Simba hatarini kupokonywa kombe; TFF kufungiwa na FIFA kwa sababu ya Yanga

Ndugu wanampira nimepitia maoni yenu yote na kugundua kuwa baadhi ya wachangiaji wamenibatiza kuwa utopolo kwa sababu wanazozijua wao. Mimi nimefungua huu uzi kama angalizo kwa TFF kwamba ikiwa hawatakuwa waangalifu Yanga wanaweza wakawatokea puani kama wataamua kuwakazia. Nina sababu lukuki na baadhi nimeishazitoa hapa lakini hakuna mtu anayenisikiliza. Napenda kujitoa kwenye kundi la utopolo ambalo baadhi yenu mmeamua kuniweka. Andiko hili nimelitoa kama mchambuzi sio kama mwanamsimbazi au mwanautopolo. Naomba nieleweke hivyo.

Sababu au dukuduku zinazonifanya niwe na wasiwasi kuhusu haya niliyoyaandika hapa ni hizi zifuatazo:

1. Kama Yanga walikuwa na makosa kutopeleka timu kiwanjani mbona hawakuadhibiwa? Kwa sababu hii, wanaweza wasipeleke timu tena tarehe 3/7 na TFF au serikali hawawezi kuwafanya lolote kwa kuwa kama wangekuwa na makosa wangechukuliwa hatua za kinidhamu tangu siku ile walipogoma kupeleka timu kiwanjani.

2. Kwa kuwa TFF hawakuwapa adhabu immediately maana yake ni kwamba hiyo adhabu (kama ipo) tayari imeisha expire. So, TFF hawawezi kuwaadhibu Yanga wala kuwapa pointi Simba na ikiwa watafanya hivyo, Yanga watawakaanga mapema sana.

3. Pesa za mashabiki walioingia kiwanjani kutazama mechi zitarejeshwa lini? Kumbuka hata waziri mkuu amewahi kuongelea jambo hili lakini TFF wameziba masiko yao viazi.

4. Gharama za maandalizi kwa timu zote mbili zitalipwa na nani na lini? Timu zote mbili tayari wameandaa bill ya maandalizi ijapokuwa bado hawajaiwasilisha rasmi TFF.

5. Kitendo cha serikali kulazimisha mechi isogezwe mbele kwa sababu za kipuuzi kabisa maana yake ni kuwa serikali imeingilia mambo ya mpira kinyume na sheria za FIFA. Kwa maana hii, kama Yanga wakiamua kupeleka hili jambo CAS au FIFA na kulishupalia kisawasawa, TFF hawana pa kutokea.....watafungiwa tu....na kisha Yanga watalipwa mabilioni ya dola kama fidia kwa usumbufu. Tatizo kuna baadhi ya watu hawajui hili, wao wanajua sheria za TFF tu. Wanashangaza 😳 😳 😳 😳

Ni hayo tu.
 
Hapo nimekuelewa vizuri sana mkuu. Lakini Simba walishindwa kupeleka timu baada ya Yanga kuondoka kiwanjani. Wangepeleka timu icheze na nani wakati Yanga wameishasepa kitambo? Na pia hapakuwepo na marefa wa kuchezesha mchezo.
Sheria inasema muda wa mchezo ukikaribia ingiza timu uwanjani, na baada ya muda wa mchezo kufika subiria nusu saa uwanjani kama.timu haijaingia uwanjani ondoa timu uwanjani na inahesabika mpinzani hajafika mchezoni, Yanga waliondoa timu saa 17:30 hapo Simba anahesabika amekimbia mechi.
 
Mechi inaweza kuahirishwa au kusohezwa mbele chini ya masaa 24 kama tu

■ Kuna tishio la kigaidi au bomu uwanjani

■ Hali ya hewa kutoruhusu mchezo kuchezwa.

■ Majanga ya ya kidunia kama tetemeko la ardhi au kimbunga kikali.

