Siku yako ya kwanza kuendesha gari ilikuwaje?

miaka hiyo, ile kuirudisha nyuma nikajikuta nimeparamia genge la watu la mboga mboga. Ilikuwa alteza.
Hatutofautiani..niko maeneo ya hapo New Afrika,sasa nataka kuondoka kuna mwamba kapachika gari mbele yangu kama mita moja...nyuma kuna vile vizuizi vina minyororo...nilirudi nyuma nikaviswaga vyuma kama vinne na minyororo yake..nikaingia barabarani bila kuangalia..hakukua na gari,nikakanyaga mafuta mbele kwa mbele..
 
Ufahamu wako wote ulikua sahihi....tatizo ni clutch ilikuwa hujaikanyaga vizuri.... vile vile bora ungekanyaga break tu gari lizime.
 
Sikupata shida sana tena nlianzia makumbusho to tegeta peke yangu ila nilikuwa napga break za ghafla yan gafla gafla tu halafu nikawa natokea ile njia ya mliman city nikala uturn pale mwenge mataa nikarudi ile njia ya kuelekea sinza. Nahisi watu walihisi huyu vipi.
Kusema ukweli kuna umuhimu wa kutotoa leseni kwa mtu ambaye hajapitia driving maana hata sikujua pale hurusiwi kupiga u turn, sikuwa naelewa hata ile mistari ya barabara ina maana gani kasoro zebra tu.
Yaani experience niliipatia road sasa imagine kama ningekuwa wa kuua ningeua watu wangapi
 
Tungekufunga
 
Nakumbuka siku najifunza kuendesha pikipiki aiseeee nilikata tamaa kwamba sitoweza.

Ile kubalance crutch, mafuta na gia ndio ugumu ulipo.

Kuna siku nilikuwa nawasha pikipiki na kuzima halafu siku inapita.

Sa hivi naendesha vizuri tu halafu naona ni rahisi sana.
 
2012...Nilivunja saitimila ya kushoto wakati naitopa parking,mzee aligomba sana si unajua gari za kiinua mgongo...

baada ya week alikuja fundi kuirekebisha hapo nikafundishwa kuendesha rasmi..
 
Katika kitu najua kuendesha ni pikipiki lakini kamwe nilijiapiza siendeshi pikipiki dar hata mara moja. Nikiwa mkoani huko naendesha ila kwa dar sijawahi. Yani vile wanavyokatiza katikati ya magari na kuchomekea mimi nahisi ntajikuta chini kwenye matairi.
Kuendeshwa pia, ila kuendesha no
 
Ongera mkuu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Unafurahisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…