Siku ya mashujaa: Bi. Khadija Mkomanile aliyebatizwa na kupewa jina la Jacinta kisha akanyongwa

Siku ya mashujaa: Bi. Khadija Mkomanile aliyebatizwa na kupewa jina la Jacinta kisha akanyongwa

Mzee udini umekujaa kwelikweli. Reference zenyewe unatupeleka kwenye maandiko yenu. Hutupeleki sehemu neutral za zamani. Siku hizi mnabadirisha historia hadi Wikipedia.
Tutafika tu.
Naweka rejea zetu kwa kuwa sisi ndiyo waasisi wa African Association na TANU.
Tuna mswada wa kitabu na nyaraka nyingine zinakwenda nyuma sasa miaka 100.

Hizi ndizo zinazosaidia kueleza historia yetu.
Hata kama nitataka kutumia rejea nje ya hizi zitatoka wapi?

Mimi sijapata kuandika chochote Wikipedia kitabu cha Abdul Sykes kinatosha kueleza
yote katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Kwakweli huyu mzee ni tatizo...

Kinjeketile Ngwale kumbe alipigana jihad?

Hahaha daah!

Na kumbe ile dawa ya maji ilikuwa ina uhusiano na Muhamed!!!

Kwa ninavyowajua waisilamu kama ile dawa ingekua na uhusiano na dini yao...

Badala ya Kinjikitile kuwaambia watu wake watamke maji, nina uhakika angewaambia watamke Takbiir...

Huu ujinga wa kila kizuri cha hii nchi kuhusishwa na Uislamu huyu mzee anatoa wapi?
Nyakubonga,
Hayo yote uliyoandika yapo katika rejea na ndiyo ukweli wenyewe.
Vipi mtu atatafsiri hilo ni jambo lingine.
 
Karne hii tunahangaika na dini kweli , acha kutuhaibisha bwana
Kulagha...
Hakuna dini hapa kuwa mtu anasomesha itikadi.
Mimi nimeandika kitabu kilichosahihisha historia ya Julius Nyerere katika TANU.

Hili si suala la dini hii ni ''Field of Enquiry'' katika utafiti wa kisomi.

Kitabu cha Abdul Sykes kimependwa na kimechapwa mara nne sasa kinakwenda
toleo la tano.

1785216798178.png
 
Mpwimbe,
Kitabu cha Abdul Sykes kilipotoka kwa mara ya kwanza hakuna aliyenitukana.
Kulikuwa na kishindo kikubwa kwa yale mapya ambayo hayakupata kufahamika.

Mathalan kuwa chanzo cha African Association ni mazungumzo kati ya Kleist Sykes
na Dr. Kwegyri Aggrey mwaka wa 1924 chama kuundwa mwaka wa 1929.

Kuonekana majina ya waasisi wa African Association Waislam 6 na Wakristo 3 na
maelezo kwa nini hali ilikuwa hivi.

Kueleza kupokelewa kwa Nyerere na akina Sykes na kuundwa kwa TANU na maelezo
ya kadi za TANU kuwa Abdul Sykes kadi No. 3, Ally Sykes kadi No. 2 na Julius Nyerere
kadi no 1 na historia nzima ya kusajili TANU na mengine mengi.

Hii ni historia ambayo haikuwa inafahamika.

Ikawa kama vile watu wamepigwa na butwaa wanashangaa vipi historia ya TANU
imeandikwa haya hayakuelezwa.

Matusi, kebehi na kejeli na shutuma za udini dhidi yangu zilikuja baadae sana.
Na haya ni hapa JF peke yake.

Kote nilikofika na kuzungumza kuhusu historia hii ilipokelewa vyema.
Kina Nyerere hawakupigania UHURU wa kidini.

AA hakikua chama cha siasa.

Tanganyika yote kulikuwa na vugu vugu la kupinga UKOLONI, na siyo kwasababu ya dini za wakoloni.

Wewe mwenyewe uko hapa unajaribu kujenga hoja ya kijinga, kuwa Majimaji ilikuwa ni JIHAD.

