Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Leo naambiwa ni siku ya mwanamke , wanaume hatumo lakini tutawashabikia.
Kuna wanawake wengi wamefanya mengi ya kuigwa, lakini mimi namweka kwenye kiti mama Samia Suluhu.
Toka tarehe 17 March 2021 hadi leo upepo wa nchi umebadilika kabisa:
- Hali ya kuogopa maisha yako kupotea kwa kusema lolote imeisha
- Watu wasiojulikana wamerudi maskani kwao
- Utekaji wa aina ya Roma Mkatoliki na Mo umepotea
- TRA siku hizi wana adabu na heshima wapodai kodi
- Kubambikizwa kesi kumepungua sana, kama si kuisha
- Zile amri za wakuu wa mikoa, mawaziri, wakuu wa wilaya kuweka watu ndani zimekoma
- ndugu zetu wa CHADEMA hadi mwenyekiti wake kulala lupango kila baada ya mwezi zimeisha
- Lema na Lissu wamerudi na hawajabugudhiwa
- Mbowe kaenda mara kadhaa kunywa chai Ikulu
- Shilingi ya Tanzania haijashuka thamani
- Watalii wamefurika, na kuja na dola zao
- Ujambazi wa serikali kupora fedha toka kwa wananchi(wafanyabiashara) umeisha-tunakumbuka kuporwa Beureu De Change nchini
- Viongozi fulani fulani wanaotumwa kutesa, kuteka, kupora kama Makonda na Sabaya sasa hawapo tena.
Mimi binafsi nampa tano mwanamke na Rais, Samia Suluhu Hassan.
Naomba atakaye pinga atoe na sababu zake, lakini mimi a Samia.
UPDATE
Kikao cha Mama Samia na wanawake wa CHADEMA , siku ya wanawake duniani, kilichofanyika jana 8/3/2923 mjini Moshi, kimetoa fursa ya kuyaona mengi yaliyo moyini mwa Rais.
Hata hivyo hata kwa sisi wana CCM ni mwendo mzuri unsotuhakikishia kuishi kistaarabu na heshima nchini.