Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Watu wa Soka,
Umofia kwenu.
Nimekuwa nikipokea SMS nyingi na maswali kwenye mitandao ya kijamii kuhusu nini kimetokea kati yangu na Klabu ya Singida Fountain Gate ambayo nilikuwa naitumikia kama Msemaji na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano.
Kuweka rekodi sawa tu, sijafukuzwa kazi wala hapakuwahi kuwepo mgogoro wowote kati yangu na Klabu. Nimefanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kufikia maono ya klabu katika eneo la kuisemea, kujenga mahusiano chanya na kuiweka timu karibu na wadau.
Kilichotokea ni makubaliano tu ya kuvunja mkataba na tulifikia makubaliano hayo pande zote mbili. Hivyo nilipata baraka zote kutoka kwa uongozi wa klabu.
Kwa sasa nipo mbioni kusaini mkataba na klabu nyingine kubwa ambako naenda kutumia ujuzi na uzoefu nilioupata kama nilivyoeleza kwenye taarifa yangu kwa umma niliyoitoa tarehe 05/05/2024.
Asanteni.