Kwahiyo Dawa aliyotoa Kinjekitile kuwapa askari, inatokana na mwongozo upi wa Quran??

Dini za watu, ni imani zao binafsi.

Haziwezi kuhalalisha JEMA au BAYA la MTU.

MWARABU, MJERUMANI, MUINGEREZA wote walikuwa wakoloni, na watanganyika walipigana nao kupata uhuru.

Hizi stori zako, simulianeni misikitini na kwenye vijiwe huko Gerezani.
 
Mpwimbe,
Kitabu cha Abdul Sykes kilipotoka kwa mara ya kwanza hakuna aliyenitukana.
Kulikuwa na kishindo kikubwa kwa yale mapya ambayo hayakupata kufahamika.

Mathalan kuwa chanzo cha African Association ni mazungumzo kati ya Kleist Sykes
na Dr. Kwegyri Aggrey mwaka wa 1924 chama kuundwa mwaka wa 1929.

Kuonekana majina ya waasisi wa African Association Waislam 6 na Wakristo 3 na
maelezo kwa nini hali ilikuwa hivi.

Kueleza kupokelewa kwa Nyerere na akina Sykes na kuundwa kwa TANU na maelezo
ya kadi za TANU kuwa Abdul Sykes kadi No. 3, Ally Sykes kadi No. 2 na Julius Nyerere
kadi no 1 na historia nzima ya kusajili TANU na mengine mengi.

Hii ni historia ambayo haikuwa inafahamika.

Ikawa kama vile watu wamepigwa na butwaa wanashangaa vipi historia ya TANU
imeandikwa haya hayakuelezwa.

Matusi, kebehi na kejeli na shutuma za udini dhidi yangu zilikuja baadae sana.
Na haya ni hapa JF peke yake.

Kote nilikofika na kuzungumza kuhusu historia hii ilipokelewa vyema.
Mzee wangu, vuguvugu la uhuru lililofanyikia Dar ambayo wengi walioishi na kushikilia milango ya jiji walikuwa waislamu, je ulitegemea kwa upande huo wakristu wawe wengi zaidi ?..

Let's say vuguvugu lingeanzia kilimanjaro na wahusika wote wakawa wakristu ina maana ni sahihi kusema uhuru wa nchi hii uliletwa na wakristu na si watanganyika ?..

Historia ya nchi hii imejengwa ka inclusion. Wapigania uhuru hawatazamwi kwa dini, kabila au nasaba zao na ndio umekuwa msingi wa amani na ustawi wa taifa hili.

Je, kama tukianza kuangalia vitu kwa minajili ya tofauti zetu, huoni hilo litatengeneza mpasuko ambao haujawahi kutokea kwq mfano

Rwanda, utusi na uhutu haukuanza kwa utofauti wa pua zao ila ni kabila fulani kuona zinashushwa au zinastahili kupata zaidi.

Huoni unachokitengeneza ni zaidi ya kurekebisha historia
 
Vugu vugu la Uhuru halikuanzia Dar.

Dar palikuwa HQ.

Kila jamii, ilikuwa busy kupambana na Mkoloni kivyake.

Uongozi wa Nyerere ndio ulitumika kuunganisha makundi yote nchi nzima, na HQ ya mapambano yakawa Dar.

Na alifanya ziara nchini kote.
 
Mzee Said ni nani alikudanganya kila unachoandika kwenye vitabu vyako ndio ukweli?
Nyakabongo,
Nafanya utafiti kabla ya kuandika.

Tuchukulie kitabu cha Abdul Sykes.

Nieleze lipi katika kitabu hiki si kweli?

Kuwa baba yake si muasisi wa African Association?

Kuwa baba yake hakujenga ofisi ya African Association Mtaa wa New Street na Kariakoo?

Baba yake si muasisi wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika)?

Kuwa Abdul Sykes si aliyemleta Nyerere katika uongozi wa TAA?

Kuwa Abdul Sykes kadi yake si no. 3 na hakuishi na Mwalimu nyumbani kwake?

Nk. nk.
 
Nyakabongo,
Nafanya utafiti kabla ya kuandika.
Tuchukulie kitabu cha Abdul Sykes.

