Siku zinavyozidi kuyoyoma ndio kauli ya Manara inapoonesha uhalisia, dogo Farhanjr amchana chana vibaya

Siku zinavyozidi kuyoyoma ndio kauli ya Manara inapoonesha uhalisia, dogo Farhanjr amchana chana vibaya

Yote haya yanakuja baada ya yanga kuonekana kufuzu nusu fainali?, Basi Simba endelee kuumia na kukusanya taarifa zote Ila yanga tutakapocheza nusu fainali ama fainali na nyie muwe na chakusema.
 
Kumbe na nalo lilikuwa kombe la looser mnalo kejeli sazi! Puuzi kabisa wahedd
CAF Cup ndio shindano ambalo lilikuwa na hadhi ya Shirikisho, na hili lilikuwa linashirikisha timu zile ambazo zilishindwa ku qualify vigezo vya kushiriki African Cup of Champions Club ambayo ndio Club Bingwa ya sasa.
 
Kumbe na nalo lilikuwa kombe la looser mnalo kejeli sazi! Puuzi kabisa wahedd
Anayekejeli nani?

Au ndio kusema umesahau?
 
Hii mada nilishawahi kuitolea ufafanuzi wa kina ila kuna watu kwa kuwa ukweli hauendani na wanachotaka watu waamini basi wanaendelea kupindisha. Yanga alishiriki hiyo CAF Cup mara mbili na mara zote alitolewa hatua ya kwanza, hilo hakuna anayesema.

Nadhani kitengo cha habari cha TFF kitoke usingizini kiwe kinatoa ufafanuzi kwenye mijadala hii ili kuepusha upotoshaji. Hizi taasisi za umma zinalala sana.
Kile ni kitengo cha wapiga deal tu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Kuna uzi niliorodhesha timu zote za Tanzania zilizowahi kushiriki kwa miaka 10 ya hiyo CAF CUP na timu zote hizo zilikuwa zilizoshika nafasi ya pili katika ligi. Hizi taarifa zipo kwenye mtandao wa CAF wenyewe, hatupo karne ya 15 kwamba unaweza kupotosha tu na watu wakakuamini.

Kuna watu kwa kuwa wana sauti katika jamii wanadhani wanaweza kuongea lolote wanalojisikia.
Kikubwa ni kwamba hadi sasa ukweli umedhihiri kwamba Simba ashacheza final ya hiki kinachoitwa Confederation Cup

Mada ishaeleweka Manara ni mjinga na mwongo tu yule

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Mtu wa mpira hawezi kumfanya manara Kama reference asee!!, Manara anaishi kwakutumia mdomo.
Lakini Yanga kama taasisi ya mpira ndio iliyomuajiri

Na hata baada ya kufungiwa, Club ilijitokeza kumkingia kifua kuwa haikubaliani na maamuzi ya TFF na iko pamoja naye kwenda kufata haki kwenye vyombo vingine vya sheria
 
Nilijua tu yanga akitinga nusu lazima vyura waongee yote.
Uzur hata Simba ana nafas ya kutinga nusu fainal club bingwa.

Kuzima hizi kelele wanaume wa Simba kakazeni Tako huko uarabun .
Tukiwatoa wydad hawa vyura hawatakua na chakusema hata km watatinga nusu fainal.
Coz ukwel wanaujua mlima wa club bingwa na shirikisho ni vitu viwil tofaut.
Kama na wao wanajiona wanaweza basi wafike robo club bingwa km ilivyo Kwa Simba alafu ndio waje watambe hapa.
Vipi yanga ingekua club bingwa na ikashinda away si wangekunya mji mzima.
Kipimo Cha yanga ya Sasa sio shirikisho Bali ni club bingwa huko ndio Kuna wanaume wa shoka ,ukitoboa huko unaona kabisa umeoiga kazi .
Fikiria umezungukwa na wydad ,mamelod ,ahly ,esperance, hicho ndio kipimo ila sio hao river ,sijui marumo,na takataka zingine .
kichwa chako kisicho na akili ni mzigo kwa shingo
 
