Simba Bob Junior wa Serengeti apinduliwa na kuuawa

Simba Bob Junior wa Serengeti apinduliwa na kuuawa

Wao kwa wao itabidi wapigane na kuuana ili abaki mmoja tu
Wapo wengine huwa wanakaa pamoja bila shida wanaform coalition yaani ile ya wafalme wawili, watatu au wanne. Inategema na wamekua vipi.

Kuna Documentary: Lion brothers : Cubs to Kings (National Geographic Wild) itafute hii utazame story ya simba wawili mtu na kaka yake ambao wamekua pamoja na hawakutengana na wakaanzisha kingdom yao na kuitawala pamoja.
 
Wapo wengine huwa wanakaa pamoja bila shida wanaform coalition yaani ile ya wafalme wawili, watatu au wanne. Inategema na wamekua vipi.

Kuna Documentary: Lion brothers : Cubs to Kings (National Geographic Wild) itafute hii utazame story ya simba wawili mtu na kaka yake ambao wamekua pamoja na hawakutengana na wakaanzisha kingdom yao na kuitawala pamoja.
Hao ni simba brothers, hao siku zote huishi pamoja, lakini lijapo swala la baba na vijana wake wa kiume kamwe huwa hawaishi pamoja.
Watoto wa Simba wakikua, lile dume (baba yao) huwafukuza wakajitegemee, lakini majike huwa hawafukuzwi.
Wale watoto wakishapata nguvu huko ndipo hupanga kuja kufanya mapinduzi ya kumuua baba yao ili wamiliki territory, ingawa wengine hupotezea na kuendelea maisha yao.
 
Nature.... hayo ndio maisha halisi ya Simba, mwanaume ukikua unafukuzwa kwenye ukoo, na ili kuanza familia na kupata eneo lako unaenda kuvamia ukoo mwingine, unapigana na ukiweza kuwakimbiza au kuua wanaume wote unachukua majike, kama yana watoto unaua wote then unaanzisha ukoo wako, na simba wengine vijana waliofukuzwa watakuwa wanakuvamia kila wakati ili kuchukua majike yako na eneo lako, ukishindwa ndio umepoteza familia nzima na watoto wako wote wanauliwa na majike kuplewa na ndume iliyoshinda, wana maisha magumu sana na ukiwa soft kama wanaume wa JF umekwisha
Kweli yani ukiwa soft umeisha.Nawaza tu yani mashoga wangekuwa jamii ya Simba wangekuwa washaisha.
 
Hapana kwa mujibu wa vitabu vya wanyama wote hawatowajibika kwa Lolote kwa kuwa hawana hakili atakaewajibika kwenda peponi na motoni ni Binadam kwa sababu ana akili
Wanyama hawana akili kivp, una uhakika hawana akil , au ni story za kusikia tu.
 
Simba wanamalizana sana wenyewe kwa wenyewe kuliko wanavyomalizwa na wanadamu.
Hapo umeutaja mto Ngarenanyuki kuwa upo Magharibi mwa Serengeti, nadhani utakuwa umechanganya kidogo, kumbukumbu zangu zinaniambia mto Ngarenanyuki upo ndani ya ya Arusha National Park
Mto huo inaishia hapo tu? Kwani mto Nile unaopita Uganda ukifika Egypty sio mto Nile? Kama geographically hauflow kwenda huko happy sawa.
 
SAD NEWS…

Taarifa ya kifo cha Simba maarufu huko Serengeti ajulikanae kama Bob imezistua Nyoyo za Watu wengi Duniani ambao walifanikiwa kumuona Simba huyo ambae alikuwa kipenzi cha Watu kwa kuwa hakuwa na tabia za kujificha wala kukwepa Camera.

Bob alikutwa na umauti baada ya kundi la Simba Watatu kumvamia na kutimiza Lengo lao la muda mrefu la kuuangusha utawala wa Bob na kusimika ufalme wao porini hapo.

Simba hao Watatu ambao Bob aliwalea tangu wakiwa wachanga inasemekana walishafanya mapinduzi mara kadhaa ya kutaka kuuangusha utawala wa Bob lakini mara zote walikutana na upinzani mkali na hata kukimbizwa maeneo hayo.

Bob ambae alikuwa mtemi na mtawala wa eneo la Namiri aliongoza Simba wa eneo hilo kwa kipindi kirefu sana na alikwepa mapinduzi ya aina mbalimbali kwa vipindi tofauti huko Mashariki ya Serengeti.

Utawala wa Bob ulikuja baada ya kumpindua na kumuua Baba yake ambae alikuwa maarufu pia kwa Watalii Duniani ambae alifahamika kama C-Boy.

Umauti ulimkuta C-Boy mwendo wa Jioni pembezoni mwa Mto Ngare Nanyuki ambapo wakiwa wawili tu Bob alifanikiwa kufanya mapinduzi hayo tukufu na kuumaliza utawala wa Baba yake.

Pumzika kwa amani Bob.
Vita ulivipigana na mwendo umeumaliza.

View attachment 2549829
View attachment 2549828
View attachment 2549827
Wanashtakiwa TANAPA au wapi?
 
Back
Top Bottom