Silaha za Masafa Marefu Zinazomilikiwa na JWTZ

Unaamini kitu gani boss ?
Watu wanaoshangilia kupasua matofali uwanjani unadhani nikisema kitu wataamini. Kenya wana procurement kubwa za silaha wanafanya, kuna muda Obama alizuia wasiuziwe light helicopters ila Trump aliruhusu. Wamenunua MRAPs kutoka Uturuki mwaka huu, mwaka jana walianza kupokea ndege zao za Skytruck walinunua 14. Mwaka jana mwishoni pia walianza kuunda meli kwenye naval base yao, kama zinaundwa kwenye naval base maana yake hata meli za kivita wataunda, ni base kubwa zaidi in Sub-Saharan Africa.

Training zao naziamini zaidi na wanapokea za ziada kutoka UK na US waliopo kwao ingawa sipendi kuwaona pale. Hao si ndio zaidi wameifundisha Ukraine. Kingine Kenya ni nchi yenye changamoto kiulinzi na inakuwa na missions chache ndogondogo kwa hiyo experience yao ni tofauti na nchi isiyo na changamoto imetulia. Duniani huwa naamini nchi iliyo na changamoto mara zote inapata uzoefu na kuwa standby. Kilichowafanya Kenya wanunue silaha zaidi na kubadilisha mbinu za mafunzo, kununua communication gear na kuunda dedicated special force yenye silaha za uhakika ni kufeli kwa jeshi lake mwanzoni mwa kupambana na Al Shabaab. Aibu waliyopata pale Westgate usitarajie itajirudia tena, wala usitarajie kuna nchi hapa East Africa ina uwezo wa kupambana na tukio kama lile kuizidi Kenya.

Mambo ni mengi
 
"Miaka ya 2000 kuna zile zilizokuwa zinalipuka zenyewe kule Mbagala."

Una uhakika zililipuka zenyewe??
 
Narudia kukwambia bado una safari ndefu kama unaamini North Korea ana hypersonic missiles na Marekani hana kama ulivyosema. North Korea walisema wamefanya testing, kufanya test na kuwa na silaha ni vitu viwili tofauti kabisa. Urusi anayo Sukhoi Su-47 Berkut kama demonstration fighter na kashindwa kufanya production, anayo T-14 Armata tangu 2015 anaionyesha kwenye parade hadi leo hajafanya production. Sasa kama ungehesabu tangu mwishoni mwa miaka ya 1990s ilipoanza kuruka Berkut si hadi leo ungesema Urusi anazo forward swept wing supersonic fighters. Au tangu 2015 si ungesema Urusi ana T-14 Armata zipo tiyari kupigana. Unaweza shangaa kina Japan, UK na wengine wenye development pia wanapata hypersonic missile kabla ya North Korea, ndio maana hatuhesabii prototype, demonstration au testing vehicle kama silaha tiyari kwa matumizi.

Marekani mwenyewe anafanya testing na mwaka huu wametumia B-52 kurusha hypersonic cruise missile na ikafanikiwa. Hao wote wapo kundi moja la testing, sio North Korea amefanya test unasema anazo alafu Marekani amefanya test vilevile unasema hana. Wote kwa sasa hawana hizo silaha.

Wenye hizo silaha kwa sasa ni China na Urusi tu ndio ukiwaanzishia vita hata leo wanazitumia. Hao North Korea wametengeneza prototype ya testing tiyari unashangilia wana silaha. Kwenye inventory yao si ajabu hupati hata hypersonic missile zaidi ya moja, its either ipo kwenye factory inatengenezwa au imepelekwa kwenye arsenal kusubiri test launch nyingine.
 
Unasema tunafanana na nchi kama Uswizi unajua inatumia gharama kiasi gani kwenye ulinzi? Last year iliagiza F-35 stealth fighters zaidi ya 30 kwa gharama zaidi ya $5 billion na hapo inaongezea ndege aina nyingine ilizonazo. Na unajua Uswizi imewekeza kiasi gani kwenye diplomasia na ujasusi. Haitokei tu ikawa salama kuna jitihada nyingi za makusudi na za gharama inafanya, na sisi hatufanyi hizo
 
OOH! KENYA.
 
Balaaaaa
 
[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
 
Maana ya ku'test' ni nini? Unapo'test' na kufanikiwa, si una hiari ya kutengeneza ulicho'test'?
Korea kafanya 'test' na amefanikiwa. Kwa hiyo unataka leo aje akwambie ameanza kutengeneza ama hapana?

Hujasema kama alipo'test' ilionekana kuwa ameshindwa. Kwa hiyo ana hiari ya kutengeneza silaha hiyo.

Inaonekana bado unayo kasumba ya kudhani kwamba ni hayo mataifa unayoyahusudu tu ndiyo yenye uwezo wa kutengeneza vitu pekee. Hii ni kasumba tu, inafaa uondokane nayo.
 