Nieleze lipi katika kitabu hiki si kweli?
Kuwa baba yake su muasisi wa African Association?

Kuwa baba yake hakujenga ofisi ya African Association Mtaa wa New Street na Kariakoo?

Kuwa Abdul Sykes si aliyemleta Nyerere katika uongozi wa TAA?

Kuwa Abdul Sykes kadi yake si no. 3 na hakuishi na Mwalimu nyumbani kwake?

Nk. nk.
Kwanini unam-group Sykes kama MUISLAM na siyo kama MZARAMO, Mwana MZIZIMA, Mtanganyika, Mwana GEREZANI au KATIBU wa TANU??
 
Mpwimbe,
Kuna kitabu hicho hapo kisome:

Jihadi kuu ya Maji Maji, 1905-1907 : historia ya Uislamu pwani ya Azania​

Author:Hussein Bashir Abdallah

Summary:On the Islamic involvement in the Maji Maji war of 1905-1907

Print Book, Swahili, 2011
Publisher: Islamic Sites Conservation, Dar es Salaam, 2011
Mpaka hatua hii, nimeamini pasina shaka kua "ili uwe muislam ni lazima urukwe na akili."
 
Kwanini unam-group Sykes kama MUISLAM na siyo kama MZARAMO, Mwana MZIZIMA, Mtanganyika, Mwana GEREZANI au KATIBU wa TANU??
Mpwimbe,
Sykes walifutwa katika historia ya TANU.

Nimeandika historia yao na mchango wao katika kuasisiwa kwa African Association na Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika hadi TANU.

Hayo ya Uzaramo na mengine sijui yanaingiaje katika huu mjadala.

Kitabu cha Sykes kimebadili historia yote ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere.
 
Mpwimbe,
Kuna kitabu hicho hapo kisome:

Jihadi kuu ya Maji Maji, 1905-1907 : historia ya Uislamu pwani ya Azania​

Author:Hussein Bashir Abdallah

Summary:On the Islamic involvement in the Maji Maji war of 1905-1907

Print Book, Swahili, 2011
Publisher: Islamic Sites Conservation, Dar es Salaam, 2011
Vita ya Maji Maji ilianza tarehe 20 Julai 1905 wakati mwanamke Nantabila Naupunda aliyeongozana na wanaume wawili Ngulumbalyo Mandai na Lindimyo Machali waling'oa miche ya mazao ya pamba kwenye shamba la serikali ya kikoloni lililokuwa katika kijiji cha Nandete. Muarabu mu Omani Seif bin Amri aliyekuwa Akida wa serikali ya kikoloni aliposikia hivyo akatuma watu wake kuwashughulikia. Watu wake wakashindwa kuwatuliza wakina Naupunda hivyo akakimbilia Kitumbi Mwando ambako alijifungia ndani na tarehe 28 Julai aliwaandikia barua mabosi wake kuwaomba msaada kuwa hali imekuwa mbaya. Wamatumbi walipofika nyumbani kwake wakakuta kesha kimbia. Siku hiyo hiyo wamatumbi wakamuua mjerumani mmoja aliyekuwa anaitwa Hopner. Vita ya kwanza kati ya waMatumbi na Wajerumani ilipigwa katika kijiji cha Samanga ambapo wajerumani walishindwa na biashara nyingi za wahindi zilichomwa moto. Mpaka kufika mwezi Agosti wangindo, wapogoro, wakichi na wazaramo walijiunga na wamatumbi.

Ukiangalia utaona kuwa mtu aliyewachomea wakina Naupunda alikuwa muislamu wa kiarabu. Nasema muislamu wa kiarabu kwa sababu bila shaka ndani ya wamatumbi walikuweko waislamu kutokana na historia ya pwani ya Tanganyika. Wamatumbi waislamu walitanguliza umatumbi wao sio uislamu wao katika vita hii. Wao na wenzao walikuwa wanapambana na serikali ya mgeni aliyekuwa anataka kuwadhulumu na kuwanyanyasa katika nchi yao wenyewe. Hawakuwa wanatetea uislamu dhidi ya wakoloni wa kikristu. Hata baadhi ya wakristu nao walijiunga nao. Hivyo hivyo, kama tulivyoona, kuna waislamu walioshirikiana na wakoloni kama ambavyo walikuweko pia wakristu waliokuwa upande wa wakoloni.

