Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) ambayo inafanyika leo Mei 3, 2022 Jijini Arusha.
Kabla ya Rais Samia kuanza kuzungumza, mijadala imeendelea ukumbini:
DKT. RIOBA: MAMLAKA ZINAPATA UGUMU KUZUIA NGUVU YA DIGITALI
Kupitia maendeleo ya teknolojia kuna vipaji vingi vimeonekana kupitia vyombo vya habari huku Serikali na taasisi zake zikipata wakati mgumu kudhibiti kila kitu kinachotoka mitandaoni.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba ambaye ameongeza kuwa licha ya nguvu ya mamlaka nyingi lakini ulimwengu wa digitali hasa mitandao ya kijamii umeleta mambo mengi na imekuwa ngumu kudhibiti kila kitu.
“Kuna watu wengi mmoja mmoja wametumia mitandao kujiendeleza na wamepata faida. Nilikuwa nazungumza na ndugu yangu Max ambaye naye aliniambia jinsi ambavyo kumekuwa na mabadiliko makubwa ya digitali katika Jamii Forums,” Rioba.
DKT. RIOBA: UHURU WA DIGITALI UMELETA MADHARA MENGI
Pamoja na maendeleo ya uhuru wa kujielezea kupitia digitali upande mwingine kuna madhara ambayo yameongezeka kutokana na maendeleo ya teknolojia.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba anasema:
“Tamaduni nyingi zimeuliwa, umoja wa taifa upo hatarini, usalama wa taifa kuwa hatarini kutokana na wale wanaotaka kupinga mamlaka, makundi ya kigaidi yanatumia mitandao kupanga mambo ya na kufundisha wengine ugaidi kwa njia ya kidigitali na kuongezeka kwa habari za uwongo.”
SALOME KITOMARI (MWENYEKITI, MISA-Tanzania)
Licha ya mafanikio katika Sekta ya Habari, bado kuna changamoto kadhaa zinazohitaji kutatuliwa
Miongoni mwao ni ushindani usio sawa, hali duni ya wanahabari na kuongezeka kutumia watu maarufu kama watangazaji
CHURCHILL OTIENO (EAES):
Bado tuna waandishi ambao wanapata msongo wa mawazo kutokana na kazi wanazofanya
Tuna Wanahabari walio chini ya ulinzi Nchini Rwanda, Ethiopia, Eritrea na DR Congo
Vilevile, vitisho dhidi ya wanahabari vinazidi kuchukua sura mpya
RAIS SAMIA AWASILI
Rais Samia ameshawasili eneo la tukio katika Ukumbi wa Hoteli ya Gran Melia Hotel Jijini Arusha na ameanza kwa kutembelea mabanda mbalimbali.
Shughuli inaanza rasmi, baadhi ya viongozi na wageni waalikwa wanazungumza
Dkt. Jim Yonazi (Katibu Mkuu Wizara ya Habari)
Maadhimisho ya World Press Freedom Day 2022 duniani yanafanyika Nchini Uruguay
Kwa Bara la Afrika, na kwa mara ya kwanza, Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari inaadhimishwa Jijini Arusha hapa Nchini kwetu
Wynne Musabayana (AU)
Umoja wa Afrika unachukua fursa hii kupongeza Vyombo vya Habari kwa kuitangaza Afrika hata katika wakati mgumu wa Janga la COVID-19
Vyombo vya Habari vina nafasi muhimu na ya kipekee katika kuhakikisha Waafrika wanapata taarifa za kimaendeleo
Tunawashukuru wanahabari kwa kazi ambayo wanaendelea kufanya, hasa katika wakati mgumu sana wa janga la Covid.
Tutaendelea kuwa marafiki wao na kurahisisha kazi zao.
Tulibainisha kwa dhati sana kwamba ni muhimu kwetu kama Waafrika kuchukua jukumu la kueleza simulizi zetu.
Zlatan Millisic: Mratibu Mkazi wa Shughuli za UN
Mwaka huu kaulimbiu ni "Uandishi wa Habari na Changamoto na Kidijiti"
Kaulimbiu hii inakutumbisha namna mbalimbali ambazo uandishi wa upo hatarini kupitia dijitali
Anders Sjöberg (Balozi wa Sweden-TZ)
Wanahabari mara nyingi wanaweza kujikuta katika mazingira hatari yanayoweza kugharimu maisha yao
Tunatoa heshima kwa Wanahabari ambao wamelipa gharama kubwa kwasababu ya kufanya kazi zao