Sikuwahi kujua majina ya wanyakyusa yana maana😀

Sikuwahi kujua majina ya wanyakyusa yana maana😀

Wakuu habari za asubuhi?

Nafika kazini asubuhi hii, namsalimu jirani yangu ananiambia Tuntufye.

Namuuliza hao si wanyakyusa, anasema majina yote ya wanyakyusa yana maana

Tuntufye ni - tumsifu[emoji3]
Gwamaka- mwenye nguvu

Embu wanyakyusa tupeni maana ya majina yenu?
Gwamaka kahiula huyu kama jina la msanii
 
  • Kissa - Huruma
  • Gwakisa - Mwenye huruma
  • Lugano - Upendo
  • Gwalugano - .....malizia
  • Tupeligwe - Tumepewa
  • Asajile - Amenisaidia/amenibariki
  • Andendekisye - Ametengeneza

Majina haya mengi ni ya kumtukuza Mungu(Kyala)kwa sababu kadhaa ambapo hizo sababu ndio unaziona kwenye jina, mathalani...

Asajile kwa kirefu ingekuwa Kyala asajile
Andendekyise kwa kirefu ingekuwa Kyala andendekyise (Mungu amenitengeneza)
Tupeligwe - Tuliyepewa na Mungu
Gwalugano - Mungu wa upendo
n.k
n.k
 
Back
Top Bottom