Sababu ya kusema hivyo ni ipi?
Toa sababu, mimi nimetoa ufafanuzi kwanini African Cup Winners’ Cup ndio ilikuwa na hadhi ya shirikisho. Shirikisho ni kwa vilabu vilivyoshinda kombe la shirikisho la nchini mwao na ndio sawa sawa na ilivyo sasa. African Cup Winners’ Cup ndio mashindano yaliyokutanisha mabingwa wa mashirikisho kwa kipindi hicho.
Tusaidie mashindano yote matatu washiriki wake walikuwa ni akina nani kwa vigezo vipi na waliishia wapi kwa pamoja?

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Tusaidie mashindano yote matatu washiriki wake walikuwa ni akina nani kwa vigezo vipi na waliishia wapi kwa pamoja?

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Sawa

Shindano la kwanza lilikuwa linaitwa Afirican cup of champions club.
Hili ndio kwasasa ni sawa sawa na klabu bingwa kwahivi sasa, na timu zilizotakiwa kushiriki hii michuano ni zile tu zinazobeba ubingwa wa ligi kuu.

2) Africa cup winner's cup

Hili ndio ni sawasawa na kombe la shirikisho kwa hivi sasa, timu ambazo zilizokuwa zinazishiri ni timu ambazo zimetwaa ubingwa wa kombe la FA kwenye mataifa yao. Kama ikitokea aliyebeba kombe la FA ndio huyo aliyebeba na ligi kuu basi aliyecheza nae fainali (runner up) ndio atakayefuzu kucheza hili kombe la African cup winner's cup

3) CAF cup

Haya ni mashindano yaliyoanzishwa na Mnigeria kama kwaajili ya timu zilizoshindwa kufuzu mashindano ya kimataifa ya CAF.
Timu ambazo zinashika nafasi ya pili, na zilizoshindwa kufuzu mashindano ya CAF ( African cup winner's cup na African cup of champions club)
CAF cup ilianzishwa mwaka 1992 na mwaka 2003 ndio ikawa mwisho wa mashindano hayo hivyo yalidumi kwa miaka 12 tu

HITIMISHO

Kwanini African cup winner's cup ndio ni sawasawa na shirikisho kwasasa?
Sababu ya kwanza ni kama nilivyoeleza juu mfumo wake upo sawasawa na ilivyo CAF confederation cup.
Sababu ya pili ni CAF super cup
CAF super cup ni shindano linalohusha mabingwa wa kombe la CAF interclub yaani kombe la shirikisho na kombe la mabingwa.
Katika kipindi hiko kabla ya kuanzishwa kwa CAF confederation cup, CAF super cup ilikuwa inakutanisha bingwa wa African cup of champions club VS bingwa wa African cup winner's cup.

Katika mwaka 1993 bingwa wa African cup winner's cup alikuwa ni Al Ahly na bingwa wa African cup of champions club alikuwa ni Zamalek. Hivyo wakakutana kwenye CAF super cup mwaka 1994 na bingwa akauchukua Zamalek wa CAF super cup.

Huo ndio ukweli wa mambo
IMG_20230426_074839.jpg
 
Source;Wazee wa karikoo kwenye kijiwe cha 'gawaha'
Screenshot_20230426-080317.jpg
 
NAOMBA NIKUKUMBUSHE KITU MY BROTHER HAJI MANARA KUHUSU SIMBA 1993.

Jana nilipata wasaa wa kuitazama clip yako kuhusu fainali ya Simba 1993 dhidi ya Stellah Abdijan.

Umesema nchi za Kiarabu hazikushiriki? Simba alicheza robo na USM El Harrach ya Algeria (Taifa la Kiarabu)

Okay naenda kwa hatua na utasahihisha pale palipokosewa na utaweka vema nilipopatia! 1993 mwaka tajwa hapo CAF alikuwa na michuano mitatu ya klabu ambayo yote ilikuwa chini yake na maelekezo yote yalitoka Mitaa ya 6th of October, Cairo yalipo makao makuu ya CAF.

