Allah anasema katika qur an kumuambia Ibilis (shetani) ukisoma katik suura al hijjir aya ya 42
إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ﴿٤٢﴾
42. Hakika Waja Wangu huna mamlaka nao isipokuwa ambaye atakufuata miongoni mwa waliopotoka.
وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٤٣﴾
43. Na hakika Jahannam ni miadi yao wote pamoja.
Akasema tena katika suurat al insaan aya ya 3
إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا﴿٣﴾
3. Hakika Sisi Tumemuongoza njia; ima (awe) ni mwenye kushukuru(kumuamini allah) au mwingi wa kukufuru.
[1]
Njia ya haqi imebainishwa kwahy kazi kwako kuchagua (mwanzo wa sura allah amekumbusha kuwa zimepita zama huko nyuma mwanadam hakuna kitu chenye kutajwa kwa maana hakuwepo je kama huko nyuma hukuwepo unadhani asili yako ni nini? Na kwanin ulizaliwa kutokana na mume na mke hukuota kama mti? Kwanin unakufa?
rejea kwa mola wako ndugu mbora na utubie kabla hakijakukuta kifo chako na kama unaweza kuzuia kifo basi endelea kutakabbar.