Sikubaliani na pendekezo la Waziri wa Fedha kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa arudishwe kwenye mshahara wake wa awali

Uamuzi wa serikali ya awamu ya sita ya kufuta utaratibu wa kuendelea kupata mshahara wa cheo cha uteuzi hata baada ya kutumbuliwa haufai kabisa kwani yalikuwa ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi kwa kuwa hilo suala lipo kisheria serikali ianze utaratibu wa kuifanyia hiyo sheria marekebisho mara moja ili kuokoa kodi zetu .Sheria ikifanyiw marekebisho itachochea uwajibikaji wa hao wateule kwani wataogopa kupoteza vyeo na vipato tofauti na sasa mtu anapoteza cheo tu ila mkwanja uko pale pale

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
 
Kwani mwanzo ilikuwaje.? Inamaana walikuwa wanakula mshahara ule ule huku wakiwa nje ya cheo walichokuwa nacho.?
 
Hiyo ni sahihi.
 
Watakaokuunga mkono ni wachache saba, Pole mkuu. Bado natafakari hekima ilojificha kwenye practice hii
 
Tatizo ni ufukuzaji au utumbuaji wa mizengwe ambao viongozi wenyewe wanafanya. Kama kiongozi kakosea na kosa ni kubwa kuwa hafai kushika nafasi aliyoteuliwa kuna utaratibu wa namna ya kumwondoa, ambao ni kumwandikia barua kuonesha kosa lake,kumshtaki,kuteua tume ya uchunguzi; lakini si kwa sababu wewe kiongozi mpya humpendi/hutaki sura yake au sababu yo yote ya kipuuzi; kisha unatamka jukwani tu bila barua, atajuaje masharti mapya ya kazi mpya! Viongozi wengi wanatamka mdomoni kuwa wanafuata misingi ya utawala bora wakati vichwani mwao hawana hata chembe ya uelewa wa maana ya utawala bora. Ni tatizo lile lile la ama wastani wa kiwango cha uelewa au kiwango cha elimu ambao hapa Tanzania unateremka kwa kasi katika ngazi zote! wastani!

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Hili pendekezo la Mh.Mwigulu ni muafaka kabisa,serikali haiwezi kuwa shamba la bibi, Hivi sekta binafsi kuna utaratibu huo? mtu alipwe mshahara ule ule ilihali ameshang'olewa kwenye kiti chake? swala la kuonewa afuate taratibu husika,pia uelewe vyeo vya uteuzi unakuwa hapo kwa mapenzi ya aliyekuteuwa,akikung'oa rudi kwenye taaluma yako au nafasi yako uliyokuwepo. Na hii move italeta nidhamu sana na uwajibikaji, maana mtu atajua akiharibu anarudi kwenye deski na wananzengo,au ntolee kabisa.
 
Mzee kama ulitumbuliwa unaenda kurudia mshahara wa awali.
Aliyekuteua si ndio anayekutumbua?
 
Mkuu Koryo2, kwanza msome huyu
Mkuu Johnny Sack , kumbe hili wewe ndio umelijua jana!, karibu angalia tarehe ya bandiko hili uone watu tulisema nini na lini
Nilisema
P.
 
Kwani mwanzo ilikuwaje.? Inamaana walikuwa wanakula mshahara ule ule huku wakiwa nje ya cheo walichokuwa nacho.?
Kwanafasi za uteuzi sina hakika ila huku kwenye taasisi na mashirika eg TANAPA, UD nk ilikuwa ukishushwa cheo mshahara haushuki
 
Hujui unaloongea! Bora kunyamaza
 
Kwahiyo mhasibu wa halmashauri alipwe mshahara wa Mkurugenzi wa jiji kisa tu aliwahi kuwa mkurugenzi wa jiji huku mkuu wa jiji husika analipwa mshahara wake?
Mtu alipwe mshahara wa mahali alipo na si vinginevyo.
Magufuli ndiye aliyeiingiizia serikali hasara na tumbuatumbua zake za kiwendawazimu.
Leo mtu anakuwa RC, kesho yuko home, keshokutwa anakuwa katibu mkuu wa wizara.
Mpaka hazina hawajui wafanye nini, baadaye wanaamua kumlipa mshahara wa U RC bila kujali yuko wapi.
 
Daaaah! Mwigulu ni shetani kabisa. Hii kitu hata JPM hajawahi kuwaza.
 
Utaelewa tuu nyie ndio mlikuwa wazembe na mkitumbuliwa mnasema cheo cha nini ntabaki na salary yangu Sasa hii itakomesha wizi bila kufokeana hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…