Mwaka tajwa kulikuwa na michuano ifuatayo! African Cup of Champions Clubs, kulikuwa na CAF Cup na African Cup Winners’ Cup! Michuano yote mitatu ni ya CAF, ambao Champions Clubs ni timu bingwa kila nchi wanachama, ubingwa alibeba Zamalek ikiwa ni taji lake la tatu na linahesabiwa, timu shiriki zilikuwa 45 na zilipigwa mechi 73 karibia.

1993 Winners’ Cup hii ilikuwa michuano ya timu zilizobeba mataji ya FA kwenye nchi husika tu! zilipigwa mechi 72 ambapo bingwa alikuwa ni Al Ahly ya Misri walikipiga na African Sports ya Cameroon bila shaka, ni michuano ambayo ilikuwa chini ya CAF.

Halafu kuna CAF CUP unaweza kuliita Kombe la Shirikisho kwa Kiswahili! CAF ni shirikisho na kombe ndio lao, mechi zilipigwa 64 hapa!Ndio maana ya CAF CUP ya 1993! Hapa fainali alicheza Mfalme wa Nyika SIMBA YA DAR ES SALAAM dhidi ya Stella Adjame ya Ivory Coast, hii ilikuwa inahusisha Washindi wa pili kwa kila ligi kwenye nchi husika pasi na shaka.

Haji unasema Simba hakucheza fainali ya kombe la Shirikisho sasa nini maana ya CAF CUP kwa Kiswahili? Ama tuseme TFF CUP ama Azam Sports Federation Cup si ndio Kombe hili la Shirikisho ambalo Yanga ni bingwa Mtetezi?

Nimeona hoja ya kutajwa kwa Tajiri mkubwa wa Nigeria wakati huo MOSHOOD OLAWALE ABIOLA kuwa ndie aliyeweka mzigo kwa ajili ya michuano hii, je kuna tatizo gani kwa Mdhamini kupatikana na wengine humpa naming rights za michuano? Hii ni kawaida sana in business

Tumesahau kuwa kuna Azam SPORTS FEDERATION CUP (Tajiri Said Salim Bakhresa) tuliwahi kuwa na BARCLAYS PREMIER LEAGUE, CARLING CUP, MTN CUP, NBC PREMIER LEAGUE, zote hizo ni walioweka mzigo wanaweka na majina yao!

I stand to be corrected.View attachment 2599233

Performance in CAF competitions

The highest success that Simba achieved was reaching the final of the CAF Cup in 1993, where they lost to Stella Club of Côte d'Ivoire. It was the highest continental achievement by a Tanzanian team to date. In 2003 Simba beat the then-reigning champions Zamalek of Egypt in the CAF Champions League second round of qualifiers to qualify to the group stages, after having beat Santos of South Africa in the first round.

CAF Champions League: 11 appearances

2002 – First Round

2003 – Group stage (Top 8)

2004 – Preliminary Round

2005 – First Round

2008 – First Round

2011 – Special play-off for Group stage

2013 – Preliminary Round

2018–19 – Quarter-finals

2019–20 – Preliminary Round

2020–21 – Quarter-finals

2021–22 – Second Round

African Cup of Champions Clubs: 9 appearances

1974 – Semi-finals

1976 – Second Round

1977 – Second Round

1978 – Second Round

1979 – Second Round

1980 – Second Round

1981 – First Round

1994 – Quarter-Finals

1995 – Second Round

CAF Confederation Cup: 6 appearances

2007 – Preliminary Round

2010 – Second Round

2011 – Play-off

2012 – Second Round

2018 – First Round

2021–22 – Quarter-finals

CAF Cup: 2 appearances

1993 – Finalist

1997 – First Round

CAF Cup Winners' Cup: 3 appearances

1985 – Second Round

1996 – Second Round

2001 – Second Round

Source: wikipedia
Huyu dogo ni mshabiki wa Simba nini ?...au kaamua tu kuweka mambo sawa ?
 
