Siku ya mashujaa: Bi. Khadija Mkomanile aliyebatizwa na kupewa jina la Jacinta kisha akanyongwa

Huyu mzee nadhani anapambana aina fulani ya mental health challenge sio mzima kabisa. Yaani ni religious fanatic m'moja asiyejitambua kwa level fulani.
 
Na linaendelea kuyumba kweli,
Mwanzo ilikua story zake tunasoma safi tu humu.
Alivyoanza,uislamu lololoolo,sykes hivi,Nyerere blah blah
Kakaa magomeni,mara gerezani,mara upanga.
Hapo ataruka kwenye misikiti,sijui shehe nani yaani dk ya mwisho utajua mzee mwehu huyu.
PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES

The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.

The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006

Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.

Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.

Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam

Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam

The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam

Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam

Sal Davis, An Autobiography, Readit/Amazon, 2023, Dar es Salaam

In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).

Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).

Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).

Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).

Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).

Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.

Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.

Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

Awards: Several Awards

Visiting Scholar: (2011)

University of Iowa, Iowa City, USA

Northwestern University, Chicago, Illinois, USA

Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

OTHER COUNTRIES VISITED

Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
Kinyungu,
Swali lako halijakaa sawasawa.
Katika majemadari 66/67 walionyongwa na kuzikwa katika kaburi la halaiki robo tatu walikuwa Waislam na ndiyo hawa waliobatizwa na Padri Yohannes Haffligger.

Swali lako linatakiwa liwe hawa makamanda Waislam pamoja na Nduna Abdulrauf Songea Mbano waliingia lini Uislam.

Haliladhalika Chief Hamin Massaninga ambae Nduna Abdulrauf Songea Mbano alimwandikia barua ya kutaka atume jeshi kwake waliingia lini Uislamu?
Hujajibu swali
 
Fundi,
Naanza na para ya kwanza.

Kwa utangulizi napenda nikufahamishe kuwa hayo uliyoandika mimi ndiye mtu wa kwanza
kuyaweka hadharani katika kitabu cha Abdul Sykes na ikiwa hukuyasoma kutoka kitabu hicho
utakuwa umeyapata kwa mtu ambaye kayasoma katika kitabu changu.
Hapana. Wewe sie mtu pekee uliyeandika kuhusu wakina Sykes. Hilo litakuwa ni kuji glorify ambacho sio kitu kizuri. Nimesoma kutoka andiko la Juma Mwapachu. Sasa tuambie kuwa wewe ulimjua Hamza mwapachu kuliko mwanae.
Hapo unaposema Mwapachu kwa kushirikiana na Abdul Sykes umetaja majina lakini liondoe jina
la Dr. Tsere kwani ilikuwapo TAA Political Subcommittee ambao wajumbe wake walikuwa: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes, Steven Abdallah Mhando na John Rupia.
Juma Mwapachu ameandika pia kuwa Dr. Tsere alikuwa interim President wa kwanza baada ya kuondolewa wazee wao. Dr. Tsere aliondoka kwenye nafasi hiyo baada ya kuhamishwa kwenda Tanga. Hao nilio wataja walikuwa viongozi wakuu na sio wajumbe wa kamati ndogo unayo i zungumzia wewe. Bila shaka kwa sababu Hamza Mwapachu alikuwa Katibu wa Uchumi na Stephen Mhando wa Elimu, walikuwa na watu waliofanya kazi nao. Hiyo kamati ndogo ya siasa ni moja tuu ya kamati ndogo nyingine.
Mshauri wa hii TAA Political Subcommitee alikuwa Earle Seaton.
Hiyo memorandum unayoieleza iliandikwa na TAA Political Sub Committee kwa msaada mkubwa wa Earle Seaton.

Lakini kulikuwa na Action Group ambayo wahusika wake walikuwa Hamza Mwapachu, Dr. Luciano Tsere na Dr. Kyaruzi.

Kwa ajili hii hii memorandum ilichangiwa na Action Group na TAA Political Subcommittee.
Nilidhani ulisema Dr. Tsere hakuhusika?
Haya nimeyapata kutoka kwa Nyaraka za Sykes na Mswada wa kitabu, ''The Muhaya Doctor'' mwandishi akiwa Dr.
Kyaruzi.

