T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Watu wanaoshangilia kupasua matofali uwanjani unadhani nikisema kitu wataamini. Kenya wana procurement kubwa za silaha wanafanya, kuna muda Obama alizuia wasiuziwe light helicopters ila Trump aliruhusu. Wamenunua MRAPs kutoka Uturuki mwaka huu, mwaka jana walianza kupokea ndege zao za Skytruck walinunua 14. Mwaka jana mwishoni pia walianza kuunda meli kwenye naval base yao, kama zinaundwa kwenye naval base maana yake hata meli za kivita wataunda, ni base kubwa zaidi in Sub-Saharan Africa.Unaamini kitu gani boss ?
Training zao naziamini zaidi na wanapokea za ziada kutoka UK na US waliopo kwao ingawa sipendi kuwaona pale. Hao si ndio zaidi wameifundisha Ukraine. Kingine Kenya ni nchi yenye changamoto kiulinzi na inakuwa na missions chache ndogondogo kwa hiyo experience yao ni tofauti na nchi isiyo na changamoto imetulia. Duniani huwa naamini nchi iliyo na changamoto mara zote inapata uzoefu na kuwa standby. Kilichowafanya Kenya wanunue silaha zaidi na kubadilisha mbinu za mafunzo, kununua communication gear na kuunda dedicated special force yenye silaha za uhakika ni kufeli kwa jeshi lake mwanzoni mwa kupambana na Al Shabaab. Aibu waliyopata pale Westgate usitarajie itajirudia tena, wala usitarajie kuna nchi hapa East Africa ina uwezo wa kupambana na tukio kama lile kuizidi Kenya.
Mambo ni mengi