Pamoja na hayo wengi walikuwa wamejikita zaidi katika imani zao za asili kuliko uislamu ndio maana ilikuwa rahisi wao kumkubali Kinjeketile. Na katika askari waliotumiwa na wajerumani kuzima walichoona kuwa ni uasi walikuwa askari wa kukodi wakizulu kutoka Afrika ya Kusini. Mmoja wa askari hao wakukodi alikuwa ni Sykes Mbuwane, baba yake Kleist Sykes ambae mama yake alikuwa mnyaturu. Kleist Sykes aliyezaliwa 1894 alijiunga na jeshi la wajerumani wakati wa vita ya kwanza ya dunia. Wajukuu wa askari wa kukodiwa Sykes Mbuwane, Ally, Abdulwahid na Abbas walikuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukoloni wa kiingereza. Katika mapambano hayo walishirikiana na wakristu Dr. Vedastus Kyalakishaija Kyaruzi na Julius Nyerere. Nao hawakupambana kama waislamu bali kama watanganyika.

Kitabu hiki kwa kuangalia vita ya Maji Maji kwa mtazamo wa kidini kinakosa uhalali na kinageuka kuwa propaganda. Hii inasikitisha sababu bila shaka nae ana mengi ya kutufunza juu ya wakati huu muhimu katika historia yetu.

Amandla....

JokaKuu
 
Nyakabongo,
Nafanya utafiti kabla ya kuandika.

Tuchukulie kitabu cha Abdul Sykes.

Nieleze lipi katika kitabu hiki si kweli?

Kuwa baba yake si muasisi wa African Association?

Kuwa baba yake hakujenga ofisi ya African Association Mtaa wa New Street na Kariakoo?

Baba yake si muasisi wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika)?

Kuwa Abdul Sykes si aliyemleta Nyerere katika uongozi wa TAA?

Kuwa Abdul Sykes kadi yake si no. 3 na hakuishi na Mwalimu nyumbani kwake?

Nk. nk.
Nyerere hakuletwa na Abdul Sykes. Rafiki wa Nyerere alikuwa Hamza Mwapachu ambae wakati wako pamoja Makerere na Tibandebaga walianzisha chama cha wanafunzi wa kitanganyika (Tanganyika Welfare Students Association) na waliwasiliana uongozi wa TAA ili kiwe tawi lake Makerere. Hao marafiki watatu wakiwa Tabora walijiunga na tawi la TAA Tabora. Mwaka 1946, Mwapachu alichaguliwa kuwa mwenyekiti, Nyerere Katibu na Tibandebage Mweka Hazina wa TAA Tabora. Mwapachu alianza kazi kama Welfare Officer Ilala 1949. Mwapachu kwa kushirikiana na Abdulwahid Sykes, Dr. Lucian Tsere, Dr. Vedast Kyaruzi, Stephen Mhando na John Rupia ( waislamu wawili na wakristu wanne) walifanya mapinduzi TAA. Mapinduzi hayo yaliongozwa na Mwapachu na Sykes ambao inasemekana walitumia nguvu kung'oa uongozi wa wazee wao. Baada ya mapinduzi Tsere alichaguliwa kuwa Rais wa muda. Baada ya uchaguzi Dr. Kyaruzi alichaguliwa kuwa Rais, Abdulwahid Sykes Katibu Mkuu, John Rupia Mweka Hazina, Hamza Mwapachu Katibu wa Uchumi na Stephen Mhando Katibu wa Elimu. Inasemekana memorandum iliyopelekwa UN iliyodai muelekeo kuelekea uhuru iliandikwa kwa kiasi kikubwa na Hamza Mwapachu.