Ningeweza kusema mengi lakini nachelea jibu hili lisiwe refu sana.
Sawa. Na mimi niliyoandika nimepata kutoka kwenye andiko la Juma Mwapachu. Naona umesahau kumtaja Judith Listowel ambae ulishawahi kusema kuwa kitabu chake kilikusaidia sana.
Mswada huu ''Muhaya Dr. upo Maktaba na nilipewa na marehemu Hamza Mwapachu na yeye alipewa na Dr. Kyaruzi.

Hakuna aliyepata kuyajua haya mapaka mimi nilipoyaeleza katika: The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,'' Minerva Press, London 1998.
Hamza Mwapachu alifariki mwaka 1962. Sijui ulikuwa umri gani wakati ule mpaka uwe umeisha anza utafiti kwa ajili ya kitabu ulicho andika 1998. Aidha, sidhani kama Dr. Kyaruzi alikuwa na nakala moja tu ya manuscript yake ambayo aliiandika 1961, mwaka mmoja kabla ya Hamza Mwapachu kufariki. Na Mwapachu nae akakupa nakala yake mara tuu baada ya kupewa na Dr. Kyaruzi. The math does not mathing.
Para ya pili.

Mazungumzo ya kuibadili TAA kuwa chama cha siasa yalianza mwaka wa 1950 kati ya Hamza Mwapachu na Abdul Sykes na Abdul yeye alimtaka Chief David Kidaha Makwaia aje TAA wampe urais wa TAA kisha waunde TANU.

Mazungumzo ya jambo hili kati ya Abdul Sykes na Chief Kidaha hayakuzaa matunda.

Mwaka wa 1953 miezi ya mwanzo Abdul Sykes akiongozana na Ali Mwinyi Tambwe alikwenda Nansio, Ukerewe
kwa Hamza Mwapachu kutaka fikra zake kuhusu Nyerere kuingizwa katika uongozi wa juu wa TAA katika uchaguzi uliokuwa unakaribia mwezi April.

Abdul Sykes wakati huu alikuwa Act. President na Secretary wa TAA.
Mazungumzo kuhusu Nyerere kushika uongozi wa TAA yalikuwa yameanza kabla ya Sykes na Tambwe kwenda Ukerere kuonana na Mwapachu. Naamini walifanya hivyo baada ya Mwapachu kumpigia debe sana rafiki yake Nyerere ambae wao walikuwa hawamfahamu vizuri ingawa aliwahi kuhudhuria mkutano wa TAA Dar 1946. Akiwa masomoni Edinburg, Nyerere alikuwa anawasiliana sana na Mwapachu. Na bila shaka yaliendelea hata baada ya kurudi Tanganyika 1952 na kuhamia Pugu 1953.
Hamza Mwapachu alimwambia Abdul yeye akiachie kiti cha urais wa TAA achukue Nyerere na amsaidie ashinde uchaguzi ule.
Kama Mwapachu ndie aliyemshauri Abdul ampishe Nyerere utasemaje Abdul ndie aliyemuingiza Nyerere kwenye uongozi wa TAA?
Ikiwa haya mimi nimeandika katika kitabu cha Abdul Sykes vipi utasema kuwa sijampa uzito Hamza Mwapachu?

Mimi ndiyo mwandishi wa kwanza kuyaweka haya hadharani na waliposoma watu kishindo kikubwa kilisikika.
Yapo mengi.

Historia hii haikamiliki bila ya kumtaja Schneider Abdillah Plantan na Uchaguzi wa Rais wa TAA kati ya Abdul Sykes na Nyerere Ukumbi wa Arnautoglou tarehe 17 April, 1953.
Kuandika kitabu cha Abdul Sykes hakumaanishi kuwa ulimpa uzito na heshima aliyostahili Mwapachu. Katika maandiko yako, unajaribu sana kuonyesha wakina Sykes ndio walikuwa Alpha na Omega wa juhudi za kutafuta uhuru nchini Tanganyika.
Schneider Abdillah Plantan alikuwa mzulu na ndugu wa wakina Sykes. Koo hizi zililetwa German East Africa ili kuwakandamiza waafrika waliokuwepo. Walitoka kwenye kijiji cha Kwa Likunyi Msumbiji na waliwasaidia wajerumani kumkamata Abushiri bin Salim bin Harith aliyekuwa anapinga utawala wa kijerumani. Abushiri alinyongwa Pangani mwaka 1889.
Hauwezi kuzungumzia historia ya mchango wa waislamu katika kugombea uhuru bila kuzungumzia mchango wa TAMU ( Tanganyika AfricanMuslim Association). Kuna article imeandikwa na James R Brennam inayozugumzia hili kwa ufasaha mkubwa.

