Siku yako ya kwanza kuendesha gari ilikuwaje?

Siku yako ya kwanza kuendesha gari ilikuwaje?

Katika kitu najua kuendesha ni pikipiki lakini kamwe nilijiapiza siendeshi pikipiki dar hata mara moja. Nikiwa mkoani huko naendesha ila kwa dar sijawahi. Yani vile wanavyokatiza katikati ya magari na kuchomekea mimi nahisi ntajikuta chini kwenye matairi.
Kuendeshwa pia, ila kuendesha no
Kuna jamaa yangu alikuwa dar akapata vihela hela vingi tu,nikashangaa mbona hanunui hata pikpik maana kwa huku mikoani huwa tunaanza na pikpik baadae gari lakin jamaa aliniambia pikpik hawez endesha kwenye jiji la dar maana kufa ni nje nje au kuvunjika viungo

Alijichanga changa baadae akachukua baby walker
 
[emoji1787][emoji28][emoji1783][emoji3064][emoji2]
Mwaka 2017 nilipata kagari kangu used aisee siku hiyo madalali wakaniendeshea mpaka home kesho ikabdi nitafute mtu nimlipe anifundishe maana enzi hizo kufundishwa shule niliambiwa laki na nusu... nikampa jamaa 20 yani tukatafuta uwanja masaa matano nazunguka tu nijue kubalance mafuta na brake. Picha linaanza tunarudi home aisee ilikuwa full kupiga mabrake ya kushtukizaa mpaka naenda mbele kwenye kona moja nusu niwavae bodabodaa.. Kichekesho nimefika home jamaa alishukia njiani nimepark vizuri ilaa funguo inagoma kutoka aisee jasho kama loteee 😀 😀 😀 mamaee piga simu kwa madalali wamenitapeli gari bovu nikashuka nikatuliza akili kwanza baadae narudi kwenye gari naangalia GIA IPO KWENYE D.. haya mambo acha tu week nzima naamka naenda kupanda daladala. Weekend moja nikaingia nalo road toka goba mpaka kkoo huko njiani ni jasho kwa kwenda mbelee hata AC sikuwasha maana madirisha niliacha wazi. Nikafanya hivyo mara 3 bhasi ndo nikawa nimejua gari rasmi bila kupata ajali ila kuna siku niligongesha kwenye msingi wa nyumba flani rohoo iliumaa snaa.
 
Acha hiyo sasa wiki moja baada ya kutoka veta nikajidai teyari nimeshakuwa dereva kwani nilishapata leseni yangu ya mchongo, bwana nikaitwa kwenye interview moja kulikuwa na gari mpya tupu.

Na hata kwenye hiyo interview tulitestiwa na gari mpya... mimi nimeshazoea migari mibovu ile ya veta ukiendesha jinsi tairi linavyozunguka unalisikilizia kwenye stering mikono.... na clutch pia nimezoea zile ambazo nilazima uilazimishe kuikanyaga utumie kanguvu kidogo....kumbe bwana nilikuwa mshamba kuna clutch nyingine haziitaji nguvu kukanya...yani ukigusisha mguu tu imo...ni kama vile umekanyaga sponch la godoro...kwenye ile interview niliaibika sana...

Nimefika kwenye gari nimekutana na kiyoyozi kikali ambacho sikuwahi kuzania kuwa kwenye gari panaweza kuwa na kiyoyozi kama hicho, ile gari haikuwa na muungurumo hata kidogo, gari ilikuwa imewashwa ila kutokana na kuwa nilikuwa mshamba wa magari nilivyoingia nikafanya kitendo tena cha kuiwasha...doh nikaumbuka mbona tena gari haiwaki...hali ya kuwa gari ipo on...ila haina muungurumo hata kidogo....kijasho kikaanza kunitoka....nikaamua kukanyaga clutch kisha nikaweka gia na 1. baadae nikakanyaga na mafuta. clutch ilikuwa nyepesi kama sponchi kilicho tokea niliondoka kwa mwendo kama wanaoondokaga nao wanaoendesha magari ya mashinda....yule jamaa alie kuwa ananifanyia test akatingisha kichwa...nikajua hapa nimesha boronga....akaniambia simama...hata kwenye break napo hali ikawa ile ile....nilikanyaga break kwa nguvu gari ikaslip...hadi abiria wengine wakajibamiza na interview ikaishia hapo.​
Nimecheka [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Kuna jamaa yangu alikuwa dar akapata vihela hela vingi tu,nikashangaa mbona hanunui hata pikpik maana kwa huku mikoani huwa tunaanza na pikpik baadae gari lakin jamaa aliniambia pikpik hawez endesha kwenye jiji la dar maana kufa ni nje nje au kuvunjika viungo

Alijichanga changa baadae akachukua baby walker
Kwakweli baby walker kwa dar ni bora zaidi. Pikipiki ni hatari sana halafu ukichanganya na jua la dar walau baby walker ina a.c
 
[emoji23][emoji23]jana nikajitutumua nikaenda na gar kanisani si mnajua vurugu za magari wakati wakutoka nikasema hapa nisubili wote watoke na mm nitoke sasa nimekaa sielewi nikapigiwa simu na mshikaji kuwa mchongo umetiki chap nikakanyaga mafuta nikaaza kuleta ubabe wakupita kwa lazima nimefosi sana mpaka jasho limenitoka nikaona ujinga ngoja nitulie oni zikaaza kupigwa sijui chakufanya nikaaza kufosi tena nusu nichubuee rangi ya gari la watu V8 khaa yule bro wa v8 akanipisha ndio ikawa pona pona yangu ila now niko good kiasi chake
 
Back
Top Bottom