Sikubaliani hata kidogo na utovu wa nidhani wa Bernard Morrison, lakini kuna hoja za msingi ni lazima zijibiwe na TFF.

Sikubaliani hata kidogo na utovu wa nidhani wa Bernard Morrison, lakini kuna hoja za msingi ni lazima zijibiwe na TFF.

Wamemfungia asicheze mechi ya Simba hao ingeakua inafika mechi 4 wangefikisha 4...Inonga ile rafu aliyomfanyia Sure Boy amepata adhabu gani mbona rafu zipo nyingi sana na hatuonj wakikaa kujadili au wao wapo busy na BM tuu...

Kwani katika hiyo mechi Iko ga hakupewa kadi? Unataka aadhibiwe mara mbili? Kama Morison angepewa kadi hta ya manjano kwa lile tukio leo bodi isinge muadhibu maana mchezaji hatakiwi kuadhibiwa mara mbili na vyombo viwili tofauti.

Wa kulaumiwa hapo ni mwamuzi ambae alimezea lile tukio. Ya Inonga pia anaepaswa kulaumiwa ni mwamuzi kwa kumpa kadi ya njano badala ya nyekundu.
 
Ya Shabani Djuma hivi ni lini ilitolewa uamzi? Au unajifanya kuyaona ya Simba yenu unajitia upofu.
Ndugu hao viande watakumalizia MB bure maana hawajui walisemalo

Yule Bangala aliwahi kuonesha dole waulize sasa alichukuliwa hatua gani

Tatzo ni waongo halafu wasahaulifu.
 
Kwani katika hiyo mechi Iko ga hakupewa kadi? Unataka aadhibiwe mara mbili? Kama Morison angepewa kadi hta ya manjano kwa lile tukio leo bodi isinge muadhibu maana mchezaji hatakiwi kuadhibiwa mara mbili na vyombo viwili tofauti.

Wa kulaumiwa hapo ni mwamuzi ambae alimezea lile tukio. Ya Inonga pia anaepaswa kulaumiwa ni mwamuzi kwa kumpa kadi ya njano badala ya nyekundu.
Vipi kuhusu Pascal Wawa?
 
Hivi wewe unafatilia mpira kweli au unapiga brah brah?

Unakumbuka kule Kigoma mukoko tonombe alifanywa nini?,Mukoko alipewa red kadi na bado hiyo kamati ilimfungia,kama ndivyo kanuni inasema ya kwamba refa akishakupa kadi uwanjani kamati haitokufungia basi tuelezwe kwanini mukoko ingawa alipewa red card ambayo hakutakiwa kucheza mechi tatu kikanuni,kwanini tena kamati ilimfungia na faini juu?

Tunapoyasema haya hatumaanishi kwamba Yanga wanapokosea wasiadhibiwe,bali tunaona kabisa kuna upendeleo,kwanini iwe wachezaji wa Yanga tu waadhibiwe?,Mtenje alipocheza rafu mbaya pale arusha alipewa Yellow card lakini hatukuona kamati ikimuadhibu,Inonga alipocheza rafu mbaya alipewa Yellow Card na hatukuona kamati ikimuadhibu,Lakini mukoko tonombe alipocheza vibaya pale kigoma alipewa red kadi na Adhabu ya kufungiwa mechi kadhaa.

Haya tunayasema kwa manufaa ya mpira,leo mashabiki na viongozi wa Yanga wanalalamika lakini yanamwisho,upepo utabadirika na ipo Siku Simba na viongozi wake wataanza kulia.

Hatuhitaji shirikisho liendeshwe kiupendeleo mpaka mashabiki wenyewe wa Simba wanashangaa namn Yanga wanavyoonewa.

Mchezaji anapocheza rafu aadhibiwe haijalishi ni mchezaji wa timu gani,lakini kusiwe na upendeleo wa kanuni,kwamba kanuni hizo ziwe zinawaminya Yanga tu huku timu nyingine zikiendelea kula kuku.
Unapoteza muda kuelewesha vilaza mkuu
 
Kwani katika hiyo mechi Iko ga hakupewa kadi? Unataka aadhibiwe mara mbili? Kama Morison angepewa kadi hta ya manjano kwa lile tukio leo bodi isinge muadhibu maana mchezaji hatakiwi kuadhibiwa mara mbili na vyombo viwili tofauti.

Wa kulaumiwa hapo ni mwamuzi ambae alimezea lile tukio. Ya Inonga pia anaepaswa kulaumiwa ni mwamuzi kwa kumpa kadi ya njano badala ya nyekundu.
Na dickson job kwanini alipewa nani pia akafungiwa mechi tatu na kamati na faini juu

Wewe ni mavi
 
Jaribu kua mfuatiliaji mzuri wa sheria na kanuni,rafu ya inonga ilishaadhibiwa na muamuzi kwenye mechi husika, kitendo alichofanya Morrison ni kutendo ambacho si cha kiuanamichezo na muamuzi hakukiadhibu kwakua hakukiona hivyo kinapaswa kuadhibiwa kwenye kamati ya maadili.