Historia ya Tanzania ni complicated na watu wa kutoka dini zote walishiriki katika ukandamizaji na ukombozi wa nchi yao. Waislamu wakina Plantan walishirikiana na wakristu wa kijerumani kuzima moto uliowashwa na muislamu mwenzao Abushiri. Inawezekana kabisa kuwa wao walimuona zaidi Abushiri kama muarabu mgandamizaji kuliko muislamu mwenzao.

Amandla...
 
Hapana. Wewe sie mtu pekee uliyeandika kuhusu wakina Sykes. Hilo litakuwa ni kuji glorify ambacho sio kitu kizuri. Nimesoma kutoka andiko la Juma Mwapachu. Sasa tuambie kuwa wewe ulimjua Hamza mwapachu kuliko mwanae.

Juma Mwapachu ameandika pia kuwa Dr. Tsere alikuwa interim President wa kwanza baada ya kuondolewa wazee wao. Dr. Tsere aliondoka kwenye nafasi hiyo baada ya kuhamishwa kwenda Tanga. Hao nilio wataja walikuwa viongozi wakuu na sio wajumbe wa kamati ndogo unayo i zungumzia wewe. Bila shaka kwa sababu Hamza Mwapachu alikuwa Katibu wa Uchumi na Stephen Mhando wa Elimu, walikuwa na watu waliofanya kazi nao. Hiyo kamati ndogo ya siasa ni moja tuu ya kamati ndogo nyingine.

Nilidhani ulisema Dr. Tsere hakuhusika?

Sawa. Na mimi niliyoandika nimepata kutoka kwenye andiko la Juma Mwapachu. Naona umesahau kumtaja Judith Listowel ambae ulishawahi kusema kuwa kitabu chake kilikusaidia sana.

Hamza Mwapachu alifariki mwaka 1962. Sijui ulikuwa umri gani wakati ule mpaka uwe umeisha anza utafiti kwa ajili ya kitabu ulicho andika 1998. Aidha, sidhani kama Dr. Kyaruzi alikuwa na nakala moja tu ya manuscript yake ambayo aliiandika 1961, mwaka mmoja kabla ya Hamza Mwapachu kufariki. Na Mwapachu nae akakupa nakala yake mara tuu baada ya kupewa na Dr. Kyaruzi. The math does not mathing.

Mazungumzo kuhusu Nyerere kushika uongozi wa TAA yalikuwa yameanza kabla ya Sykes na Tambwe kwenda Ukerere kuonana na Mwapachu. Naamini walifanya hivyo baada ya Mwapachu kumpigia debe sana rafiki yake Nyerere ambae wao walikuwa hawamfahamu vizuri ingawa aliwahi kuhudhuria mkutano wa TAA Dar 1946. Akiwa masomoni Edinburg, Nyerere alikuwa anawasiliana sana na Mwapachu. Na bila shaka yaliendelea hata baada ya kurudi Tanganyika 1952 na kuhamia Pugu 1953.

Kama Mwapachu ndie aliyemshauri Abdul ampishe Nyerere utasemaje Abdul ndie aliyemuingiza Nyerere kwenye uongozi wa TAA?

Kuandika kitabu cha Abdul Sykes hakumaanishi kuwa ulimpa uzito na heshima aliyostahili Mwapachu. Katika maandiko yako, unajaribu sana kuonyesha wakina Sykes ndio walikuwa Alpha na Omega wa juhudi za kutafuta uhuru nchini Tanganyika.
Schneider Abdillah Plantan alikuwa mzulu na ndugu wa wakina Sykes. Koo hizi zililetwa German East Africa ili kuwakandamiza waafrika waliokuwepo. Walitoka kwenye kijiji cha Kwa Likunyi Msumbiji na waliwasaidia wajerumani kumkamata Abushiri bin Salim bin Harith aliyekuwa anapinga utawala wa kijerumani. Abushiri alinyongwa Pangani mwaka 1889.
Hauwezi kuzungumzia historia ya mchango wa waislamu katika kugombea uhuru bila kuzungumzia mchango wa TAMU ( Tanganyika AfricanMuslim Association). Kuna article imeandikwa na James R Brennam inayozugumzia hili kwa ufasaha mkubwa.