Kawaida mtu akishajua weakness yko ni rahisi sana kukushambulia. Lakini hao US na NATO sioni wanachokifanya.
Si kama ilivyokuwa Iraq , Afghanistan na nchi zingine?
 
Saa unasemaje Marekani hana hizo silaha wakati yeye mwenyewe kafanya test na kufanikiwa? Why successful testing ya North Korea useme wana hypersonic missiles alafu ya Marekani useme hawana?

Kwenye silaha prototype na type ni vitu viwili tofauti. Russia alitengeneza Sukhoi Su-57 prototypes jumla ya 10 kwa ajili ya testing kwa vipindi tofauti tofauti, hata alipokuwa na prototype ya 10 bado Su-57 hatukuwa tunahesabu kwenye silaha maana hazipo. North Korea wameanza kurusha makombora kabla ya mwaka 2000 ila ICBM ya kwanza walikuwa nayo mwaka 2017, walifanya test za nuclear weapons 6 kiujumla. Itakuwa wewe uliposikia wametest mara ya kwanza ulisema wana nukes tiyari.

Kuna nchi nyingi zina projects za hypersonic missiles ila ni nchi mbili tu China na Russia zenye hizo silaha kwa sasa. Kipanya ana prototype ya gari lake, lile haliuzwi wala kwenye soko halipo. Tutaanza kuhesabu magari yake yatakapokuwa kwenye production, tungehesabu hili hapa basi Tanzania kungekuwa na model ya gari ile iliyotengenezwa na Nyumbu miaka ya Nyerere uko na ambayo haipo sokoni.
 
Kaka kuwa specific kwamba Russia wamepitwa na nani? nitajie nchi tano tu zinazoongoza kwa utengenezaji wa siraha za kisasa za kivita.Kwanza Russia hajakutana stiff resistance ya kupelekea yeye kutumia modern tech yake kwenye siraha.
 
Mkuu, tusizungushane bure. Unayokazania hapa ni 'semantics' tu zisizokuwa na maana yoyote.
Kama 'prototype' ya kitu ipo, na imekwishaonyeshwa kwamba kitu hicho kinawezekana kutengenezwa, ni swala la maamuzi tu la mhusika kutengeneza au asitengeneze ikitegemea na mahitaji yaliyopo.
Kama Korea Kaskazini, katengeneza 'prototype', na kuijaribu, na kuona inafanya kazi, na mahitaji yake yakijulikana ni ya haraka kwa ulinzi wake, wewe ni nani ung'ang'anie kwamba hana. Kwa hiyo hapa unaweza kudai pia kwamba hana silaha za nuklia, kwa vile amekuwa akifanya majaribio yake? Unadai pia kuwa hana 'ICBM', na hana makombora hayo?

Vipi bwana, mbona unajitoa ufahamu hivyo?

Sawa, unaweza kuwa na uelewa kiasi juu ya haya mambo ya masilaha, lakini hilo halikupi ujuaji wa kujua ni nani anazo na nani hana, na ukijua 'prototype' tayari zipo. Maamuzi ya kutengeneza ni ya nchi husika, ikizingatia mahitaji ya nchi yenyewe.
 
Kaka kuwa specific kwamba Russia wamepitwa na nani? nitajie nchi tano tu zinazoongoza kwa utengenezaji wa siraha za kisasa za kivita.Kwanza Russia hajakutana stiff resistance ya kupelekea yeye kutumia modern tech yake kwenye siraha.
Hata Ujerumani inawazidi. Hawajapata stiff resistance huku majenerali wanauwawa kama makoplo? Kazi yao kubwa ni kurusha makombora ya kuuwa raia na kubomoa makazi ya watu lakini wanapokutana vita ya ana kwa ana hawana ubavu. Vifaru vinabomolewa kama vibuyu
 
Kaka hii ni kwa mujibu wa takwimu au maelezo yako?!😃
 
Afadhali ww umewatolea tongotongo watu maana mimi nimesoma nikakosa nianzie wapi ila mwenye akili na aelewe
 
Kaka hii ni kwa mujibu wa takwimu au maelezo yako?!😃
Unajua Urusi imepoteza majenerali na makanali wangapi? Na ni vifaru vingapi vinaozea kwenye ardhi ya Ukraine leo?

Iwapo Ukraine ingekuwa na jeshi kubwa la kupambana sehemu mbalimbali sasa hivi Urusi wangekuwa taabuni sana. Ila Advantage kwa Urusi ni kwa vile wana wapiganaji wengi sana walioanza kwa kuizunguka Ukraine yote, na jeshi la Ukraine haiwezi kusambazwa sehemu zote hizo. Lakini pale jeshi la Ukraine linapopigania, Urusi wanapata tabu sana. Watatumia makombora ya kubomoa makazi ya watu na miundo mbinu lakini wanapokutana na wanaume wenzao uso kwa uso wanakunja mkia.
 
Urusi alianza Marekani akafatia nimekuelewa kwa hili,kwa mtazamo wako huoni kuwa Urusi ni bora kuliko Marekani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…