Mwapachu alihamishiwa Ukerere ambako alikutana na Paul Bomani. Na ni Mwapachu ndie aliyeanza mazungumzo na Nyerere mwaka 1953 kuhusu Nyerere kushika uongozi wa TAA. Nyerere alipohamishiwa St. Francis College kama mwalimu wa historia, ni Mwapachu ndie aliyemuunganisha na wakina Sykes. Wakati anaunganishwa tayari alishawahi kuwa kiongozi wa TAA ( alikuwa Katibu na baada ya Mwapachu kuondoka Rais wa TAA Tabora) hivyo kusema Abdul Sykes ndiye aliyemleta katika uongozi wa TAA ni uongo.

Kinachosikitisha ni kuwa focus yako katika dini na ukoo wa wakina Sykes unakufanya usiwape umuhimu watu kama Hamza Mwapachu ambae bila shaka mchango wake katika mapambano ya uhuru ulikuwa sawa na wakina Nyerere na Sykes.

Fundi,
Naanza na para ya kwanza.

Kwa utangulizi napenda nikufahamishe kuwa hayo uliyoandika mimi ndiye mtu wa kwanza
kuyaweka hadharani katika kitabu cha Abdul Sykes na ikiwa hukuyasoma kutoka kitabu hicho
utakuwa umeyapata kwa mtu ambaye kayasoma katika kitabu changu.

Hapo unaposema Mwapachu kwa kushirikiana na Abdul Sykes umetaja majina lakini liondoe jina
la Dr. Tsere kwani ilikuwapo TAA Political Subcommittee ambao wajumbe wake walikuwa: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes, Steven Abdallah Mhando na John Rupia.

Mshauri wa hii TAA Political Subcommitee alikuwa Earle Seaton.
Hiyo memorandum unayoieleza iliandikwa na TAA Political Sub Committee kwa msaada mkubwa wa Earle Seaton.

Lakini kulikuwa na Action Group ambayo wahusika wake walikuwa Hamza Mwapachu, Dr. Luciano Tsere na Dr. Kyaruzi.

Kwa ajili hii hii memorandum ilichangiwa na Action Group na TAA Political Subcommittee.

Haya nimeyapata kutoka kwa Nyaraka za Sykes na Mswada wa kitabu, ''The Muhaya Doctor'' mwandishi akiwa Dr.
Kyaruzi.

Ningeweza kusema mengi lakini nachelea jibu hili lisiwe refu sana.

Mswada huu ''Muhaya Dr. upo Maktaba na nilipewa na marehemu Hamza Mwapachu na yeye alipewa na Dr. Kyaruzi.

Hakuna aliyepata kuyajua haya mapaka mimi nilipoyaeleza katika: The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,'' Minerva Press, London 1998.

Para ya pili.

Mazungumzo ya kuibadili TAA kuwa chama cha siasa yalianza mwaka wa 1950 kati ya Hamza Mwapachu na Abdul Sykes na Abdul yeye alimtaka Chief David Kidaha Makwaia aje TAA wampe urais wa TAA kisha waunde TANU.

Mazungumzo ya jambo hili kati ya Abdul Sykes na Chief Kidaha hayakuzaa matunda.

Mwaka wa 1953 miezi ya mwanzo Abdul Sykes akiongozana na Ali Mwinyi Tambwe alikwenda Nansio, Ukerewe
kwa Hamza Mwapachu kutaka fikra zake kuhusu Nyerere kuingizwa katika uongozi wa juu wa TAA katika uchaguzi uliokuwa unakaribia mwezi April.

Abdul Sykes wakati huu alikuwa Act. President na Secretary wa TAA.

Hamza Mwapachu alimwambia Abdul yeye akiachie kiti cha urais wa TAA achukue Nyerere na amsaidie ashinde uchaguzi ule.

Ikiwa haya mimi nimeandika katika kitabu cha Abdul Sykes vipi utasema kuwa sijampa uzito Hamza Mwapachu?

Mimi ndiyo mwandishi wa kwanza kuyaweka haya hadharani na waliposoma watu kishindo kikubwa kilisikika.
Yapo mengi.

Historia hii haikamiliki bila ya kumtaja Schneider Abdillah Plantan na Uchaguzi wa Rais wa TAA kati ya Abdul Sykes na Nyerere Ukumbi wa Arnautoglou tarehe 17 April, 1953.

Hii ndiyo sababu kitabu cha Abdul Sykes kimependwa na wasomaji na kimechapwa mara nne na tunakwenda toleo la tano.

View: https://youtu.be/L7_2cV2GIsM

1785248328078.png
 
Vita ya Maji Maji ilianza tarehe 20 Julai 1905 wakati mwanamke Nantabila Naupunda aliyeongozana na wanaume wawili Ngulumbalyo Mandai na Lindimyo Machali waling'oa miche ya mazao ya pamba kwenye shamba la serikali ya kikoloni lililokuwa katika kijiji cha Nandete. Muarabu mu Omani Seif bin Amri aliyekuwa Akida wa serikali ya kikoloni aliposikia hivyo akatuma watu wake kuwashughulikia. Watu wake wakashindwa kuwatuliza wakina Naupunda hivyo akakimbilia Kitumbi Mwando ambako alijifungia ndani na tarehe 28 Julai aliwaandikia barua mabosi wake kuwaomba msaada kuwa hali imekuwa mbaya. Wamatumbi walipofika nyumbani kwake wakakuta kesha kimbia. Siku hiyo hiyo wamatumbi wakamuua mjerumani mmoja aliyekuwa anaitwa Hopner. Vita ya kwanza kati ya waMatumbi na Wajerumani ilipigwa katika kijiji cha Samanga ambapo wajerumani walishindwa na biashara nyingi za wahindi zilichomwa moto. Mpaka kufika mwezi Agosti wangindo, wapogoro, wakichi na wazaramo walijiunga na wamatumbi.

Ukiangalia utaona kuwa mtu aliyewachomea wakina Naupunda alikuwa muislamu wa kiarabu. Nasema muislamu wa kiarabu kwa sababu bila shaka ndani ya wamatumbi walikuweko waislamu kutokana na historia ya pwani ya Tanganyika. Wamatumbi waislamu walitanguliza umatumbi wao sio uislamu wao katika vita hii. Wao na wenzao walikuwa wanapambana na serikali ya mgeni aliyekuwa anataka kuwadhulumu na kuwanyanyasa katika nchi yao wenyewe. Hawakuwa wanatetea uislamu dhidi ya wakoloni wa kikristu. Hata baadhi ya wakristu nao walijiunga nao. Hivyo hivyo, kama tulivyoona, kuna waislamu walioshirikiana na wakoloni kama ambavyo walikuweko pia wakristu waliokuwa upande wa wakoloni.

Pamoja na hayo wengi walikuwa wamejikita zaidi katika imani zao za asili kuliko uislamu ndio maana ilikuwa rahisi wao kumkubali Kinjeketile. Na katika askari waliotumiwa na wajerumani kuzima walichoona kuwa ni uasi walikuwa askari wa kukodi wakizulu kutoka Afrika ya Kusini. Mmoja wa askari hao wakukodi alikuwa ni Sykes Mbuwane, baba yake Kleist Sykes ambae mama yake alikuwa mnyaturu. Kleist Sykes aliyezaliwa 1894 alijiunga na jeshi la wajerumani wakati wa vita ya kwanza ya dunia. Wajukuu wa askari wa kukodiwa Sykes Mbuwane, Ally, Abdulwahid na Abbas walikuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukoloni wa kiingereza. Katika mapambano hayo walishirikiana na wakristu Dr. Vedastus Kyalakishaija Kyaruzi na Julius Nyerere. Nao hawakupambana kama waislamu bali kama watanganyika.

Kitabu hiki kwa kuangalia vita ya Maji Maji kwa mtazamo wa kidini kinakosa uhalali na kinageuka kuwa propaganda. Hii inasikitisha sababu bila shaka nae ana mengi ya kutufunza juu ya wakati huu muhimu katika historia yetu.

Amandla....