Historia ya Tanzania ni complicated na watu wa kutoka dini zote walishiriki katika ukandamizaji na ukombozi wa nchi yao. Waislamu wakina Plantan walishirikiana na wakristu wa kijerumani kuzima moto uliowashwa na muislamu mwenzao Abushiri. Inawezekana kabisa kuwa wao walimuona zaidi Abushiri kama muarabu mgandamizaji kuliko muislamu mwenzao.

Amandla..
Fundi,
Hapana tatizo,
Nimekueleza niyajuayo na ikiwa huyaamini kwangu yote sawa.

Niwie radhi nimekosea mswada wa Dr. Kyaruzi kanipa Juma Mwapachu.
 
Fundi...
Sina cha kujifunza katika historia ya Maji Maji kwani tayari nimejifunza na kuandika mengi.
Hebu tuanze na kipande hicho hapo chini:

​
Vita vya Maji Maji vilipoanza kusini ya Tanganyika mwaka 1905 kwa nia ya kuwafukuza Wajerumani kutoka Tanganyika, zile sehemu zenye Wakristo wengi zilikataa kujiunga na vita na badala yake wakajiunga na majeshi ya Wajerumani na kupigana bega kwa bega dhidi ya wazalendo. Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumani ulianza katika maeneo yenye Waislam wengi na vita vikachukua sura ya vita vya Kiislamu dhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo. Kwa kuwa wamishonari walikuwa washirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituo vyao vinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji. Kutokana mashambulizi haya, Wakristo walivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. Harakati za Maji Maji zilishindwa na Wajerumani walifanya fisadi kubwa dhidi ya wananchi na viongozi wao. Jambo hili liliacha kovu kubwa katika fikra za wananchi na kwa upande wa Wakristo ambao walinusurika na ghadhabu ya Wajerumani, wengi wao wakajiweka mbali na aina yoyote ya kupinga ukoloni.​

​
​
​
003_3.JPG
Selemani Mamba Shujaa wa Vita vya Maji Maji Aliyenyongwa
na Wajerumani. Selemani Mamba alikuwa Kiongozi wa Wamwera.
Viongozi Wengine Walionyongwa walikuwa Kinjikitile Ngwale Kiongozi
wa Wamatumbi, Abdallah Chiami Kiongozi wa Wangindo, Mataka Ambuje
Kiongozi wa Wayao na Songea Rauf Mbano Kiongozi wa Wangoni

​
(TANU Ilivyovunja Ngome ya Kanisa Katoliki Jimbo la Kusini, 1955 Sehemu ya Kwanza)

Selemani Mamba naye alimuua Askofu wa Kijerumani Kassian Spiss Mikukuyumbu, Liwale, Lindi.

Haya uliyoandika ya askari wa kukodi yaani mamluki kutoka Afrika Kusini - Chief Mohosh Shangaan na Sykes Mbuwane hawa walitokea Imhambane, Mozambique kijiji kinachoitwa kwa Likunyi na waliletwa German Ostafrika na Hermann von Wissman.

Haya uliyoandika yametoka kwangu yamo katika kitabu cha Abdul Sykes na mimi nimeyapata kutoka kumbukumbu za Sykes na zipo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam toka mwaka wa 1968.

Sykes Mbuwane hakupigana Maji Maji yeye alipigana na Bushiri bin Salim kisha Mkwawa na walipokuwa wakitoka Kalenga baada ya kumshinda Sykes Mbuwane akafa maji Mto Ruaha.

Askari wa Kizulu walipigana Maji Maji na hawa nimewajua kwa kuyasoma majina yao katika Nyaraka za Sykes ni pamoja na Chief Mohosh Shangaan (Afande Plantan), Chakullan na Machakaomo.

Hii ndiyo tofauti yangu kubwa na nyie.
Mimi nilifunguliwa Nyaraka za Sykes na nikasoma mafaili yote.

