Sikubaliani na jinsi Rais Samia anavyofanya Teuzi, na zitakuja kumfanya kujuta baadaye

Status
Not open for further replies.
Bila kupepesa macho na kupindisha maneno

Mimi ni CCM damu damu ambaye nimeanza kuwa Mwana chama wengi wenu hamjazaliwa, tokea Niko Pugu Mwaka 1979 na baadae tukasoma kupewa kadi ya CCM siyo zinazogawiwa Kama njugu...
Tatizo ni mfumo! Over
 
Mimi niko kinyume kidogo na ninyi.

Mimi ninamlaani Mbowe.

Chadema imeaminiwa na Watanzania wengi, ilitosha kumpa sauti kubwa kukemea au hata kuita maandamano lkn badala yake aneungana na watesi wetu.

Upinzani imara huifanya serikali kuwajibika
Siasa za Mbowe ni za kiujanjaujanja tu, yupo kimkakati zaidi kuisaidia Ccm kichinichini.

Yale maigizo ya maridhiano yamemteka.

Bams JokaKuu zitto junior Tindo
 
Duh,
Nchi inatafunwa balaa!
 
Kitu nilichoshindwa kuelewa had leo,Maharage aliteuliwa na January lakini kabadilishwa na Samia....apo kidogo nimekuwa confused.....haya mambo yanayotokea huwezi shangaa kama ulishafanya kazi na boss wako ni Mwanamama na amepata hicho cheo by favour or chance tu na wala sio uwezo wake....kama hana maono hiyo taasisi/kampuni au chochote anachokiongoza kama hajawahiwa lazima kiingie kaburini
 
Siasa za Mbowe ni za kiujanjaujanja tu, yupo kimkakati zaidi kuisaidia Ccm kichinichini.

Yale maigizo ya maridhiano yamemteka.

Bams JokaKuu zitto junior Tindo
Asipoachia uenyekiti cdm itadumaa, amefikia ukomo.

Mikutano yako haisisimui tena japo anatumia chopa.

Lissu hata akitembea kwa miguu ni habari ya mjini
 
Tatizo lipo kwa mteuaji kwani na yeye ni sehemu ya ufisadi unaoendelea kulitafuna taifa letu
 
Duuuuu!
 
1. Alipuuzia kuunda parallel intelligence. Pengine hajui umuhimu wake kwa kuamini kila aliyeko chini yake hana uwezo wa kutenda kinyume na maagizo.

2. Amejiweka kwenye mazingira ambayo mnyetishaji yeyote mwenye jicho la tatu ni ngumu kumfikia unless uwe chawa. Kwa bahati mbaya wanyetishaji wengi sio chawa hivyo basi wanamuacha aamue kadiri aonavyo inafaa yeye na kikundi 'Kilichomsaidia' kurithi madaraka kidemokrasia.
 
Hii Ni mipango ya CCM na Serikali yake ya awamu ya 6 Ni maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi wa Raisi na wabunge 2025.
Serikali lazima iwaweke Watendaji wajanja wajanja ( Makada) na wataambiwa wasisikilize maneno ya kwenye mitandao au wapinzani. Kiongozi Mkuu anajua kila kinachoendelea hapo, na wapinzani nao wameahidiwa ruzuku.Wavuja jasho shauri yao.
-Siku hizi sina uhakika Kama kampuni hewa ya kimagumashi Kama Meremeta au Sukita, ambazo zilitumika miaka ya nyuma kama zipo baada ya CAG wa Zamani kutoa hoja za ukaguzi.
Ushauri
-iundwe Bodi au tume maalum ya wataalam ya kuwafanyia usaili Watendaji wakuu na wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za umma .Last week nimeona Gavana wa Bank Kuu Kenya anafanyiwa interview na kamati maalum ambayo itatoa mapendekezo kwa Rais kwa uteuzi Katika maswali wawe wanaulizwa mali na madeni waliyonayo (Net worth) na vyanzo vya mapato yao.Aidha waombaji wawe wanaulizwa,namna watakavyo tumia muda wao kuhudumu kwenye taasisi ya umma na binafsi.
-suala hili liwekwe kwenye katiba pendekezwa
 
"ukipewa ushauri wa kipumbavu,nawe ukajua niwa kipumbavu na ukaufanyia Kazi basi aliyekupa ushauri huo anakudharau"Mwl.Nyerere
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…