JokaKuu
Fundi...
Sina cha kujifunza katika historia ya Maji Maji kwani tayari nimejifunza na kuandika mengi.
Hebu tuanze na kipande hicho hapo chini:

Vita vya Maji Maji vilipoanza kusini ya Tanganyika mwaka 1905 kwa nia ya kuwafukuza Wajerumani kutoka Tanganyika, zile sehemu zenye Wakristo wengi zilikataa kujiunga na vita na badala yake wakajiunga na majeshi ya Wajerumani na kupigana bega kwa bega dhidi ya wazalendo. Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumani ulianza katika maeneo yenye Waislam wengi na vita vikachukua sura ya vita vya Kiislamu dhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo. Kwa kuwa wamishonari walikuwa washirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituo vyao vinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji. Kutokana mashambulizi haya, Wakristo walivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. Harakati za Maji Maji zilishindwa na Wajerumani walifanya fisadi kubwa dhidi ya wananchi na viongozi wao. Jambo hili liliacha kovu kubwa katika fikra za wananchi na kwa upande wa Wakristo ambao walinusurika na ghadhabu ya Wajerumani, wengi wao wakajiweka mbali na aina yoyote ya kupinga ukoloni.​
​
003_3.JPG
Selemani Mamba Shujaa wa Vita vya Maji Maji Aliyenyongwa
na Wajerumani. Selemani Mamba alikuwa Kiongozi wa Wamwera.
Viongozi Wengine Walionyongwa walikuwa Kinjikitile Ngwale Kiongozi
wa Wamatumbi, Abdallah Chiami Kiongozi wa Wangindo, Mataka Ambuje
Kiongozi wa Wayao na Songea Rauf Mbano Kiongozi wa Wangoni
​
(TANU Ilivyovunja Ngome ya Kanisa Katoliki Jimbo la Kusini, 1955 Sehemu ya Kwanza)

Selemani Mamba naye alimuua Askofu wa Kijerumani Kassian Spiss Mikukuyumbu, Liwale, Lindi.

Haya uliyoandika ya askari wa kukodi yaani mamluki kutoka Afrika Kusini - Chief Mohosh Shangaan na Sykes Mbuwane hawa walitokea Imhambane, Mozambique kijiji kinachoitwa kwa Likunyi na waliletwa German Ostafrika na Hermann von Wissman.

Haya uliyoandika yametoka kwangu yamo katika kitabu cha Abdul Sykes na mimi nimeyapata kutoka kumbukumbu za Sykes na zipo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam toka mwaka wa 1968.

Sykes Mbuwane hakupigana Maji Maji yeye alipigana na Bushiri bin Salim kisha Mkwawa na walipokuwa wakitoka Kalenga baada ya kumshinda Sykes Mbuwane akafa maji Mto Ruaha.

Askari wa Kizulu walipigana Maji Maji na hawa nimewajua kwa kuyasoma majina yao katika Nyaraka za Sykes ni pamoja na Chief Mohosh Shangaan (Afande Plantan), Chakullan na Machakaomo.

Hii ndiyo tofauti yangu kubwa na nyie.
Mimi nilifunguliwa Nyaraka za Sykes na nikasoma mafaili yote.

Sikuandika kwa kubahatisha.
 
Huyu Mzee dishi limeyumba
Na linaendelea kuyumba kweli,
Mwanzo ilikua story zake tunasoma safi tu humu.
Alivyoanza,uislamu lololoolo,sykes hivi,Nyerere blah blah
Kakaa magomeni,mara gerezani,mara upanga.
Hapo ataruka kwenye misikiti,sijui shehe nani yaani dk ya mwisho utajua mzee mwehu huyu.
 
Mohamed Said
Naomba jibu tafadhali
Kinyungu,
Swali lako halijakaa sawasawa.
Katika majemadari 66/67 walionyongwa na kuzikwa katika kaburi la halaiki robo tatu walikuwa Waislam na ndiyo hawa waliobatizwa na Padri Yohannes Haffligger.

Swali lako linatakiwa liwe hawa makamanda Waislam pamoja na Nduna Abdulrauf Songea Mbano waliingia lini Uislam.

Haliladhalika Chief Hamin Massaninga ambae Nduna Abdulrauf Songea Mbano alimwandikia barua ya kutaka atume jeshi kwake waliingia lini Uislamu?
 
Back
Top Bottom