Dr am 4 real PhD
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 20,877
- 43,633
Nimecheka kama mtoto mdogo....pole sana nduguAcha hiyo sasa wiki moja baada ya kutoka veta nikajidai teyari nimeshakuwa dereva kwani nilishapata leseni yangu ya mchongo, bwana nikaitwa kwenye interview moja kulikuwa na gari mpya tupu.
Na hata kwenye hiyo interview tulitestiwa na gari mpya... mimi nimeshazoea migari mibovu ile ya veta ukiendesha jinsi tairi linavyozunguka unalisikilizia kwenye stering mikono.... na clutch pia nimezoea zile ambazo nilazima uilazimishe kuikanyaga utumie kanguvu kidogo....kumbe bwana nilikuwa mshamba kuna clutch nyingine haziitaji nguvu kukanya...yani ukigusisha mguu tu imo...ni kama vile umekanyaga sponch la godoro...kwenye ile interview niliaibika sana...
Nimefika kwenye gari nimekutana na kiyoyozi kikali ambacho sikuwahi kuzania kuwa kwenye gari panaweza kuwa na kiyoyozi kama hicho, ile gari haikuwa na muungurumo hata kidogo, gari ilikuwa imewashwa ila kutokana na kuwa nilikuwa mshamba wa magari nilivyoingia nikafanya kitendo tena cha kuiwasha...doh nikaumbuka mbona tena gari haiwaki...hali ya kuwa gari ipo on...ila haina muungurumo hata kidogo....kijasho kikaanza kunitoka....nikaamua kukanyaga clutch kisha nikaweka gia na 1. baadae nikakanyaga na mafuta. clutch ilikuwa nyepesi kama sponchi kilicho tokea niliondoka kwa mwendo kama wanaoondokaga nao wanaoendesha magari ya mashinda....yule jamaa alie kuwa ananifanyia test akatingisha kichwa...nikajua hapa nimesha boronga....akaniambia simama...hata kwenye break napo hali ikawa ile ile....nilikanyaga break kwa nguvu gari ikaslip...hadi abiria wengine wakajibamiza na interview ikaishia hapo.
😂😂😂😂