Sikuandika kwa kubahatisha.
Mtu yeyote anayeandika kuwa hana la kujifunza ni kuwa hajaelimika. Hakuna msomi anaeweza kusema kuwa hana la kujifunza.
Ukiangalia sentensi yako ya kwanza tuu inaonyesha upotoshaji wako. Nantabila na wenzake hawakung'oa miche ya pamba kwa sababu walitaka kumng'oa mjerumani kutoka Tanganyika ( Tanganyika hata haikuwepo). Walifanya hivyo kwa sababu waliona kuwa wajerumani na vibaraka wake ( akiwemo Akida muislamu Seif bin Amir) walikuwa hawawatendei haki kwa kuwalazimisha kulima kwenye mashamba yao, kulipishwa kodi kubwa na wao kulazimishwa kulima pamba. Wakina Nantabila walipigana kabila zao na sio kwa sababu za dini kama unavyotaka kutuaminisha.
Sijasema Sykes alipigana katika vita vya Maji Maji bali wazulu wenzake walishiriki katika vita hiyo. Hao askari wa kizulu ambao walipigana katika vita ya Maji Maji walikodishwa na wajerumani. Hawa hawakujali kuwa ndani ya wamatumbi walikuwepo waislamu wenzao, waliwafyeka tu. Hii ilichangia na imani yao kuwa walikuwa karibu zaidi na wazungu kwa sababu walikuwa schutztruppen.

Wewe kutegemea simulizi na maandiko ya upande mmoja ndio weakness kubwa ya maandishi yako. Ndio maana maandiko yako hayawi cited na academics wengi katika tafiti zao. Kusema nilifunguliwa kabati na wakina Sykes sio ushahidi wa kutosha wa kufanya maandiko yako yaaminiwe. Ili yaaminiwe ilipaswa kuwa na sources nyingi zaidi ya hao ndugu zako. Utaaminiwa na selective audience unayoiandikia ambao wengi wana sence of victimhood. Wanapenda maandiko yako kwa sababu yana validate imani yao kuwa wamedhulumiwa haki yao na wagalatia. Imani kama hizi zinaweza kutupeleka kubaya kama taifa.

Amandla...
 
Fundi,
Hapana tatizo,
Nimekueleza niyajuayo na ikiwa huyaamini kwangu yote sawa.

Niwie radhi nimekosea mswada wa Dr. Kyaruzi kanipa Juma Mwapachu.
Unaona sasa! Nisingekusahihisha watu wangeamini kuwa ulikuwa karibu na Hamza Mwapachu kwa hiyo hamna anayejua habari zake kuliko wewe. Maandishi yako yana dosari nyingi kama hizi kwa sababu unaamini unajua kila kitu kuhusu unachokiandika na, unfortunately, hiyo ajenda yako ya udini.

Amandla....
 
Mpwimbe,
Sykes walifutwa katika historia ya TANU.

Nimeandika historia yao na mchango wao katika kuasisiwa kwa African Association na Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika hadi TANU.

Hayo ya Uzaramo na mengine sijui yanaingiaje katika huu mjadala.

Kitabu cha Sykes kimebadili historia yote ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere.
Wewe Mzee wa ovyo saana
 
Mtu yeyote anayeandika kuwa hana la kujifunza ni kuwa hajaelimika. Hakuna msomi anaeweza kusema kuwa hana la kujifunza.
Ukiangalia sentensi yako ya kwanza tuu inaonyesha upotoshaji wako. Nantabila na wenzake hawakung'oa miche ya pamba kwa sababu walitaka kumng'oa mjerumani kutoka Tanganyika ( Tanganyika hata haikuwepo). Walifanya hivyo kwa sababu waliona kuwa wajerumani na vibaraka wake ( akiwemo Akida muislamu Seif bin Amir) walikuwa hawawatendei haki kwa kuwalazimisha kulima kwenye mashamba yao, kulipishwa kodi kubwa na wao kulazimishwa kulima pamba. Wakina Nantabila walipigana kabila zao na sio kwa sababu za dini kama unavyotaka kutuaminisha.
Sijasema Sykes alipigana katika vita vya Maji Maji bali wazulu wenzake walishiriki katika vita hiyo. Hao askari wa kizulu ambao walipigana katika vita ya Maji Maji walikodishwa na wajerumani. Hawa hawakujali kuwa ndani ya wamatumbi walikuwepo waislamu wenzao, waliwafyeka tu. Hii ilichangia na imani yao kuwa walikuwa karibu zaidi na wazungu kwa sababu walikuwa schutztruppen.