Kama muamuzi angekiona na kutoa adhabu yake pale pale ya kadi yoyote ile Morrison asingeadhibiwa tena!!!
Mukoko aliadhibiwa ndani ya dk 90 kule kigoma baada kumpiga kiwiko boco,na bado kamati ya masaa 72 ikamfungia michezo 3,kitendo alichofanya morrison kilifanywa na wawa alipomkanyaga nchimbi lakini wawa akupewa adhabu yoyote si ya kadi uwanjani au kufungiwa michezo 3
 
Kwani katika hiyo mechi Iko ga hakupewa kadi? Unataka aadhibiwe mara mbili? Kama Morison angepewa kadi hta ya manjano kwa lile tukio leo bodi isinge muadhibu maana mchezaji hatakiwi kuadhibiwa mara mbili na vyombo viwili tofauti.

Wa kulaumiwa hapo ni mwamuzi ambae alimezea lile tukio. Ya Inonga pia anaepaswa kulaumiwa ni mwamuzi kwa kumpa kadi ya njano badala ya nyekundu.
Mukoko alipewa kadi Kigoma na baadae kamati ilimfungia...hapa unabahatisha tuu hawa jamaa tuwaache na maamuzi yao leo watasema hili kesho lile...
 
Hii sidhani kama ni hoja kubwa sana. Kikubwa mchezaji mwenyewe anatakiwa kucheza kwa kujali afya za wachezaji wenzake kama wao wanavyojali afya yake. TFF ina madhaifu yake lakini wachezaji wa Yanga wanapaswa kuishi kwa kulijua hilo na hivyo wawe makini.
 
3ANAANDIKA Mchao Tv

KWA MFANO TU

Mechi ya Azam dhidi ya Yanga ilipigwa Septemba 6, 2022 (zaidi ya wiki mbili zilizopita, ni siku 16 zilizopita) ambapo mchezaji wa Yanga Bernard Morrison alifanya utovu wa nidhamu kwa kumkanyaga Lusajo Mwaikenda wa Azam kwa makusudi.

Kwa mfano Bodi ya Ligi wangekaa na kamati yao ya saa 72 na kutoa maamuzi kungekuwa na ubaya gani???

Na kama maamuzi yangekuwa kama jinsi walivyoamua, maana yake Morrison angeikosa michezo ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Septemba 13, angeukosa pia mchezo dhidi ya Ihefu (ambao ulipangwa kuchezwa Septemba 29 kabla ya kusogezwa mbele) na angeukosa pia mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao unatarajiwa kuchezwa Oktoba 3.

Tuna-assume mchezo kati ya Yanga dhidi ya Ihefu ungeahirishwa kama ilivyo hivi sasa, maana yake ni kwamba Morrison angeikosa michezo ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar (Septemba 13), dhidi ya Ruvu (Oktoba 3) na adhabu yake angeimalizia kwa kuukosa mchezo dhidi ya Namungo ambao kwa mujibu wa ratiba utachezwa Oktoba 13... halafu kwenye Kariakoo Derby dhidi ya Simba (Oktoba 23) mtoto mtukutu angekuwa ndani ya nyumba.

Jana Bodi ya Ligi walitoa taarifa ya kuusogeza mbele mchezo kati ya Yanga na Ihefu (kutoka Septemba 29 hadi Novemba 29, yaan miezi miwili mbele) halafu leo Bodi ya Ligi hao hao wanatoa taarifa za kumfungia Morrison michezo mitatu kutoka sasa ambapo mchezo dhidi ya Simba unakuwa mmojawapo kwa kosa la siku 16 nyuma.

KWA MFANO TU lakini.....Yanga wakihoji uhalali wa adhabu ya BM33 kutoka leo Shirikisho la TFF na Bodi ya Ligi watajitetea kwa lipi??

KWA MFANO TU lakini.....Yanga wakiituhumu TFF kuwa inawahujumu, ni utetezi upi utakaotolewa na wenye mamlaka kupinga hoja hiyo??

KWA MFANO TU.....Yanga ikilalamika kuwa kuna bingwa anaandaliwa na Shirikisho la soka (TFF) kama jinsi Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu alivyowahi kulituhumu Shirikisho, ni nani atakayekuwa na mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu juu ya kauli hiyo.

KWA MFANO TU......yaan ni mfano tu, ni mfano ambao........
Huu ni mwendelezo wa ujinga. Kanuni inasema adhabu ya kukosa michezo mitatu baada ya kutangazwa. Kanuni haijataja michezo gani. Kuuchukulia kuukosa mchezo dhidi ya Simba ni uonevu, huo ni upumbavu
 
Mngeyakemea madudu kama haya wakati wa kamati ya masaa 72 ya Jamal Malinzi tungewaona ni watu mnaopenda haki itendeke .Lakini kwakuwa mlikuwa mnaona ni sawa tu, tena mkawa mnashangilia basi hamna Maana ni vema mkanyamaza tu soka letu liende kivyetuvyetu

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom