Mara yangu ya kwanza kuendesha gari niligonga...ile gari ilikuwa eicher tani 10....niliikuta imepaki dereva ni rafiki yangu funguo aliziacha...sasa nikajidai fundi nikaingia kwenye ile gari nikiwa na principle zangu kichwa za kuhadithiana.
Sasa nikawa nimekanyaga clutch lakini bahati haikuwa yangu kwani ile gari clutch yake ilikuwa ngumu sana hivyo mimi bila kujua nikajua kuwa teyari nimeshaikanya kumbe nilitakiwa kuikanyaga ile clutch hadi mwisho....
Baada ya kujiona nimeikanyaga ile clucth kumbe nimeikanyaga nusu, nikawasha gari, ikawaka huku inatembea, sasa jasho likaanza kunitoka kwani kwa hadithi nilizowahi kusimuliwa ni kuwa ukikanyaga clutch halafu unawasha gari kisha unaweka gia then unakanyaga mafuta na kuachia clutch kidogo kidogo, pale hali ilikuwa tofauti gari ilianza kutembea kuelekea mbele pale palikuwa na kijitelemshi kidogo na gari ilikuwa na mzigo.
Mbele kama mita 5 hivi palikuwa na eicher nyingine zile ndogo za tani 3.5...nikawa nahangaika kuweka free gari ili nikanyage break jamani ushamba huu acheni tuu {priciple yangu kichwani ilikuwa ni ili nikanyage break lazima gari iwe free....} kumbe hiyo principle ilikuwa ya uongo.. hatimae nikaibamiza hiyo eicha uso kwa uso.
Namshukuru Mungu sikufa na wala sikuvunja zile windmirrow sijui kama ningeweza kulipa kwa uharibifu nilio ufanya siku ile ilinitoka 600k...kesho yake nikaamua kwenda Veta Tanga kusomea udereva rasmi...