Wewe kutegemea simulizi na maandiko ya upande mmoja ndio weakness kubwa ya maandishi yako. Ndio maana maandiko yako hayawi cited na academics wengi katika tafiti zao. Kusema nilifunguliwa kabati na wakina Sykes sio ushahidi wa kutosha wa kufanya maandiko yako yaaminiwe. Ili yaaminiwe ilipaswa kuwa na sources nyingi zaidi ya hao ndugu zako. Utaaminiwa na selective audience unayoiandikia ambao wengi wana sence of victimhood. Wanapenda maandiko yako kwa sababu yana validate imani yao kuwa wamedhulumiwa haki yao na wagalatia. Imani kama hizi zinaweza kutupeleka kubaya kama taifa.

Amandla...
Mchundo,
Kuna citation kubwa kuliko Cambridge Journal of African History?

Kuna citation kubwa kuliko Dictionary of African Biography (DAB)?

Nimo kote humo.
Hujasoma Nyerere Biography?
 
Kinyungu,
Swali lako halijakaa sawasawa.
Katika majemadari 66/67 walionyongwa na kuzikwa katika kaburi la halaiki robo tatu walikuwa Waislam na ndiyo hawa waliobatizwa na Padri Yohannes Haffligger.

Swali lako linatakiwa liwe hawa makamanda Waislam pamoja na Nduna Abdulrauf Songea Mbano waliingia lini Uislam.

Haliladhalika Chief Hamin Massaninga ambae Nduna Abdulrauf Songea Mbano alimwandikia barua ya kutaka atume jeshi kwake waliingia lini Uislamu?
Uislamu wao utakuwa na maana tu kama walikuwa wanapigana ili kuanzisha Caliphate itakayo chukua nafasi ya utawala wa kigalatia. Wengi wa hawa walikuwa wanapigania makabila yao bila kujali dini zao. Mimi sijawahi kusikia Caliphate yeyote iliyokuwepo sehemu ambayo ilikuja kuwa Tanganyika. Sijawahi kusikia chifu yeyote nje ya Zanzibar, Kilwa n.k. ambae alitawala kiislamu. Kwa wengi wao imani zao za kiasili zilikuwa zina nafasi kubwa zaidi ya uislamu au ukristu. Hao wote walikuwa wanafanya matambiko yaliyopingana na ukristu na uislamu.

Amandla...
 
Mchundo,
Kuna citation kubwa kuliko Cambridge Journal of African History?

Kuna citation kubwa kuliko Dictionary of African Biography (DAB)?

Nimo kote humo.
Hujasoma Nyerere Biography?
Naona haujui maana ya citation. Citation sio kuwekwa kwenye journal au dictionary. Citation ni waandishi wengine kutumia maandishi yako katika kujenga hoja za maandiko yao. Na hiyo ya Dictionary of African Biography ni uliandika kuhusu Kleist Sykes tu. Hapana, maandiko yako hayana uzito wowote katika academia.

Siwezi kudai chochote.
Labda nikueleze kuwa huenda hunijui vyema.

Hili halina lawama.

Lakini nimealikwa katika vyuo kadhaa hapa nyumbani na nje ya mipaka kuzungumza.

Nimetiwa kwenye miradi kadhaa na wachapaji
wakubwa kuandika vitabu vya historia.

Hakika sijui maana ya citation na sijui mengi.
 
Fundi,
Siwezi kudai chochote.
Labda nikueleze kuwa huenda hunijui vyema.

Hili halina lawama.

Lakini nimealikwa katika vyuo kadhaa hapa
nyumbani na nje ya mipaka kuzungumza.

Nimetiwa kwenye miradi kadhaa na wachapaji
wakubwa kuandika vitabu vya historia.

Hakika sijui maana ya citation na sijui mengi.
Hivyo vyote ni vitu vyema na una stahili pongezi. Lakini bado nasema impact ya maandishi yako sio kubwa katika academia kama ambavyo unaamini.

Just out of curiosity, mara ya mwisho kualikwa kuzungumza katika chuo nje ya nchi na ilikuwa chuo kipi? Na kitabu chako cha mwisho kuchangia kilikuwa kipi? Nauliza maswali haya maana maandiko mengi unayojisifia ( rightly so) ni ya 1990s.

Back
Top Bottom