DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Mimi ni mmoja wa watu wachache sana ambao tuliitabiria makubwa Simba kabla hata msimu huu haujaanza. Kwa maana hiyo mimi ni mmoja wa watu wachache ambao tuna kibali cha kuona na kutafsiri kwa usahihi sehemu ambapo klabu au timu imeteleza.
Wakati timu ikijiandaa kwenda Morocco kwa ajili ya mechi ya kwanza ya fainali ya CAFCC, wapenzi na mashabiki wa Simba tuna matarajio makubwa katika fainali hii ili kombe hili libaki Tanzania.
Bila kusema mengi, pamoja na kwamba hata mchezo mmoja wa fainali bado haujachezwa ila kuna makosa mawili makubwa ya kiufundi yamefanyika ambayo kuna uwezekano yakaenda kuigharimu Simba katika harakati zake za ubingwa huu wa CAFCC.
Nitahifadhi na nisingependa kutaja hayo makosa waziwazi kwa wakati huu ili yasije yakazua mijadala ambayo kwa kipindi hiki haina faida sana.
Kwa bahati mbaya moja kati ya makosa haya, klabu haipo kwenye nafasi ya kulirekebisha ila moja lipo ndani ya uwezo wa klabu kama utashi wa kulifanyia kazi utakuwepo. Shida ni kwamba sioni hata kama kuna mtu ndani ya klabu amelitilia maanani au ameona umuhimu wake kwa hiyo najua hili nalo halitafanyiwa kazi na ndiyo maana yananitia wasiwasi. Najua hata nikijaribu kulipenyeza kwa uongozi hawatanielewa au kutaka kulifanyia kazi.
Iwapo Simba itakosa ubingwa wa CAFCC, nitarudi katika uzi huu nitaje hizo sababu mbili kuu.
Nimalizie kwa kusema, nafasi ya Simba kuwa bingwa wa CAFCC msimu huu bado ni kubwa sana na dua na maombi ya wanasimba wote yanaelekezwa katika kufanikisha hilo.