Sikubaliani na pendekezo la Waziri wa Fedha kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa arudishwe kwenye mshahara wake wa awali

Huwezi kuwa na nchi ina wakurugenzi 700 na wakati halmashauri zipo 184 tu
Halmashauri zipo 184,na Wakurugenzi ni 184.
Taasisi za umma zipo karibu 210 na kila Taasisi INA wastani wa Wakurugenzi 5-7 hapo kuna Wakurugenzi 1050,na hapo bado kuna Managers
Kuna Wizara takribani 20 piga wastani wa Wakurugenzi 14-20 kwa kila Wizara
 
Mi naongolea halmashauri bibi wewe
 
Kwanza tuulizane kwa nini iliwekwa hivyo?
Jibu ni simple tu hamuwezi kua na uelewa au mtazamo unaofanana miaka yote! Ni lazima kuna kipindi atakuja tokea mtu mwenye uelewa na mtazamo tofauti na wale waliotangulia! It is the Nature that determines what to do!
Walioweka utaratibu huo ni binadamu, hivyo ni rahisi kabisa kwa binadamu mwingine kung'amua mapungufu yaliyopo!
 
Toa reason na mifano ya kueleweka kusapoti hoja yako....
Hiyo ni sahihi kabisa . Kama wewe ulikuwa ni Mwl. kwa mfano baadaye ukateuliwa kuwa DED na ukawa unapokea mshahara wa DED siku unapoacha nafasi ya DED kwa sababu yoyote ile na muda wako wa kustaafu bado haujaisha unatakiwa kurudi kupokea mshaahra wako wa zamani. yaani haina maana nchi inayo wakurugenzi 268 lakini watumishi wanaolipwa mishahara ya wakurugenzi wawe ni 350, it is very unfair. itasaidia sana kupunguza matumizi mabaya ya fedha za serikali. na vile vile kwa wakuu wa idara kwenye local Government. huko ndio wako wengi, mtu uateuliwa baada ya miezi 3 unarudi kwenye kazi yako ya zamani na kitita cha mkuu wa idara. Fedha hizi zingetumika kuboresha maslahi ya watumishi wote kwa ujumla wake.
 
Sijui unaona je unapoambiwa tuna Halmashauri 184 hivi lakini kuna maafisa masuuli zaidi ya 300 wako kwenye pay rol l,kuna nafasi za kazi kibao kwenye loca government haziajiriki kutoka a na ufinyu wa wa bajeti.kumbuka mshahara mmoja wa mkurugenzi ni almost sh 5,000,000/=na graduate analipwa sh700,000\=Ina maana mshahara mmoja wa afisa masuhuli unatosha kulipa graduate 7.sema(300-184)=116x7=812 ,hebo safi saana.
 
Vipi mkuu, na wewe ni miongoni mwao katika waliotumbuliwa?
Huo utetezi wa kutaka mtu alipwe kwa kazi asiyoifanya una mantiki gani? Yaani mtu alikuwa ofisa elimu, akateuliwa kuwa mkurugenzi, kisha ukurugenzi ukamshinda akatumbuliwa, unataka alipwe mshahara wa ukurugenzi kwa lipi? Kila mtu anastahili malipo halali na stahiki kwa kazi aifanyayo, siyo ufanye kazi ya ualimu ulipwe mshahara wa ukurugenzi, huo ni ubadhirifu.
 
Wewe boya kweli, yaani uteuzi umetenguliwa halafu eti uendelee kulipwa mzigo ule ule wa awali!! Hapo Waziri yuko sawa kabisa
 
Hoja dhaifu, nyepesi na isiyo na nguvu wala ushawishi.
 
Kwani taratibu za utumidhi sirikarini zinasemaje? Au ni kola waziri na yake?
 
Hapa ndio tunapokosea!! Na kama hii ndio tabi iliyoendelea miaka yote - ni moja ya sababu kwanini kama nchi hatutapata kuendelea!

Kutenguliwa ni kuondolewa kwenye mamlaka au kazi husika. Ninkufukuzwa kazi!! Ili kuepuka matumizi mabaya ya fedha:
a) Tunatakiwa kurekebisha sheria za kazi ili mtu anapotenguliwa anakuwa hana kazi tena. Haki zake zitimizwe alipwe chake na aende. Jambo hili litasaidia kufanya watu waogope kupoteza kazi na hivo kuondoa uzembe na mambo mengine.
b) Kuwe na mikataba ya kazi zao mpya itakayoondoa mastahili yao kwenye kazi za zamani au mpya mara wanapotenguliwa. Kuendelea kumlipa mtu aliyetenguliwa ni matumizi mabaya ya fedha kwa mtu ambaye hana kiti cha kufanya!

Dhana ya kuwa kazi ya serikali ni ya kudumu si sahihi. Ndio chanzo cha ufanisi mbaya! Huku private sector ukitenguliwa bila kushushwa cheo unakwenda nyumbani!!
 
Hivi hawa wateule wa uwaziri huwaga wanasomaga mikataba na sheria za kimataifa au ni mavilaza tu yanayofikiria kuwa wao ni mwisho wa kila kitu. Mwigulu kasome ILO code of good practice ambazo serikali uliyopo wamesaini.
 
Hivi hawa wateule wa uwaziri huwaga wanasomaga mikataba na sheria za kimataifa au ni mavilaza tu yanayofikiria kuwa wao ni mwisho wa kila kitu. Mwigulu kasome ILO code of good practice ambazo serikali uliyopo wamesaini.
 
Itoshe kusema kuwa hii sheria ya kumlipa mtu kwa cheo asichokuwa nacho ilikuwa ya ovyo .
 
Inawezekana una mshahara huo ,lakini hiyo ni nzuri maana itakufanya uwajibike ili usije kurudi ulikotoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…