Sawa

Shindano la kwanza lilikuwa linaitwa Afirican cup of champions club.
Hili ndio kwasasa ni sawa sawa na klabu bingwa kwahivi sasa, na timu zilizotakiwa kushiriki hii michuano ni zile tu zinazobeba ubingwa wa ligi kuu.

2) Africa cup winner's cup

Hili ndio ni sawasawa na kombe la shirikisho kwa hivi sasa, timu ambazo zilizokuwa zinazishiri ni timu ambazo zimetwaa ubingwa wa kombe la FA kwenye mataifa yao. Kama ikitokea aliyebeba kombe la FA ndio huyo aliyebeba na ligi kuu basi aliyecheza nae fainali (runner up) ndio atakayefuzu kucheza hili kombe la African cup winner's cup

3) CAF cup

Haya ni mashindano yaliyoanzishwa na Mnigeria kama kwaajili ya timu zilizoshindwa kufuzu mashindano ya kimataifa ya CAF.
Timu ambazo zinashika nafasi ya pili, na zilizoshindwa kufuzu mashindano ya CAF ( African cup winner's cup na African cup of champions club)
CAF cup ilianzishwa mwaka 1992 na mwaka 2003 ndio ikawa mwisho wa mashindano hayo hivyo yalidumi kwa miaka 12 tu

HITIMISHO

Kwanini African cup winner's cup ndio ni sawasawa na shirikisho kwasasa?
Sababu ya kwanza ni kama nilivyoeleza juu mfumo wake upo sawasawa na ilivyo CAF confederation cup.
Sababu ya pili ni CAF super cup
CAF super cup ni shindano linalohusha mabingwa wa kombe la CAF interclub yaani kombe la shirikisho na kombe la mabingwa.
Katika kipindi hiko kabla ya kuanzishwa kwa CAF confederation cup, CAF super cup ilikuwa inakutanisha bingwa wa African cup of champions club VS bingwa wa African cup winner's cup.

Katika mwaka 1993 bingwa wa African cup winner's cup alikuwa ni Al Ahly na bingwa wa African cup of champions club alikuwa ni Zamalek. Hivyo wakakutana kwenye CAF super cup mwaka 1994 na bingwa akauchukua Zamalek wa CAF super cup.

Huo ndio ukweli wa mambo
View attachment 2599934
Uzi ufungwe sasa. Safi sana mkuu
 
Mtu wa mpira hawezi kumfanya manara Kama reference asee!!, Manara anaishi kwakutumia mdomo.
Kwahiyo yanga sio watu wa mpira ????maana ndio wanaomwamini........
 
Uzi ufungwe sasa. Safi sana mkuu
Ufungwe kwa hizo porojo????[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kwahiyo mashindano kama ya Azam Sports Federation ni ya Bakhresa?
Kagame cup?NBC PL ya benki,VPL ya kampuni ya simu, huu ni upunguani wa mashabiki wa utopolo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yanga akibeba kombe je?
Anabeba mbele ya Nan?
Angalia uzito wa club anazokutana Nazo.
Yanga huu msimu ni km Wana Bahat sana ingawa nao Wana ubora mzuri sana .
Ila club alizokutana Nazo Sion km ni kipimo tosha kwake.
Timu yenye uafadhar huko shirikisho Kwa msimu huu ni pyramid pekee ,na hao ndio kipimo Cha yanga.
All in all akibeba ni mafanikio mazur sana kwake ila sio kutamba kwamba mpinzan wake asingeweza Fanya anayoyafanya ,hapa ni Bahat tu imemuangukia Hana wapinzan wenye nguvu kiivo.
Shirikisho ya msimu huu na ya misimu iliyopita Kuna utofaut mkubwa sana.
Kwa akili Yako kwenye hizo timu za shirikisho za msimu huu unaiona ni timu gan ingemzuia Simba kufika fainal?
Sasa why Yanga ashindwe?
Simba na Yanga Zina ubora unaokaribiana Kwa Kila kitu ingawa yanga Ina kikosi kipana kuliko Cha Simba ila ubora wako sawa tu.
 
Back
Top Bottom