Lakini siyo nje ya hapo
 
Tatizo simba huyu ameenda pole mno hadi ataikosa nyama au atakuta imeioza. Tazama nchi zote duniani ligi zao zimefika tamati lakini ligi hii ya TFF inatarajiwa kufika tamati mwaka ujao. Haya ni maajabu ya dunia ndugu yangu Bujibuji .
Vipi ligi ya Misri?
 
Endeleeni kuamini hivyo na mawazo yenu ya kiutopolo. Mmeshindwa mpira uwanjani mnaaanza kulalama. Mapimbi kweli nyie. [emoji38][emoji38][emoji38]
Kucheza hatuchezi sisi ila wewe ndio unaoaniki nankuchukia![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Kanuni imesema emergency ambayo TFF wanalidhia kuwa ni dharura na muhimu. Si hizo tu.
Tukubali kulikuwa na hali ya kukariri badala ya kuelewa kanuni.

Kwa hiyo ikitokea uwanja unawaka moto au kubomoka, mechi itaendelea kwa kuwa haijatajwa?
 
Wakikwambia kulikuwa na shughuli ya kiserikali hivyo watu wa usalama wakaelekezwa huko kwanza na hawakuwa na watu wa kutosha kuangalia usalama uwanjani, kwenye shughuli ya kiserikali na jamii kwa pamoja. Wewe una lipi la kupinga?
Hiyo shughuli ya kiserikali ilikuwa ni ya ghafla au ilipangwa muda mrefu?

Kwani kulikuwa na ugumu gani wa kutoa ahirisho la mechi siku moja kabla?
 
Hili jambo sioni kama litafika huko. Siku ya mchezo timu ambayo haifiki uwanjani hupewa adhabu na iliofika hupewa ushindi. TFF na board ya ligi ni mbuzi wa kafara ktk mchezo wa kwanza ulio ahirishwa. Mhusika ni serikali kupitia wizara ya michezo ilio ona ni busara kusogeza mbele mchezo ili watanzania washuhudie uzinduzi wa kitabu cha 'baba' na 'mwana' kumzawadia gari.
.
 
Huoni kuwa, kwa kauli yako hii, TFF ni wapuuzi wa kupindukia? Kwanini TFF walikubali kuahirisha mchezo kwa sababu FEKI kama hii?
 
Mjinga ww ambae unadandia treni kwa mbili huu uzi uliandikwa jana usiku na sehem ya team aliweka team 20 uliwa waliouona mapema so unakua boyaboya tu
Wewe ni 'mjinga', na kiasi mjuaji. Mbona kaandika timu zipo 18? Kuandika timu itacheza michezo 34 hujaelewa?
 
Mjinga ww ambae unadandia treni kwa mbili huu uzi uliandikwa jana usiku na sehem ya team aliweka team 20 uliwa waliouona mapema so unakua boyaboya tu
Afu wee jamaa mbona unashupalia sana hii hoja wakati kila mtu anajua ligi ina timu 18? Sawa tumekuelewa. Hebu changia hoja sasa.
 
Subiri tarehe 3 tuutoe huo mwiko matakoni 100% najua mtaleta team
Afu wee jamaa mbona unashupalia sana hii hoja wakati kila mtu anajua ligi ina timu 18? Sawa tumekuelewa. Hebu changia hoja sasa.
 
Subiri tarehe 3 tuutoe huo mwiko matakoni 100% najua mtaleta team
Mbona wee chalii unapenda kuandika matusi kiasi hiki? Hivi huwezi kuchangia hoja bila kuweka matusi? Bora tu shule zifunguliwe mrudi shule mkapambane na walimu wenu tumewachoka.
 
Mnazingua sana mnajikuta viazi mnaleta tu nyuzi ambazo hazina mashiko sisi tunategema jf kukuta vitu smart sa nikikutana na huu utopolo nashindwa kujizuia
Mbona wee chalii unapenda kuandika matusi kiasi hiki? Hivi huwezi kuchangia hoja bila kuweka matusi? Bora tu shule zifunguliwe mrudi shule mkapambane na walimu wenu tumewachoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…