa wajerumani ?...
Tangawizi,Mzee mdini umepitiliza...unapoteza muda wako tu. Nyerere ambaye amepewa hadhi ya baba wa Taifa, wewe hutakaa kubadilisha.
Andika unavyoweza kuandika ili kufurahisha kadamnashi ya watu wachache wenye akili kama wewe, for just nothing
Nadhani ungenipa ufafanuzi au taarifa mpya ambayo pengine inakinzana na kile nilichokisoma darasani ama online. Lakini pia mapokeo ya kihistoria ambayo wazee wa kusini wamekuwa wakiihadithia kwa miaka mingi kwa minajili ya kikabila na imani za kiasili na si kidini.Eyce,
Soma historia ya Maji Maji kuna mengi utajifunza.
Ukitegemea kuuliza hapa JF matokeo yake ni ubishi mkubwa.
Wapiganaji wa Maji Maji walikuwa wanawashambulia Wamishionari.
Lazima kutakuwa na sababu ya kufanya hivyo.
Tangawizi,Maandishi yake yamejikita katika kutaka tuamini kwamba, bila waislamu Tanganyika isingepata uhuru. Moja ya uongo mkubwa sana kuingiza kwenye ubongo wa mtu anayejitambua.
Uhuru wa Tanganyika, kama ilivyo sehemu nyingine, ulitafutwa na watanganyika. Hii ya kulazimisha dini moja ionekana superior, ndio inferiority complex yenyewe.
Kitu kimoja kinachonipa ujasiri wa kudharau huu ujinga ni kuwa, haitabadili lolote lile....uhuru umepatikana. Tuna mapambano mengine kabisa kwa sasa, ya kutafuta maendeleo ya kweli ya Taifa letu. Yakutafuta ethics na maadili mema ya viongozi wetu.
Yeye amelala usingizi wa pono...na waswahili wenzangu wanasema, aliyelala usimwamshe.....muda unazidi kuongea.
Eyce,Nadhani ungenipa ufafanuzi au taarifa mpya ambayo pengine inakinzana na kile nilichokisoma darasani ama online. Lakini pia mapokeo ya kihistoria ambayo wazee wa kusini wamekuwa wakiihadithia kwa miaka mingi kwa minajili ya kikabila na imani za kiasili na si kidini.
Kuhusu wamisionari kupigwa sidhani kama ni suala jipya maana hata kagera kuna vijiji ambavyo vina historia mbayaya kuwawinda mapadre na watawa kwa ajili ya chakula. Again ni dhahania
Ningependa unipe historia sahihi kama ambavyo huwa unazitoa hata za Abdul sykes pasipo kukwama
Je, kama vita vya majimaji vilikuwa ni Jihad. Je wenyeji wa kikristu waliungana na wajerumani kuwapiga wenyeji waislamu?..
Pamoja na maswali yangu mengine yaliyopita
Edward...Acha udini wewe Mzee,kaa ulee wajukuu zako.
Hakuna anayekusifia
Hili si suala la udini ni suala la kurekebisha historia iliyokuwa imejaa makosa.Mpumbavu na mdini naye huzeeka.
Kitabu kinaweza kuandikwa tu na mtu mwenye akili za kidini kama zako, anayejua kusoma na kuandika.Mpwimbe,
Kuna kitabu hicho hapo kisome:
Jihadi kuu ya Maji Maji, 1905-1907 : historia ya Uislamu pwani ya Azania
Author:Hussein Bashir Abdallah
Summary:On the Islamic involvement in the Maji Maji war of 1905-1907
Print Book, Swahili, 2011
Publisher: Islamic Sites Conservation, Dar es Salaam, 2011
Kwakweli huyu mzee ni tatizo...Ila mnapenda udini sana. Very stupid idiot.
Mpwimbe,Kitabu kinaweza kuandikwa tu na mtu mwenye akili za kidini kama zako, anayejua kusoma na kuandika.
Ni fikra tu, ambazo zinaweza kuwa za kijinga tu , zinahamishiwa kwenye maandishi.