Sikufukuzwa kazi Singida Fountain Gate, nilivunja mkataba kwa makubaliano

Sikufukuzwa kazi Singida Fountain Gate, nilivunja mkataba kwa makubaliano

Jicho la mwerevu huona jambo kabla ya kutokea (Wahenga walisema).

Ukweli ni kwamba, ulipiga picha. Ukaona Singida FG, inaenda kupitia hali ngumu hapo baadae.

Kabla ya msimu kutamatika, ukajitoa na kujiweka sokoni. Wewe ni kama parachichi linalotamani kuliwa. Wakati bado halijaiva, likaamua kujidondosha liminywe minywe mpaka litakapoiva.

Nakutakia kila la kheri kwenye majukumu yako mapya Singids BS.

Asante sana mkuu ila mbona umenifananisha na parachichi daah 😅
 
Kwa kuwa umeweka public lazima tukuulize sababu ni nini. Usimba na Yanga kwa sababu mtu wa Simba hawezi kamwe kuruhusiwa kufanya kazi Yanga, labda ajitoe akili kama Haji

Ooh sawa. Nilipata ofa kutoka Ihefu lakini haikunivutia nikaachana nayo. Ndio maana nikasema sitakuja kuisemea maana wengi walidhani kituo kinachofuata ni Ihefu.
 
Swali likiulizwa kwa kejeli linastahili kujibiwa kwa kejeli mkuu wangu
Lakini hapo kejeli iko wapi unatakiwa kuwa mstahamilivu kama ukiwa kwenye press ndio maana mnafeli mnageuka vituko badala ya weledi wasemaji au mafsa habari wa ajabu unawapa tanzania hawana tofauti na mashabiki wa vijiwe vya kahawa!
 
😅😅😅😅 mbona wewe hujawa mstahamilivu? Nimekujaribu kidogo tu umezidi kumwaga kashfa na kejeli. Kumbe nilikuwa sahihi
 
😅😅😅😅 mbona wewe hujawa mstahamilivu? Nimekujaribu kidogo tu umezidi kumwaga kashfa na kejeli. Kumbe nilikuwa sahihi
NIlijua utajibu vile sababu huwa mnajigeuza makocha wachezaji hapo hapo wapiga ngoma mtaani na vijisipika unategemea utajibu nini ukiulizwa malengo yenu!
 
Back
Top Bottom